Zaburi Chapter 72

For English

Read Zaburi Chapter 72 Online

Read Zaburi Chapter 72 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of Zaburi in the Old Testament. Browse every verse with easy chapter navigation, continue to the next chapter, or explore the complete Book of Zaburi and the Holy Bible online.

Choose a Chapter

Zaburi 72

Sura 72

1. Ee Mungu, mpe mfalme hukumu zako, Na mwana wa mfalme haki yako.

2. Atawaamua watu wako kwa haki, Na watu wako walioonewa kwa hukumu.

3. Milima itawazalia watu amani, Na vilima navyo kwa haki.

4. Atawahukumu walioonewa wa watu, Atawaokoa wahitaji, atamseta mwenye kuonea.

5. Watakuogopa wakati wote wa kudumu jua, Na wakati wa kung'aa mwezi kizazi hata kizazi.

6. Atashuka kama mvua juu ya majani yaliyokatwa, Kama manyunyu yainyweshayo nchi.

7. Siku zake yeye, mtu mwenye haki atasitawi, Na wingi wa amani hata mwezi utakapokoma.

8. Na awe na enzi toka bahari hata bahari, Toka Mto hata miisho ya dunia.

9. Wakaao jangwani na wainame mbele zake; Adui zake na warambe mavumbi.

10. Wafalme wa Tarshishi na visiwa na walete kodi; Wafalme wa Sheba na Seba na watoe vipawa.

11. Naam, wafalme wote na wamsujudie; Na mataifa yote wamtumikie.

12. Kwa maana atamkomboa mhitaji aliapo, Na mtu aliyeonewa iwapo hana msaidizi.

13. Atamhurumia aliye dhaifu na maskini, Na nafsi za wahitaji ataziokoa.

14. Atawakomboa nafsi zao na kuonewa na udhalimu, Na damu yao ina thamani machoni pake.

15. Basi na aishi; Na wampe dhahabu ya Sheba; Na wamwombee daima; Na kumbariki mchana kutwa.

16. Na uwepo wingi wa nafaka Katika ardhi juu ya milima; Matunda yake na yawaye-waye kama Lebanoni, Na watu wa mjini wasitawi kama majani ya nchi.

17. Jina lake na lidumu milele, Pindi ling'aapo jua jina lake liwe na wazao; Mataifa yote na wajibariki katika yeye, Na kumwita heri.

18. Na ahimidiwe Bwana, Mungu, Mungu wa Israeli, Atendaye miujiza Yeye peke yake;

19. Jina lake tukufu na lihimidiwe milele; Dunia yote na ijae utukufu wake. Amina na Amina.

20. Maombi ya Daudi mwana wa Yese yamekwisha.

About Zaburi Chapter 72

Read Zaburi Chapter 72 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of Zaburi in the Old Testament. Continue reading with the chapter navigation above or explore the complete book.

Book Information

Book: Zaburi
Chapter: 72
Testament: Old Testament

How to Read this Chapter

Use the Previous and Next Chapter buttons to continue reading Zaburi. You can also adjust the font size for comfortable reading and browse other books of the Bible using the navigation links.

https://www.youtube.com/watch?v=rzsT_Q3KLzE

More Resources

Continue Reading the Bible

Continue reading Zaburi Chapter 72 and explore every book, chapter and verse of the Holy Bible. Use the navigation links above and below to move through the Scriptures with ease.

Frequently Asked Questions

What is Zaburi Chapter 72?

Zaburi Chapter 72 is part of the Book of Zaburi in the Holy Bible.

Can I read this chapter online?

Yes. You can read the complete Zaburi Chapter 72 online for free with easy chapter navigation.

More Chapters from Agano la Kale

  1. Zaburi Chapter 1
  2. Habakuki Chapter 3
  3. Ayubu Chapter 1
  4. Zaburi Chapter 2
  5. Kutoka Chapter 11
  6. Kutoka Chapter 2
  7. Ayubu Chapter 4

Explore More from Zaburi

  1. Zaburi Chapter 145
  2. Zaburi Chapter 18
  3. Zaburi Chapter 46
  4. Zaburi Chapter 120
  5. Zaburi Chapter 105
  6. Zaburi Chapter 3
  7. Zaburi Chapter 92

Related Chapters & Readings

  1. Malaki Chapter 4
  2. Ezekieli Chapter 34
  3. 1 Wathesalonike Chapter 1
  4. Yeremia Chapter 37
  5. Ruthu Chapter 2
  6. 1 Timotheo Chapter 4
  7. Zaburi Chapter 65
Share Your Love

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *