Kutoka Chapter 11

For English

Read Kutoka Chapter 11 Online

Read Kutoka Chapter 11 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of Kutoka in the Old Testament. Browse every verse with easy chapter navigation, continue to the next chapter, or explore the complete Book of Kutoka and the Holy Bible online.

Choose a Chapter

Kutoka 11

Sura 11

1. Bwana akamwambia Musa, Liko pigo moja bado, nitakaloleta juu ya Farao na juu ya Misri; baadaye atawapa ninyi ruhusa mtoke huku; naye hapo atakapowapa ruhusa, atawafukuza mtoke huku kabisa kabisa.

2. Basi nena wewe masikioni mwa watu hawa, na kila mtu mume na atake kwa jirani yake, na kila mwanamke atake kwa jirani yake, vyombo vya fedha, na vyombo vya dhahabu.

3. Bwana akawapa watu hao kibali machoni pa Wamisri. Zaidi ya hayo, huyo Musa alikuwa ni mkuu sana katika nchi ya Misri, machoni pa watumishi wa Farao, na machoni pa watu wake.

4. Musa akasema, Bwana asema hivi, Kama usiku wa manane mimi nitatoka nipite kati ya Misri;

5. na wazaliwa wa kwanza wote katika nchi ya Misri watakufa, tangu yule mzaliwa wa kwanza wa Farao aketiye katika kiti chake cha enzi, hata mzaliwa wa kwanza wa huyo kijakazi aliye pale nyuma ya jiwe la kusagia; na wazaliwa wa kwanza wote wa wanyama.

6. Ndipo kutakuwa na kilio kikuu katika nchi yote ya Misri, ambacho mfano wake haujakuwa bado majira yo yote, wala hautakuwako mfano wake tena kabisa.

7. Lakini katika wana wa Israeli hapana hata mbwa atakayetoa ulimi juu yao, juu ya mtu wala juu ya mnyama; ili kwamba mpate kujua jinsi Bwana anavyowatenga Wamisri na Waisraeli.

8. Tena hao watumishi wako wote watanitelemkia kwangu mimi, nao watanisujudia, wakisema, Toka wewe, na hawa watu wote wakufuatao; na baada ya hayo nitatoka. Basi akatoka kwa Farao na hasira kuu.

9. Bwana akamwambia Musa, Farao hatawasikiza ninyi; kusudi ajabu zangu ziongezeke katika nchi ya Misri.

10. Musa na Haruni walifanya ajabu hizo zote mbele ya Farao; Bwana akaufanya moyo wa Farao kuwa mgumu, asiwape wana wa Israeli ruhusa watoke nchi yake.

About Kutoka Chapter 11

Read Kutoka Chapter 11 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of Kutoka in the Old Testament. Continue reading with the chapter navigation above or explore the complete book.

Book Information

Book: Kutoka
Chapter: 11
Testament: Old Testament

How to Read this Chapter

Use the Previous and Next Chapter buttons to continue reading Kutoka. You can also adjust the font size for comfortable reading and browse other books of the Bible using the navigation links.

https://www.youtube.com/watch?v=rzsT_Q3KLzE

More Resources

Continue Reading the Bible

Continue reading Kutoka Chapter 11 and explore every book, chapter and verse of the Holy Bible. Use the navigation links above and below to move through the Scriptures with ease.

Frequently Asked Questions

What is Kutoka Chapter 11?

Kutoka Chapter 11 is part of the Book of Kutoka in the Holy Bible.

Can I read this chapter online?

Yes. You can read the complete Kutoka Chapter 11 online for free with easy chapter navigation.

More Chapters from Agano la Kale

  1. Zaburi Chapter 1
  2. Habakuki Chapter 3
  3. Ayubu Chapter 1
  4. Zaburi Chapter 2
  5. Kutoka Chapter 2
  6. Ayubu Chapter 4
  7. 1 Samweli Chapter 1

Explore More from Kutoka

  1. Kutoka Chapter 36
  2. Kutoka Chapter 32
  3. Kutoka Chapter 38
  4. Kutoka Chapter 8
  5. Kutoka Chapter 3
  6. Kutoka Chapter 35
  7. Kutoka Chapter 18

Related Chapters & Readings

  1. Mambo ya Walawi Chapter 14
  2. 1 Mambo ya Nyakati Chapter 21
  3. 1 Mambo ya Nyakati Chapter 10
  4. 2 Samweli Chapter 16
  5. Isaya Chapter 5
  6. 1 Timotheo Chapter 1
  7. Ayubu Chapter 1
Share Your Love

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *