Kumbukumbu la Torati Chapter 14

For English

Read Kumbukumbu la Torati Chapter 14 Online

Read Kumbukumbu la Torati Chapter 14 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of Kumbukumbu la Torati in the Old Testament. Browse every verse with easy chapter navigation, continue to the next chapter, or explore the complete Book of Kumbukumbu la Torati and the Holy Bible online.

Choose a Chapter

Kumbukumbu la Torati 14

Sura 14

1. Ninyi mmekuwa wana wa Bwana, Mungu wenu; msijitoje miili yenu, wala msifanye upaa katikati ya macho yenu kwa ajili ya aliyekufa.

2. Kwa kuwa u taifa takatifu kwa Bwana, Mungu wako, na Bwana amekuchagua kuwa watu wake hasa, kuliko mataifa yote yaliyo juu ya uso wa nchi.

3. Usile kitu cho chote kichukizacho.

4. Wanyama mtakaokula ni hawa ng'ombe, na kondoo, na mbuzi,

5. kulungu, na paa, na kongoni, na mbuzi wa mwitu, na paa mweupe, na pofu, na mbuzi wa mlima;

6. na kila mnyama aliyepasuliwa ukwato, ukapasuka ukwato wake zikawa mbili, naye ni mnyama mwenye kucheua akatafuna tena, katika wanyama wote, ndiye mnyama mtakayemla.

7. Lakini, hawa msile katika wale wenye kucheua, na hao waliopasuliwa ukwato; ngamia, na sungura, na kwang'a, kwa kuwa hucheua, lakini hawakupasuliwa kwato, ni najisi kwenu;

8. na nguruwe, kwa kuwa amepasuliwa ukwato lakini hacheui, huyu ni najisi kwenu msile nyama zao, wala mizoga yao msiiguse.

9. Mtakula hawa katika wote walio majini; kila kilicho na mapezi na magamba mtakula;

10. na kila kisichokuwa na mapezi na magamba msile; ni najisi kwenu.

11. Mna ruhusa kula katika nyuni wote walio safi.

12. Lakini hawa msiwale; tai, na furukombe, na kipungu;

13. na kengewa, na kozi, na mwewe kwa aina zake;

14. na kila kunguru kwa aina zake;

15. na mbuni, na kirukanjia, na dudumizi, na kipanga kwa aina zake;

16. na bundi, na mumbi, na bundi mkubwa;

17. na mwari, na nderi, na mnandi;

18. na membe, na koikoi, kwa aina zake; na hudihudi, na popo.

19. Na wadudu wote watambaao wenye mabawa ni najisi kwenu; msiwale.

20. Mna ruhusa kula katika nyuni wote walio safi.

21. Msile nyamafu yo yote; waweza kumpa mgeni aliye ndani ya malango yako, ili apate kula; au kumliza mtu wa mataifa; kwa kuwa wewe u taifa takatifu kwa Bwana, Mungu wako. Usimtokose mwana-mbuzi katika maziwa ya mamaye.

22. Usiache kutoa zaka ya fungu la kumi katika maongeo yote ya mbegu zako, yatokayo shamba mwaka baada ya mwaka.

23. Nawe utakula mbele za Bwana, Mungu wako, mahali atakapochagua apakalishe jina lake, zaka ya nafaka zako, na divai yako, na mafuta yako, na wazaliwa wa kwanza wa makundi yako ya ng'ombe na ya kondoo; ili upate kujifunza kumcha Bwana, Mungu wako, daima.

24. Na njia ikiwa ndefu mno nawe, usiweze kuzichukua kwa kuwa mahali ni mbali nawe mno atakapochagua Bwana, Mungu wako, apakalishe jina lake, hapo atakapokubarikia Bwana, Mungu wako;

25. ndipo uzibadili ziwe fedha, na kufunga zile fedha uende nazo mkononi mwako, hata mahali atakapochagua Bwana, Mungu wako;

26. na zile fedha zitumie kwa cho chote itakachotamani roho yako, ng'ombe, au kondoo, au divai, au kileo, au roho yako itakacho kwako cho chote; nawe utakula huko mbele za Bwana, Mungu wako; tena furahi, wewe na nyumba yako;

27. na Mlawi aliye ndani ya malango yako usimwache, kwani hana fungu wala urithi pamoja nawe.

28. Kila mwaka wa tatu, mwisho wake, toa fungu la kumi lote la maongeo yako ya mwaka huo, uliweke ndani ya malango yako;

29. na Mlawi kwa kuwa hana fungu wala urithi pamoja nawe, na mgeni, na yatima, na mjane aliyefiliwa na mumewe, walio ndani ya malango yako, na waje wale na kushiba; ili kwamba Bwana, Mungu wako, akubarikie katika kazi yote ya mkono wako uifanyayo.

About Kumbukumbu la Torati Chapter 14

Read Kumbukumbu la Torati Chapter 14 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of Kumbukumbu la Torati in the Old Testament. Continue reading with the chapter navigation above or explore the complete book.

Book Information

Book: Kumbukumbu la Torati
Chapter: 14
Testament: Old Testament

How to Read this Chapter

Use the Previous and Next Chapter buttons to continue reading Kumbukumbu la Torati. You can also adjust the font size for comfortable reading and browse other books of the Bible using the navigation links.

https://www.youtube.com/watch?v=rzsT_Q3KLzE

More Resources

Continue Reading the Bible

Continue reading Kumbukumbu la Torati Chapter 14 and explore every book, chapter and verse of the Holy Bible. Use the navigation links above and below to move through the Scriptures with ease.

Frequently Asked Questions

What is Kumbukumbu la Torati Chapter 14?

Kumbukumbu la Torati Chapter 14 is part of the Book of Kumbukumbu la Torati in the Holy Bible.

Can I read this chapter online?

Yes. You can read the complete Kumbukumbu la Torati Chapter 14 online for free with easy chapter navigation.

More Chapters from Agano la Kale

  1. Zaburi Chapter 1
  2. Habakuki Chapter 3
  3. Ayubu Chapter 1
  4. Zaburi Chapter 2
  5. 1 Samweli Chapter 1
  6. Kutoka Chapter 11
  7. Kutoka Chapter 2

Explore More from Kumbukumbu La Torati

  1. Kumbukumbu la Torati Chapter 1
  2. Kumbukumbu la Torati Chapter 33
  3. Kumbukumbu la Torati Chapter 17
  4. Kumbukumbu la Torati Chapter 7
  5. Kumbukumbu la Torati Chapter 26
  6. Kumbukumbu la Torati Chapter 23
  7. Kumbukumbu la Torati Chapter 25

Related Chapters & Readings

  1. Hesabu Chapter 25
  2. Ufunuo wa Yohana Chapter 5
  3. 1 Wafalme Chapter 19
  4. Mwanzo Chapter 30
  5. Zaburi Chapter 15
  6. Yeremia Chapter 31
  7. 2 Wafalme Chapter 5
Share Your Love

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *