Read Zaburi Chapter 109 Online
Read Zaburi Chapter 109 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of Zaburi in the Old Testament. Browse every verse with easy chapter navigation, continue to the next chapter, or explore the complete Book of Zaburi and the Holy Bible online.
Choose a Chapter
Zaburi 109
Sura 109
1. Ee Mungu wa sifa zangu, usinyamaze,
2. Kwa maana wamenifumbulia kinywa; Kinywa cha mtu asiye haki, cha hila, Wamesema nami kwa ulimi wa uongo.
3. Naam, kwa maneno ya chuki wamenizunguka, Wamepigana nami bure.
4. Badala ya upendo wangu wao hunishitaki, Ijapokuwa naliwaombea.
5. Wamenichukuza mabaya badala ya mema, Na chuki badala ya upendo wangu.
6. Uweke mtu mkorofi juu yake, Mshitaki asimame mkono wake wa kuume.
7. Katika kuhukumiwa ataonekana hana haki, Na sala yake itadhaniwa kuwa ni dhambi.
8. Siku zake na ziwe chache, Usimamizi wake na atwae mtu mwingine.
9. Wanawe na wawe yatima, Na mkewe na awe mjane.
10. Kutanga na watange wanawe na kuomba, Watafute chakula mbali na mahame yao.
11. Mdai na anase vitu vyote alivyo navyo, Wageni na wateke mapato ya kazi yake.
12. Asiwe na mtu wa kumfanyia fadhili, Wala mtu wa kuwahurumia yatima wake.
13. Wazao wake waangamizwe, Jina lao likafutwe katika kizazi cha pili.
14. Uovu wa baba zake ukumbukwe mbele za Bwana, Na dhambi ya mamaye isifutwe.
15. Ziwe mbele za Bwana daima, Aliondoe kumbukumbu lao duniani.
16. Kwa kuwa hakukumbuka kutenda fadhili, Bali alimfukuza mnyonge na mhitaji, Hata akamfisha mtu aliyevunjika moyo,
17. Naye alipenda kulaani, nako kukampata. Hakupendezwa na kubariki, kukawa mbali naye,
18. Alijivika laana kana kwamba ni vazi lake. Ikamwingilia moyoni kama maji, Na kama mafuta mifupani mwake.
19. Na iwe kwake kama vazi ajivikalo, Na kama mshipi ajifungao daima.
20. Ndiyo malipo ya washitaki wangu toka kwa Bwana, Na ya hao wanaoisingizia nafsi yangu mabaya.
21. Na Wewe, MUNGU, Bwana, unitendee kwa ajili ya jina lako, Kwa kuwa fadhili zako ni njema uniokoe.
22. Kwa maana mimi ni mnyonge na mhitaji, Na moyo wangu umejeruhi ndani yangu.
23. Ninapita kama kivuli kianzacho kutoweka, Ninapeperushwa kama nzige.
24. Magoti yangu yamedhoofu kwa kufunga, Na mwili wangu umekonda kwa kukosa mafuta.
25. Nami nalikuwa laumu kwao, Wanionapo hutikisa vichwa vyao.
26. Ee Bwana, Mungu wangu, unisaidie, Uniokoe sawasawa na fadhili zako.
27. Nao wakajue ya kuwa ndio mkono wako; Wewe, Bwana, umeyafanya hayo.
28. Wao walaani, bali Wewe utabariki, Wameondoka wao wakaaibishwa, Bali mtumishi wako atafurahi.
29. Washitaki wangu watavikwa fedheha, Watajivika aibu yao kama joho.
30. Nitamshukuru Bwana kwa kinywa changu, Naam, nitamsifu katikati ya mkutano.
31. Maana atasimama mkono wa kuume wa mhitaji Amwokoe na wanaoihukumu nafsi yake.
About Zaburi Chapter 109
Read Zaburi Chapter 109 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of Zaburi in the Old Testament. Continue reading with the chapter navigation above or explore the complete book.
Book Information
Book: Zaburi
Chapter: 109
Testament: Old Testament
How to Read this Chapter
Use the Previous and Next Chapter buttons to continue reading Zaburi. You can also adjust the font size for comfortable reading and browse other books of the Bible using the navigation links.
More Resources
Continue Reading the Bible
Continue reading Zaburi Chapter 109 and explore every book, chapter and verse of the Holy Bible. Use the navigation links above and below to move through the Scriptures with ease.
Frequently Asked Questions
What is Zaburi Chapter 109?
Zaburi Chapter 109 is part of the Book of Zaburi in the Holy Bible.
Can I read this chapter online?
Yes. You can read the complete Zaburi Chapter 109 online for free with easy chapter navigation.
More Chapters from Agano la Kale
- Zaburi Chapter 1
- Habakuki Chapter 3
- Ayubu Chapter 1
- Zaburi Chapter 2
- 1 Samweli Chapter 1
- Kutoka Chapter 11
- Kutoka Chapter 2
Explore More from Zaburi
- Zaburi Chapter 54
- Zaburi Chapter 134
- Zaburi Chapter 136
- Zaburi Chapter 78
- Zaburi Chapter 23
- Zaburi Chapter 75
- Zaburi Chapter 65