Zaburi Chapter 44

For English

Read Zaburi Chapter 44 Online

Read Zaburi Chapter 44 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of Zaburi in the Old Testament. Browse every verse with easy chapter navigation, continue to the next chapter, or explore the complete Book of Zaburi and the Holy Bible online.

Choose a Chapter

Zaburi 44

Sura 44

1. Ee Mungu, tumesikia kwa masikio yetu Baba zetu wametuambia, Matendo uliyoyatenda siku zao, siku za kale.

2. Wewe kwa mkono wako uliwafukuza mataifa, Ukawakalisha wao. Wewe uliwatesa watu wa nchi, Ukawaeneza wao.

3. Maana si kwa upanga wao walivyoimiliki nchi, Wala si mkono wao uliowaokoa; Bali mkono wako wa kuume, naam, mkono wako, Na nuru ya uso wako, kwa kuwa uliwaridhia.

4. Ee Mungu, Wewe ndiwe mfalme wangu, Uagize mambo ya wokovu kwa Yakobo.

5. Kwa nguvu zako tutawaangusha watesi wetu; Kwa jina lako tutawakanyaga watupingao.

6. Maana sitautumainia upinde wangu, Wala upanga wangu hautaniokoa.

7. Bali Wewe ndiwe uliyetuokoa na watesi wetu; Na watuchukiao umewaaibisha.

8. Tumejisifia Mungu mchana kutwa, Na jina lako tutalishukuru milele.

9. Lakini umetutupa, umetufedhehesha, Wala hutoki na majeshi yetu.

10. Waturudisha nyuma tukampa mtesi kisogo, Na watuchukiao wanajipatia mateka.

11. Umetutoa kama kondoo tuwe chakula, Na kututawanya kati ya mataifa.

12. Wawauza watu wako bila kupata mali, Wala hukupata faida kwa thamani yao.

13. Umetufanya kuwa lawama kwa jirani zetu, Mzaha na dhihaka kwao wanaotuzunguka.

14. Umetufanya kuwa mithali kwa mataifa, Sababu ya kutikisa kichwa kwa watu wa nchi.

15. Mchana kutwa fedheha yangu i mbele yangu, Na haya ya uso wangu imenifunika,

16. Kwa sauti ya mwenye kulaumu na kukufuru, Kwa sababu ya adui na mjilipiza kisasi.

17. Haya yote yametupata, bali hatukukusahau, Wala hatukulihalifu agano lako.

18. Hatukuiacha mioyo yetu irudi nyuma, Wala hatua zetu hazikuiacha njia yako.

19. Hata utuponde katika kao la mbwa-mwitu, Na kutufunika kwa uvuli wa mauti.

20. Ikiwa tumelisahau jina la Mungu wetu, Au kumnyoshea mungu mgeni mikono yetu;

21. Je! Mungu hatalichunguza neno hilo? Maana ndiye azijuaye siri za moyo.

22. Hasha! Kwa ajili yako tunauawa mchana kutwa; Tunafanywa kondoo waendao kuchinjwa.

23. Amka, Bwana, mbona umelala? Ondoka, usitutupe kabisa.

24. Mbona unatuficha uso wako, Na kusahau kuonewa na kudhulumiwa kwetu?

25. Maana nafsi yetu imeinama mavumbini, Tumbo letu limegandamana na nchi.

26. Uondoke, uwe msaada wetu, Utukomboe kwa ajili ya fadhili zako.

About Zaburi Chapter 44

Read Zaburi Chapter 44 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of Zaburi in the Old Testament. Continue reading with the chapter navigation above or explore the complete book.

Book Information

Book: Zaburi
Chapter: 44
Testament: Old Testament

How to Read this Chapter

Use the Previous and Next Chapter buttons to continue reading Zaburi. You can also adjust the font size for comfortable reading and browse other books of the Bible using the navigation links.

https://www.youtube.com/watch?v=rzsT_Q3KLzE

More Resources

Continue Reading the Bible

Continue reading Zaburi Chapter 44 and explore every book, chapter and verse of the Holy Bible. Use the navigation links above and below to move through the Scriptures with ease.

Frequently Asked Questions

What is Zaburi Chapter 44?

Zaburi Chapter 44 is part of the Book of Zaburi in the Holy Bible.

Can I read this chapter online?

Yes. You can read the complete Zaburi Chapter 44 online for free with easy chapter navigation.

More Chapters from Agano la Kale

  1. Zaburi Chapter 1
  2. Habakuki Chapter 3
  3. Ayubu Chapter 1
  4. Zaburi Chapter 2
  5. Kutoka Chapter 11
  6. Kutoka Chapter 2
  7. Ayubu Chapter 4

Explore More from Zaburi

  1. Zaburi Chapter 119
  2. Zaburi Chapter 91
  3. Zaburi Chapter 23
  4. Zaburi Chapter 56
  5. Zaburi Chapter 116
  6. Zaburi Chapter 2
  7. Zaburi Chapter 46

Related Chapters & Readings

  1. Ayubu Chapter 32
  2. Luka Chapter 7
  3. Hesabu Chapter 5
  4. Kumbukumbu la Torati Chapter 13
  5. 2 Wafalme Chapter 23
  6. 1 Wakorintho Chapter 8
  7. Warumi Chapter 2
Share Your Love

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *