Read Zaburi Chapter 118 Online
Read Zaburi Chapter 118 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of Zaburi in the Old Testament. Browse every verse with easy chapter navigation, continue to the next chapter, or explore the complete Book of Zaburi and the Holy Bible online.
Choose a Chapter
Zaburi 118
Sura 118
1. Haleluya. Mshukuruni Bwana kwa kuwa ni mwema, Kwa maana fadhili zake ni za milele.
2. Israeli na aseme sasa, Ya kwamba fadhili zake ni za milele.
3. Mlango wa Haruni na waseme sasa, Ya kwamba fadhili zake ni za milele.
4. Wamchao Bwana na waseme sasa, Ya kwamba fadhili zake ni za milele.
5. Katika shida yangu nalimwita Bwana; Bwana akanijibu akaniweka panapo nafasi.
6. Bwana yuko upande wangu, sitaogopa; Mwanadamu atanitenda nini?
7. Bwana yuko upande wangu, msaidizi wangu, Kwa hiyo nitawaona wanaonichukia wameshindwa.
8. Ni heri kumkimbilia Bwana Kuliko kuwatumainia wanadamu.
9. Ni heri kumkimbilia Bwana. Kuliko kuwatumainia wakuu.
10. Mataifa yote walinizunguka; Kwa jina la Bwana naliwakatilia mbali.
11. Walinizunguka, naam, walinizunguka; Kwa jina la Bwana naliwakatilia mbali.
12. Walinizunguka kama nyuki, Walizimika kama moto wa miibani; Kwa jina la Bwana naliwakatilia mbali.
13. Ulinisukuma sana ili nianguke; Lakini Bwana akanisaidia.
14. Bwana ni nguvu zangu na wimbo wangu, Naye amekuwa wokovu wangu.
15. Sauti ya furaha na wokovu Imo hemani mwao wenye haki; Mkono wa kuume wa Bwana hutenda makuu.
16. Mkono wa kuume wa Bwana umetukuzwa; Mkono wa kuume wa Bwana hutenda makuu.
17. Sitakufa bali nitaishi, Nami nitayasimulia matendo ya Bwana.
18. Bwana ameniadhibu sana, Lakini hakuniacha nife.
19. Nifungulieni malango ya haki, Nitaingia na kumshukuru Bwana.
20. Lango hili ni la Bwana, Wenye haki ndio watakaoliingia.
21. Nitakushukuru kwa maana umenijibu, Nawe umekuwa wokovu wangu.
22. Jiwe walilolikataa waashi Limekuwa jiwe kuu la pembeni.
23. Neno hili limetoka kwa Bwana, Nalo ni ajabu machoni petu.
24. Siku hii ndiyo aliyoifanya Bwana, Tutashangilia na kuifurahia.
25. Ee Bwana, utuokoe, twakusihi; Ee Bwana, utufanikishe, twakusihi.
26. Na abarikiwe yeye ajaye kwa jina la Bwana; Tumewabarikia toka nyumbani mwa Bwana.
27. Bwana ndiye aliye Mungu, Naye ndiye aliyetupa nuru. Ifungeni dhabihu kwa kamba Pembeni mwa madhabahu.
28. Ndiwe Mungu wangu, nami nitakushukuru, Ndiwe Mungu wangu, nami nitakutukuza.
29. Mshukuruni Bwana kwa kuwa ni mwema, Kwa maana fadhili zake ni za milele.
About Zaburi Chapter 118
Read Zaburi Chapter 118 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of Zaburi in the Old Testament. Continue reading with the chapter navigation above or explore the complete book.
Book Information
Book: Zaburi
Chapter: 118
Testament: Old Testament
How to Read this Chapter
Use the Previous and Next Chapter buttons to continue reading Zaburi. You can also adjust the font size for comfortable reading and browse other books of the Bible using the navigation links.
More Resources
Continue Reading the Bible
Continue reading Zaburi Chapter 118 and explore every book, chapter and verse of the Holy Bible. Use the navigation links above and below to move through the Scriptures with ease.
Frequently Asked Questions
What is Zaburi Chapter 118?
Zaburi Chapter 118 is part of the Book of Zaburi in the Holy Bible.
Can I read this chapter online?
Yes. You can read the complete Zaburi Chapter 118 online for free with easy chapter navigation.
More Chapters from Agano la Kale
- Isaya Chapter 1
- Isaya Chapter 3
- Isaya Chapter 2
- Isaya Chapter 6
- Isaya Chapter 7
- Isaya Chapter 5
- Isaya Chapter 14
Explore More from Zaburi
- Zaburi Chapter 83
- Zaburi Chapter 76
- Zaburi Chapter 52
- Zaburi Chapter 113
- Zaburi Chapter 4
- Zaburi Chapter 143
- Zaburi Chapter 105