Zaburi Chapter 106

For English

Read Zaburi Chapter 106 Online

Read Zaburi Chapter 106 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of Zaburi in the Old Testament. Browse every verse with easy chapter navigation, continue to the next chapter, or explore the complete Book of Zaburi and the Holy Bible online.

Choose a Chapter

Zaburi 106

Sura 106

1. Haleluya. Mshukuruni Bwana kwa kuwa ni mwema, Kwa maana fadhili zake ni za milele.

2. Nani awezaye kuyanena matendo makuu ya Bwana, Kuzihubiri sifa zake zote?

3. Heri washikao hukumu, Na kutenda haki sikuzote.

4. Ee Bwana, unikumbuke mimi, Kwa kibali uliyo nayo kwa watu wako. Unijilie kwa wokovu wako,

5. Ili niuone wema wa wateule wako. Nipate kuifurahia furaha ya taifa lako, Na kujisifu pamoja na watu wako.

6. Tumetenda dhambi pamoja na baba zetu, Tumetenda maovu, tumefanya ubaya.

7. Baba zetu katika Misri Hawakufikiri matendo yako ya ajabu; Hawakukumbuka wingi wa fadhili zako; Wakaasi penye bahari, bahari ya Shamu.

8. Lakini akawaokoa kwa ajili ya jina lake, Ayadhihirishe matendo yake makuu.

9. Akaikemea bahari ya Shamu ikakauka, Akawaongoza vilindini kana kwamba ni uwanda.

10. Akawaokoa na mkono wa mtu aliyewachukia, Na kuwakomboa na mkono wa adui zao.

11. Maji yakawafunika watesi wao, Hakusalia hata mmoja wao.

12. Ndipo walipoyaamini maneno yake, Waliziimba sifa zake.

13. Wakayasahau matendo yake kwa haraka, Hawakulingojea shauri lake.

14. Bali walitamani sana jangwani, Wakamjaribu Mungu nyikani.

15. Akawapa walichomtaka, Akawakondesha roho zao.

16. Wakamhusudu Musa matuoni, Na Haruni, mtakatifu wa Bwana.

17. Nchi ikapasuka ikammeza Dathani, Ikaufunika mkutano wa Abiramu.

18. Moto ukawaka katika mkutano wao, Miali yake ikawateketeza wabaya.

19. Walifanya ndama huko Horebu, Wakaisujudia sanamu ya kuyeyuka.

20. Wakaubadili utukufu wao Kuwa mfano wa ng'ombe mla majani.

21. Wakamsahau Mungu, mwokozi wao, Aliyetenda makuu katika Misri.

22. Matendo ya ajabu katika nchi ya Hamu, Mambo ya kutisha penye bahari ya Shamu.

23. Akasema ya kuwa atawaangamiza Kama Musa, mteule wake, asingalisimama, Mbele zake kama mahali palipobomoka, Ili aigeuze hasira yake asije akawaharibu.

24. Wakaidharau nchi ile ya kupendeza, Wala hawakuliamini neno lake.

25. Bali wakanung'unika hemani mwao, Wala hawakuisikiliza sauti ya Bwana.

26. Ndipo alipowainulia mkono wake, Ya kuwa atawaangamiza jangwani,

27. Na kuwatawanya wazao wao kati ya mataifa, Na kuwatapanya katika nchi mbali.

28. Wakajiambatiza na Baal-Peori, Wakazila dhabihu za wafu.

29. Wakamkasirisha kwa matendo yao; Tauni ikawashambulia.

30. Ndipo Finehasi akasimama akafanya hukumu; Tauni ikazuiliwa.

31. Akahesabiwa kuwa ana haki Kizazi baada ya kizazi hata milele.

32. Wakamghadhibisha penye maji ya Meriba, Hasara ikampata Musa kwa ajili yao,

33. Kwa sababu waliiasi roho yake, Akasema yasiyofaa kwa midomo yake.

34. Hawakuwaharibu watu wa nchi Kama Bwana alivyowaambia;

35. Bali walijichanganya na mataifa, Wakajifunza matendo yao.

36. Wakazitumikia sanamu zao, Nazo zikawa mtego kwao.

37. Naam, walitoa wana wao na binti zao Kuwa dhabihu kwa mashetani.

38. Wakamwaga damu isiyo na hatia, Damu ya wana wao na binti zao, Waliowatoa dhabihu kwa sanamu za Kanaani; Nchi ikatiwa unajisi kwa damu.

39. Ndivyo walivyotiwa uchafu kwa kazi zao, Wakafanya uasherati kwa matendo yao.

40. Hasira ya Bwana ikawaka juu ya watu wake, Akauchukia urithi wake.

41. Akawatia mikononi mwa mataifa, Nao waliowachukia wakawatawala.

42. Adui zao wakawaonea, Wakatiishwa chini ya mkono wao.

43. Mara nyingi aliwaponya, Bali walikuwa wakimwasi kwa mashauri yao, Wakadhilika katika uovu wao.

44. Lakini aliyaangalia mateso yao, Aliposikia kilio chao.

45. Akawakumbukia agano lake; Akawahurumia kwa wingi wa fadhili zake;

46. Akawajalia kuhurumiwa Na watu wote waliowateka.

47. Ee Bwana, Mungu wetu, utuokoe, Utukusanye kwa kututoa katika mataifa, Tulishukuru jina lako takatifu, Tuzifanyie shangwe sifa zako.

48. Na ahimidiwe Bwana, Mungu wa Israeli, Tangu milele hata milele. Watu wote na waseme, Amina. Haleluya.

About Zaburi Chapter 106

Read Zaburi Chapter 106 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of Zaburi in the Old Testament. Continue reading with the chapter navigation above or explore the complete book.

Book Information

Book: Zaburi
Chapter: 106
Testament: Old Testament

How to Read this Chapter

Use the Previous and Next Chapter buttons to continue reading Zaburi. You can also adjust the font size for comfortable reading and browse other books of the Bible using the navigation links.

https://www.youtube.com/watch?v=rzsT_Q3KLzE

More Resources

Continue Reading the Bible

Continue reading Zaburi Chapter 106 and explore every book, chapter and verse of the Holy Bible. Use the navigation links above and below to move through the Scriptures with ease.

Frequently Asked Questions

What is Zaburi Chapter 106?

Zaburi Chapter 106 is part of the Book of Zaburi in the Holy Bible.

Can I read this chapter online?

Yes. You can read the complete Zaburi Chapter 106 online for free with easy chapter navigation.

More Chapters from Agano la Kale

  1. Zaburi Chapter 1
  2. Habakuki Chapter 3
  3. Ayubu Chapter 1
  4. Zaburi Chapter 2
  5. Kutoka Chapter 11
  6. Kutoka Chapter 2
  7. Ayubu Chapter 4

Explore More from Zaburi

  1. Zaburi Chapter 87
  2. Zaburi Chapter 23
  3. Zaburi Chapter 93
  4. Zaburi Chapter 148
  5. Zaburi Chapter 16
  6. Zaburi Chapter 100
  7. Zaburi Chapter 82

Related Chapters & Readings

  1. Zaburi Chapter 59
  2. Luka Chapter 5
  3. Mambo ya Walawi Chapter 7
  4. Nehemia Chapter 1
  5. 2 Wafalme Chapter 17
  6. Marko Chapter 12
  7. Kumbukumbu la Torati Chapter 13
Share Your Love

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *