Read 2 Mambo ya Nyakati Chapter 10 Online
Read 2 Mambo ya Nyakati Chapter 10 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of 2 Mambo ya Nyakati in the Old Testament. Browse every verse with easy chapter navigation, continue to the next chapter, or explore the complete Book of 2 Mambo ya Nyakati and the Holy Bible online.
Choose a Chapter
2 Mambo ya Nyakati 10
Sura 10
1. Rehoboamu akaenda Shekemu; maana Israeli wote walikuwa wamekuja Shekemu, ili wamfanye mfalme.
2. Ikawa Yeroboamu mwana wa Nebati aliposikia, (maana alikuwako Misri, ambako amekimbilia mbele ya mfalme Sulemani), Yeroboamu akarudi kutoka Misri.
3. Wakapeleka ujumbe, wakamwita, Yeroboamu akaja na Israeli wote, wakamwambia Rehoboamu, wakasema,
4. Baba yako alilifanya zito kongwa letu; basi sasa upunguze utumwa mgumu wa baba yako, na kongwa lake zito alilotutwika, nasi tutakutumikia.
5. Akawaambia, Mnirudie baada ya siku tatu. Watu wakaenda zao.
6. Mfalme Rehoboamu akataka shauri kwa wazee, waliosimama mbele ya Sulemani baba yake, alipokuwa hai bado, akasema, Mwanipa shauri gani la kuwajibu watu hawa?
7. Wakamwambia, wakasema, Ukiwa mwema kwao watu hawa, na kuwapendeza, na kuwaambia maneno mazuri, ndipo watakapokuwa watumishi wako siku zote.
8. Lakini akaliacha shauri lile la wazee walilompa, akataka shauri kwa wale vijana waliokua pamoja naye, waliosimama mbele yake.
9. Akawaambia, Je! Mwanipa shauri gani la kuwajibu watu hawa, waliosema nami, wakisema, Utufanyie jepesi kongwa alilotutwika baba yako.
10. Na wale vijana waliokua pamoja naye wakamwambia, wakasema, Uwaambie hivi watu wale waliosema nawe, wakinena, Baba yako alilifanya zito kongwa letu, lakini wewe tufanyie jepesi; uwaambie hivi, Kidole changu cha mwisho ni kinene kuliko kiuno cha baba yangu.
11. Basi kama baba yangu aliwatwika kongwa zito, mimi nitaongeza kongwa lenu; baba yangu akiwapiga kwa mijeledi, lakini mimi nitawapiga kwa nge.
12. Basi Yeroboamu na watu wote wakamjia Rehoboamu siku ya tatu, kama mfalme alivyoamuru, akisema, Mnirudie siku ya tatu.
13. Mfalme akawajibu kwa ukali; mfalme Rehoboamu akaliacha shauri la wazee, akasema nao kwa shauri la vijana,
14. akinena, Baba yangu aliwafanyia kongwa zito, nami nitawaongezea; baba yangu aliwapiga kwa mijeledi, lakini mimi nitawapiga kwa nge.
15. Basi mfalme hakuwasikia wale watu; maana jambo hili lilitoka kwa Mungu, ili alithibitishe neno lake alilomwambia Yeroboamu mwana wa Nebati kwa mkono wa Ahiya Mshiloni.
16. Basi Israeli wote walipoona ya kuwa mfalme hawasikilizi, watu wakamjibu mfalme, wakasema, Tuna sehemu gani katika Daudi? Wala hatuna urithi katika mwana wa Yese; nendeni zenu hemani kwenu, enyi Israeli, kila mtu; sasa itunze nyumba yako mwenyewe, Daudi. Basi wakaenda zao Israeli wote hemani kwao.
17. Lakini kwa habari za wana wa Israeli waliokaa katika miji ya Yuda, Rehoboamu alitawala juu yao.
18. Ndipo mfalme Rehoboamu akamtuma Adoramu, msimamizi wa shokoa; nao wana wa Israeli wakamtupia mawe, hata akafa. Mfalme Rehoboamu akafanya haraka kupanda garini mwake, ili akimbilie Yerusalemu.
19. Hivyo Israeli wakaasi juu ya nyumba ya Daudi, hata leo.
About 2 Mambo ya Nyakati Chapter 10
Read 2 Mambo ya Nyakati Chapter 10 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of 2 Mambo ya Nyakati in the Old Testament. Continue reading with the chapter navigation above or explore the complete book.
Book Information
Book: 2 Mambo ya Nyakati
Chapter: 10
Testament: Old Testament
How to Read this Chapter
Use the Previous and Next Chapter buttons to continue reading 2 Mambo ya Nyakati. You can also adjust the font size for comfortable reading and browse other books of the Bible using the navigation links.
More Resources
Continue Reading the Bible
Continue reading 2 Mambo ya Nyakati Chapter 10 and explore every book, chapter and verse of the Holy Bible. Use the navigation links above and below to move through the Scriptures with ease.
Frequently Asked Questions
What is 2 Mambo ya Nyakati Chapter 10?
2 Mambo ya Nyakati Chapter 10 is part of the Book of 2 Mambo ya Nyakati in the Holy Bible.
Can I read this chapter online?
Yes. You can read the complete 2 Mambo ya Nyakati Chapter 10 online for free with easy chapter navigation.
More Chapters from 2 MambO Ya Nyakati
- 2 Mambo ya Nyakati Chapter 17
- 2 Mambo ya Nyakati Chapter 5
- 2 Mambo ya Nyakati Chapter 21
- 2 Mambo ya Nyakati Chapter 13
- 2 Mambo ya Nyakati Chapter 12
- 2 Mambo ya Nyakati Chapter 9
- 2 Mambo ya Nyakati Chapter 4
Explore More from Agano la Kale
- Yeremia Chapter 1
- Mhubiri Chapter 3
- 2 Mambo ya Nyakati Chapter 2
- Zaburi Chapter 99
- Yeremia Chapter 33
- Waamuzi Chapter 9
- Hesabu Chapter 22