Read Ayubu Chapter 22 Online
Read Ayubu Chapter 22 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of Ayubu in the Old Testament. Browse every verse with easy chapter navigation, continue to the next chapter, or explore the complete Book of Ayubu and the Holy Bible online.
Choose a Chapter
Ayubu 22
Sura 22
1. Ndipo huyo Elifazi Mtemani akajibu, na kusema,
2. Je! Yumkini mtu awaye yote kumfaa Mungu? Hakika yeye aliye na hekima hujifaa mwenyewe.
3. Je! Mwenyezi hupata furaha katika wewe kuwa mwenye haki? Au je, ni faida kwake, kwamba wafanya njia zako kuwa timilifu?
4. Je! Ni kwa wewe kumcha yeye anakukemea? Na kuingia hukumuni nawe?
5. Je! Uovu wako si mkuu? Wala maovu yako hayana mwisho.
6. Kwa kuwa umetwaa dhamana kwa nduguyo bure, Na kuwavua nguo zao walio uchi.
7. Hukumpa maji ya kunywa huyo aliyechoka, Nawe umemnyima chakula huyo mwenye njaa.
8. Lakini huyo shujaa, nchi ilikuwa yake; Na huyo mwenye kusifiwa, yeye aliikaa.
9. Umewafukuza wanawake wajane hali ya utupu, Na mikono ya mayatima imevunjwa.
10. Kwa hiyo umezungukwa na mitego, Na hofu ya ghafula yakutaabisha,
11. Au je! Huoni giza, Na maji mengi yanayokufunika?
12. Je! Mungu hayuko mbinguni juu? Tena tazama umbali wa nyota, jinsi zilivyo juu!
13. Nawe wasema, Mungu anajua nini? Je! Aweza kuamua kati ya giza kuu?
14. Mawingu mazito ni kifuniko chake, hata asione; Naye yuatembea juu ya kuba ya mbingu.
15. Je! Utaiandama njia ya zamani Waliyoikanyaga watu waovu?
16. Ambao walinyakuliwa kabla ya wakati wao, Msingi wao ulimwagika kama kijito cha maji;
17. Waliomwambia Mungu, Tuondokee; Tena, Huyo Mwenyezi aweza kutufanyia nini?
18. Naye ndiye aliyezijaza nyumba zao vitu vyema; Lakini mashauri ya waovu na yawe mbali nami.
19. Wenye haki huyaona hayo wakafurahi; Nao wasio na hatia huwacheka;
20. Wasema, Hakika hao waliotuinukia wamekatiliwa mbali, Na mabaki yao moto umeyateketeza.
21. Mjue sana Mungu, ili uwe na amani; Ndivyo mema yatakavyokujia.
22. Uyapokee, tafadhali, mafunzo yatokayo kinywani mwake, Na maneno yake yaweke moyoni mwako.
23. Ukimrudia Mwenyezi, utajengwa; Ukiuondoa udhalimu mbali na hema yako.
24. Nawe hazina zako ziweke mchangani, Na dhahabu ya Ofiri iweke kati ya mawe ya vijito;
25. Naye Mwenyezi atakuwa hazina yako, Atakuwa ni fedha ya thamani kwako.
26. Kwani ndipo utakapojifurahisha katika Mwenyezi, Na kuinua uso wako kumwelekea Mungu.
27. Utamwomba yeye naye atakusikia; Nawe utazitimiliza nadhiri zako.
28. Nawe utakusudia neno, nalo litathibitika kwako; Na mwanga utaziangazia njia zako.
29. Hapo watakapokuangusha, utasema, Kuna kuinuka tena; Naye mnyenyekevu Mungu atamwokoa.
30. Atamwokoa na huyo asiye na hatia; Naam, utaokolewa kwa sababu ya usafi wa mikono yako.
About Ayubu Chapter 22
Read Ayubu Chapter 22 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of Ayubu in the Old Testament. Continue reading with the chapter navigation above or explore the complete book.
Book Information
Book: Ayubu
Chapter: 22
Testament: Old Testament
How to Read this Chapter
Use the Previous and Next Chapter buttons to continue reading Ayubu. You can also adjust the font size for comfortable reading and browse other books of the Bible using the navigation links.
More Resources
Continue Reading the Bible
Continue reading Ayubu Chapter 22 and explore every book, chapter and verse of the Holy Bible. Use the navigation links above and below to move through the Scriptures with ease.
Frequently Asked Questions
What is Ayubu Chapter 22?
Ayubu Chapter 22 is part of the Book of Ayubu in the Holy Bible.
Can I read this chapter online?
Yes. You can read the complete Ayubu Chapter 22 online for free with easy chapter navigation.
More Chapters from Agano la Kale
- Isaya Chapter 1
- Isaya Chapter 3
- Isaya Chapter 2
- Isaya Chapter 6
- Isaya Chapter 7
- Isaya Chapter 14
- Isaya Chapter 5
Explore More from Ayubu
- Ayubu Chapter 39
- Ayubu Chapter 13
- Ayubu Chapter 23
- Ayubu Chapter 28
- Ayubu Chapter 36
- Ayubu Chapter 30
- Ayubu Chapter 8