Ayubu Chapter 11

For English

Read Ayubu Chapter 11 Online

Read Ayubu Chapter 11 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of Ayubu in the Old Testament. Browse every verse with easy chapter navigation, continue to the next chapter, or explore the complete Book of Ayubu and the Holy Bible online.

Choose a Chapter

Ayubu 11

Sura 11

1. Ndipo Sofari Mnaamathi akajibu, na kusema,

2. Je! Huu wingi wa maneno usijibiwe? Na mtu aliyejaa maneno, je! Ahesabiwe kuwa na haki?

3. Je! Majivuno yako yawanyamazishe watu wawe kimya? Nawe hapo ufanyapo dhihaka, je! Hapana mtu atakayekutahayarisha?

4. Kwa kuwa wewe wasema, Mafunzo yangu ni safi, Nami ni safi machoni pako.

5. Lakini, laiti Mungu angenena, Na kuifunua midomo yake juu yako;

6. Tena akuonyeshe hizo siri za hekima, Ya kuwa hufanikiwa katika kuyatimiza makusudi yake! Ujue basi ya kuwa Mungu akuachilia katika uovu wako.

7. Je! Wewe waweza kuuvumbua ukuu wa Mungu? Waweza kuufikilia upeo wa huyo Mwenyezi?

8. Ni juu mno kama mbingu; waweza kufanya nini wewe? Ni wenye kina kuliko kuzimuni; waweza kujua nini wewe?

9. Cheo chake ni kirefu kuliko dunia, Ni kipana zaidi ya bahari.

10. Yeye akipita, na kufunga watu, Na kuwaita hukumuni, ni nani basi awezaye kumzuia?

11. Kwani yeye awajua watu baradhuli; Huona na uovu pia, hata asipoufikiri.

12. Lakini mpumbavu aweza kupata ufahamu, Ingawa mwanadamu huzaliwa kama mtoto wa punda-mwitu.

13. Wewe ukiuweka moyo wako kwa uelekevu, Na kumnyoshea mikono yako;

14. Ikiwa una uovu mkononi mwako, uweke mbali nawe, Wala usikubali upuzi kukaa hemani mwako;

15. Hakika ndipo utakapopata kuinua uso pasipo ila; Naam, utathibitika, wala hutakuwa na hofu;

16. Kwa kuwa utasahau mashaka yako; Utayakumbuka kama maji yaliyokwisha pita;

17. Na maisha yako yatakuwa meupe kuliko adhuhuri; Lijapokuwa ni giza, litakuwa kama alfajiri.

18. Nawe utakuwa salama, kwa sababu kuna matumaini; Naam, utatafuta-tafuta kando yako, na kupumzika katika salama.

19. Tena utalala, wala hapana atakayekutia hofu; Naam, wengi watakutafuta uso wako.

20. Lakini macho ya waovu yataingia kiwi, Nao hawatakuwa na njia ya kukimbilia, Na matumaini yao yatakuwa ni kutoa roho.

About Ayubu Chapter 11

Read Ayubu Chapter 11 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of Ayubu in the Old Testament. Continue reading with the chapter navigation above or explore the complete book.

Book Information

Book: Ayubu
Chapter: 11
Testament: Old Testament

How to Read this Chapter

Use the Previous and Next Chapter buttons to continue reading Ayubu. You can also adjust the font size for comfortable reading and browse other books of the Bible using the navigation links.

https://www.youtube.com/watch?v=rzsT_Q3KLzE

More Resources

Continue Reading the Bible

Continue reading Ayubu Chapter 11 and explore every book, chapter and verse of the Holy Bible. Use the navigation links above and below to move through the Scriptures with ease.

Frequently Asked Questions

What is Ayubu Chapter 11?

Ayubu Chapter 11 is part of the Book of Ayubu in the Holy Bible.

Can I read this chapter online?

Yes. You can read the complete Ayubu Chapter 11 online for free with easy chapter navigation.

More Chapters from Agano la Kale

  1. Zaburi Chapter 1
  2. Habakuki Chapter 3
  3. Ayubu Chapter 1
  4. Zaburi Chapter 2
  5. Kutoka Chapter 11
  6. Kutoka Chapter 2
  7. Ayubu Chapter 4

Explore More from Ayubu

  1. Ayubu Chapter 28
  2. Ayubu Chapter 19
  3. Ayubu Chapter 31
  4. Ayubu Chapter 17
  5. Ayubu Chapter 7
  6. Ayubu Chapter 15
  7. Ayubu Chapter 26

Related Chapters & Readings

  1. Mhubiri Chapter 3
  2. 1 Wakorintho Chapter 15
  3. Luka Chapter 5
  4. 1 Mambo ya Nyakati Chapter 20
  5. Waamuzi Chapter 11
  6. Mathayo Chapter 14
  7. Wafilipi Chapter 1
Share Your Love

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *