Read Zekaria Chapter 6 Online
Read Zekaria Chapter 6 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of Zekaria in the Old Testament. Browse every verse with easy chapter navigation, continue to the next chapter, or explore the complete Book of Zekaria and the Holy Bible online.
Choose a Chapter
Zekaria 6
Sura 6
1. Nikainua macho yangu tena, nikaona, na tazama, yanatokea magari ya vita manne, yanatoka kati ya milima miwili, na milima hiyo ilikuwa ni milima ya shaba.
2. Katika gari la kwanza walikuwa farasi wekundu; na katika gari la pili walikuwa farasi weusi;
3. na katika gari la tatu walikuwa farasi weupe; na katika gari la nne walikuwa farasi wa rangi ya kijivujivu.
4. Nikajibu, nikamwuliza yule malaika aliyesema nami, Hawa ni nini, Bwana wangu?
5. Malaika akajibu, akaniambia, Hawa ni pepo nne za mbinguni, zitokeazo baada ya kusimama mbele za Bwana wa dunia yote.
6. Gari lile lenye farasi weusi latoka kwenda hata nchi ya kaskazini; nao farasi weupe wakatoka wakafuata nyuma yao; na wale wa rangi ya kijivujivu wakatoka kwenda hata nchi ya kusini.
7. Na wale wekundu wakatoka, wakataka kwenda huko na huko katika dunia; naye akawaambia, Haya! Tokeni, mwende huko na huko katika dunia. Basi wakaenda huko na huko katika dunia.
8. Ndipo akaniita, akaniambia akisema, Tazama, wale waendao mpaka nchi ya kaskazini wameituliza roho yangu katika nchi ya kaskazini.
9. Neno la Bwana likanijia, kusema,
10. Pokea vitu mikononi mwa baadhi ya watu waliohamishwa, yaani, Heldai, na Tobia, na Yedaya; na siku iyo hiyo enenda ukaingie katika nyumba ya Yosia, mwana wa Sefania, waliyoifikia kutoka Babeli;
11. naam, pokea fedha na dhahabu, ukafanye taji, ukamvike kichwani Yoshua, mwana wa Yehosadaki, kuhani mkuu;
12. ukamwambie, ukisema, Bwana wa majeshi asema hivi, ya kwamba, Tazama, mtu huyu ndiye ambaye jina lake ni Chipukizi; naye atakua katika mahali pake, naye atalijenga hekalu la Bwana.
13. Naam, yeye atalijenga hekalu la Bwana; naye atauchukua huo utukufu; ataketi akimiliki katika kiti chake cha enzi; na kutakuwa na kuhani katika kiti chake cha enzi; na shauri la amani litakuwa kati ya hao wawili.
14. Na hizo taji zitakuwa za Heldai, na Tobia, na Yedaya; na kwa fadhili za mwana wa Sefania; ziwe ukumbusho katika hekalu la Bwana.
15. Nao walio mbali watakuja na kujenga katika hekalu la Bwana, nanyi mtajua ya kuwa Bwana wa majeshi amenituma kwenu. Na haya yatatokea, kama mkijitahidi kuitii sauti ya Bwana, Mungu wenu.
About Zekaria Chapter 6
Read Zekaria Chapter 6 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of Zekaria in the Old Testament. Continue reading with the chapter navigation above or explore the complete book.
Book Information
Book: Zekaria
Chapter: 6
Testament: Old Testament
How to Read this Chapter
Use the Previous and Next Chapter buttons to continue reading Zekaria. You can also adjust the font size for comfortable reading and browse other books of the Bible using the navigation links.
More Resources
Continue Reading the Bible
Continue reading Zekaria Chapter 6 and explore every book, chapter and verse of the Holy Bible. Use the navigation links above and below to move through the Scriptures with ease.
Frequently Asked Questions
What is Zekaria Chapter 6?
Zekaria Chapter 6 is part of the Book of Zekaria in the Holy Bible.
Can I read this chapter online?
Yes. You can read the complete Zekaria Chapter 6 online for free with easy chapter navigation.
More Chapters from Agano la Kale
- Isaya Chapter 1
- Isaya Chapter 2
- Isaya Chapter 3
- Isaya Chapter 6
- Isaya Chapter 7
- Isaya Chapter 14
- Isaya Chapter 5
Explore More from zekaria
- Zekaria Chapter 14
- Zekaria Chapter 12
- Zekaria Chapter 7
- Zekaria Chapter 13
- Zekaria Chapter 10
- Zekaria Chapter 11
- Zekaria Chapter 3