Ayubu Chapter 28

For English

Read Ayubu Chapter 28 Online

Read Ayubu Chapter 28 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of Ayubu in the Old Testament. Browse every verse with easy chapter navigation, continue to the next chapter, or explore the complete Book of Ayubu and the Holy Bible online.

Choose a Chapter

Ayubu 28

Sura 28

1. Hakika kuna shimo wachimbako fedha, Na mahali wapatapo dhahabu waisafishayo.

2. Chuma hufukuliwa katika ardhi, Na shaba huyeyushwa katika mawe.

3. Binadamu hukomesha giza; Huyatafuta-tafuta hata mpaka ulio mbali, Mawe ya giza kuu, giza tupu.

4. Hufukua shimo mbali na makao ya watu; Husahauliwa na nyayo zipitazo; Huning'inia mbali na watu, huyumba-yumba huko na huko.

5. Katika ardhi ndimo kitokeamo chakula; Na chini yake hupinduliwa kama kwa moto.

6. Mawe yake ni mahali zipatikanapo yakuti; Nayo ina mchanga wa dhahabu.

7. Njia ile hapana ndege mkali aijuaye, Wala jicho la tai halijaiona;

8. Wanyama wakali wajivunao hawajaikanyaga, Wala simba mkali hajaipita.

9. Huunyoshea mwamba wa gumegume mkono wake; Huipindua milima hata misingi yake.

10. Hukata mifereji kati ya majabali; Na jicho lake huona kila kito cha thamani

11. Hufunga vijito visichuruzike; Na kitu kilichostirika hukifunua.

12. Bali hekima itapatikana wapi? Na mahali pa ufahamu ni wapi?

13. Mwanadamu hajui thamani yake, Wala haionekani katika nchi ya walio hai.

14. Vilindi vyasema, Haimo ndani yangu; Na bahari yasema, Haiko kwangu.

15. Haipatikani kwa dhahabu, Wala fedha haitapimwa iwe thamani yake.

16. Haiwezi kutiwa thamani kwa dhahabu ya Ofiri, Wala kwa shohamu ya thamani nyingi, wala kwa yakuti ya samawi.

17. Dhahabu na vioo haviwezi kulinganishwa nayo; Wala kubadili kwake hakutakuwa kwa vyombo vya dhahabu safi.

18. Havitatajwa fedhaluka wala bilauri; Naam, kima cha hekima chapita marijani.

19. Yakuti ya rangi ya manjano ya Kushi haitasawazishwa nayo, Wala haitatiwa kima kwa dhahabu safi.

20. Basi hekima yatoka wapi? Na mahali pa ufahamu ni wapi?

21. Kwa kuwa imefichwa mbali na macho ya wote walio hai, Na kusitirika na ndege wa angani.

22. Uharibifu na Mauti husema, Tumesikia habari zake kwa masikio yetu.

23. Mungu ndiye aijuaye njia yake, Naye anajua mahali pake.

24. Maana anatazama hata miisho ya nchi, Na kuona chini ya mbingu nzima.

25. Apate kuufanyia upepo uzito wake; Naam, anayapima maji kwa kipimo.

26. Hapo alipoiwekea mvua amri, Na njia kwa umeme wa radi.

27. Ndipo alipoiona na kuitangaza; Aliithibitisha, naam, na kuichunguza.

28. Kisha akamwambia mwanadamu, Tazama, kumcha Bwana ndiyo hekima, Na kujitenga na uovu ndio ufahamu.

About Ayubu Chapter 28

Read Ayubu Chapter 28 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of Ayubu in the Old Testament. Continue reading with the chapter navigation above or explore the complete book.

Book Information

Book: Ayubu
Chapter: 28
Testament: Old Testament

How to Read this Chapter

Use the Previous and Next Chapter buttons to continue reading Ayubu. You can also adjust the font size for comfortable reading and browse other books of the Bible using the navigation links.

https://www.youtube.com/watch?v=rzsT_Q3KLzE

More Resources

Continue Reading the Bible

Continue reading Ayubu Chapter 28 and explore every book, chapter and verse of the Holy Bible. Use the navigation links above and below to move through the Scriptures with ease.

Frequently Asked Questions

What is Ayubu Chapter 28?

Ayubu Chapter 28 is part of the Book of Ayubu in the Holy Bible.

Can I read this chapter online?

Yes. You can read the complete Ayubu Chapter 28 online for free with easy chapter navigation.

More Chapters from Agano la Kale

  1. Zaburi Chapter 1
  2. Habakuki Chapter 3
  3. Ayubu Chapter 1
  4. Zaburi Chapter 2
  5. Kutoka Chapter 11
  6. Kutoka Chapter 2
  7. Ayubu Chapter 4

Explore More from Ayubu

  1. Ayubu Chapter 21
  2. Ayubu Chapter 9
  3. Ayubu Chapter 41
  4. Ayubu Chapter 20
  5. Ayubu Chapter 19
  6. Ayubu Chapter 30
  7. Ayubu Chapter 29

Related Chapters & Readings

  1. 1 Mambo ya Nyakati Chapter 8
  2. Isaya Chapter 5
  3. Zaburi Chapter 132
  4. Kutoka Chapter 39
  5. Yoshua Chapter 7
  6. Luka Chapter 18
  7. Marko Chapter 16
Share Your Love

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *