Isaya Chapter 45

For English

Read Isaya Chapter 45 Online

Read Isaya Chapter 45 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of Isaya in the Old Testament. Browse every verse with easy chapter navigation, continue to the next chapter, or explore the complete Book of Isaya and the Holy Bible online.

Choose a Chapter

Isaya 45

Sura 45

1. Haya ndiyo Bwana amwambiayo Koreshi, masihi wake, ambaye nimemshika mkono wake wa kuume, ili kutiisha mataifa mbele yake, nami nitalegeza viuno vya wafalme; ili kufungua milango mbele yake, hata malango hayatafungwa.

2. Nitakwenda mbele yako, na kupasawazisha mahali palipoparuza; nitavunja vipande vipande milango ya shaba, na kukata-kata mapingo ya chuma;

3. nami nitakupa hazina za gizani, na mali zilizofichwa za mahali pa siri, upate kujua ya kuwa mimi ni Bwana, nikuitaye kwa jina lako, naam, Mungu wa Israeli.

4. Kwa ajili ya Yakobo, mtumishi wangu, na Israeli, mteule wangu, nimekuita kwa jina lako; nimekupa jina la sifa; ijapokuwa hukunijua.

5. Mimi ni Bwana, wala hapana mwingine; zaidi yangu mimi hapana Mungu; nitakufunga mshipi ijapokuwa hukunijua;

6. ili wapate kujua toka maawio ya jua, na toka magharibi, ya kuwa hapana mwingine zaidi ya mimi; Mimi ni Bwana, wala hapana mwingine.

7. Mimi naiumba nuru, na kulihuluku giza; mimi nafanya suluhu, na kuhuluku ubaya; Mimi ni Bwana, niyatendaye hayo yote.

8. Dondokeni, enyi mbingu, toka juu, Mawingu na yamwage haki; Nchi na ifunuke, ili kutoa wokovu, Nayo itoe haki ikamee pamoja; Mimi, Bwana, nimeiumba.

9. Ole wake ashindanaye na Muumba wake! Kigae kimoja katika vigae vya dunia! Je! Udongo umwambie yeye aufinyangaye; Unafanya nini? Au kazi yako, Hana mikono?

10. Ole wake amwambiaye baba yake, Wazaa nini? Au mwanamke, Una utungu wa nini?

11. Bwana, Mtakatifu wa Israeli, na Muumba wake, asema hivi; Niulize habari za mambo yatakayokuja; mambo ya wana wangu, na habari ya kazi ya mikono yangu; haya! Niagizeni.

12. Mimi nimeiumba dunia, nimemhuluku mwanadamu juu yake; Mimi, naam, mikono yangu mimi, imezitanda mbingu, na jeshi lake lote nimeliamuru.

13. Mimi nimemwinua katika haki, nami nitazinyosha njia zake zote; ataujenga mji wangu, naye atawaacha huru watu wangu waliohamishwa, si kwa kulipwa fedha, wala kwa kupewa zawadi, asema Bwana wa majeshi.

14. Bwana asema hivi, Kazi ya Misri, na bidhaa ya Kushi, na Waseba, watu walio warefu, watakujilia, nao watakuwa wako; watakufuata; watakuja katika minyororo; wataanguka chini mbele yako, watakuomba, wakisema, Hakika Mungu yu ndani yako; wala hapana mwingine, hapana Mungu tena.

15. Hakika wewe u Mungu ujifichaye nafsi yako, Ee Mungu wa Israeli, Mwokozi.

16. Watatahayarika, naam, watafadhaika, wote pia; wale wafanyao sanamu wataingia fadhaa pamoja.

17. Bali Israeli wataokolewa na Bwana kwa wokovu wa milele; ninyi hamtatahayarika, wala kufadhaika, milele na milele.

18. Maana Bwana, aliyeziumba mbingu, asema hivi; Yeye ni Mungu; ndiye aliyeiumba dunia na kuifanya; ndiye aliyeifanya imara; hakuiumba ukiwa, aliiumba ili ikaliwe na watu; Mimi ni Bwana, wala hapana mwingine.

19. Sikusema kwa siri, katika mahali pa nchi ya giza; sikuwaambia wazao wa Yakobo; Nitafuteni bure; Mimi, Bwana, nasema haki; nanena mambo ya adili.

20. Jikusanyeni mje; na kukaribia pamoja, ninyi wa mataifa mliookoka; hawana maarifa wale wachukuao mti wa sanamu yao ya kuchonga; wamwombao mungu asiyeweza kuokoa.

21. Hubirini, toeni habari; naam, na wafanye mashauri pamoja; ni nani aliyeonyesha haya tangu zamani za kale? Ni nani aliyeyahubiri hapo zamani? Si mimi, Bwana? Wala hapana Mungu zaidi ya mimi; Mungu mwenye haki, mwokozi; hapana mwingine zaidi ya mimi.

22. Niangalieni mimi, mkaokolewe, enyi ncha zote za dunia; maana mimi ni Mungu; hapana mwingine.

23. Kwa nafsi yangu nimeapa, neno hili limetoka kinywani mwangu katika haki, wala halitarudi, ya kwamba mbele zangu kila goti litapigwa, kila ulimi utaapa.

24. Mmoja ataniambia, Kwa Bwana, peke yake, iko haki na nguvu; naam, watu watamwendea yeye, na wote waliomkasirikia watatahayarika.

25. Katika Bwana wazao wote wa Israeli watapewa haki, na kutukuka.

About Isaya Chapter 45

Read Isaya Chapter 45 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of Isaya in the Old Testament. Continue reading with the chapter navigation above or explore the complete book.

Book Information

Book: Isaya
Chapter: 45
Testament: Old Testament

How to Read this Chapter

Use the Previous and Next Chapter buttons to continue reading Isaya. You can also adjust the font size for comfortable reading and browse other books of the Bible using the navigation links.

https://www.youtube.com/watch?v=rzsT_Q3KLzE

More Resources

Continue Reading the Bible

Continue reading Isaya Chapter 45 and explore every book, chapter and verse of the Holy Bible. Use the navigation links above and below to move through the Scriptures with ease.

Frequently Asked Questions

What is Isaya Chapter 45?

Isaya Chapter 45 is part of the Book of Isaya in the Holy Bible.

Can I read this chapter online?

Yes. You can read the complete Isaya Chapter 45 online for free with easy chapter navigation.

More Chapters from Agano la Kale

  1. Zaburi Chapter 1
  2. Habakuki Chapter 3
  3. Ayubu Chapter 1
  4. Zaburi Chapter 2
  5. Kutoka Chapter 11
  6. Kutoka Chapter 2
  7. Ayubu Chapter 4

Explore More from Isaya

  1. Isaya Chapter 7
  2. Işaýa Chapter 23
  3. Işaýa Chapter 44
  4. Isaya Chapter 39
  5. Işaýa Chapter 54
  6. Isaya Chapter 29
  7. Işaýa Chapter 16

Related Chapters & Readings

  1. Yona Chapter 4
  2. 2 Samweli Chapter 24
  3. Sefania Chapter 1
  4. Yohana Chapter 19
  5. Ezra Chapter 3
  6. Zaburi Chapter 55
  7. Ufunuo wa Yohana Chapter 22
Share Your Love

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *