Read Ayubu Chapter 27 Online
Read Ayubu Chapter 27 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of Ayubu in the Old Testament. Browse every verse with easy chapter navigation, continue to the next chapter, or explore the complete Book of Ayubu and the Holy Bible online.
Choose a Chapter
Ayubu 27
Sura 27
1. Kisha Ayubu akaendelea na mithali yake, na kusema,
2. Kama aishivyo Mungu, aliyeniondolea haki yangu; Huyo Mwenyezi aliyeitesa nafsi yangu;
3. (Kwa kuwa uhai wangu ukali mzima ndani yangu, Na roho ya Mungu i katika pua yangu;)
4. Hakika midomo yangu haitanena yasiyo haki, Wala ulimi wangu hautatamka udanganyifu.
5. Hasha! Nisiwahesabie ninyi kuwa na haki; Hata nitakapokufa sitajiondolea uelekevu wangu.
6. Haki yangu naishika sana, wala sitaiacha; Moyo wangu hautanisuta wakati nikiwapo hai.
7. Adui yangu na awe kama huyo mwovu, Na mwenye kuondoka kinyume changu na awe kama asiye haki.
8. Kwani tumaini la mpotovu ni nini, ingawa ajipatia faida, Hapo Mungu amwondoleapo roho yake?
9. Je! Mungu atakisikia kilio chake, Taabu zitakapomfikilia?
10. Je! Atajifurahisha katika Mwenyezi, Na kumlingana Mungu nyakati zote?
11. Nitawafundisha ninyi mambo ya mkono wa Mungu; Hayo yaliyo kwa Mwenyezi sitayaficha.
12. Tazama, ninyi nyote mmeyaona wenyewe; Mbona basi mmebatilika kabisa?
13. Hii ndiyo sehemu ya mtu mwovu kwa Mungu, Na urithi wa hao waoneao, waupokeao kwa Mwenyezi.
14. Watoto wake wakiongezeka ni kwa upanga; Na wazao wake hawatashiba chakula.
15. Hao watakaosalia kwake watazikwa katika kufa, Wala wajane wake waliofiwa na waume hawataomboleza.
16. Ajapokusanya fedha kama mavumbi, Na kujifanyia mavazi kama udongo kwa wingi;
17. Yumkini kuyatengeza, lakini wenye haki watayavaa, Nao wasio na hatia watazigawanya hizo fedha.
18. Yeye hujenga nyumba yake kama mdudu, Na kama kibanda afanyacho mlinzi.
19. Yeye hujilaza hali ni tajiri, lakini ndio mwisho; Hufunua macho yake, naye hayuko.
20. Vitisho vyampata kama maji mengi; Dhoruba humwiba usiku.
21. Upepo wa mashariki humchukua, naye huondoka; Na kumkumba atoke mahali pake.
22. Kwani Mungu atamtupia asimhurumie; Angependa kuukimbia mkono wake.
23. Watu watampigia makofi, Na kumzomea atoke mahali pake.
About Ayubu Chapter 27
Read Ayubu Chapter 27 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of Ayubu in the Old Testament. Continue reading with the chapter navigation above or explore the complete book.
Book Information
Book: Ayubu
Chapter: 27
Testament: Old Testament
How to Read this Chapter
Use the Previous and Next Chapter buttons to continue reading Ayubu. You can also adjust the font size for comfortable reading and browse other books of the Bible using the navigation links.
More Resources
Continue Reading the Bible
Continue reading Ayubu Chapter 27 and explore every book, chapter and verse of the Holy Bible. Use the navigation links above and below to move through the Scriptures with ease.
Frequently Asked Questions
What is Ayubu Chapter 27?
Ayubu Chapter 27 is part of the Book of Ayubu in the Holy Bible.
Can I read this chapter online?
Yes. You can read the complete Ayubu Chapter 27 online for free with easy chapter navigation.
More Chapters from Agano la Kale
- Isaya Chapter 1
- Isaya Chapter 3
- Isaya Chapter 2
- Isaya Chapter 6
- Isaya Chapter 7
- Isaya Chapter 5
- Isaya Chapter 14
Explore More from Ayubu
- Ayubu Chapter 24
- Ayubu Chapter 20
- Ayubu Chapter 18
- Ayubu Chapter 10
- Ayubu Chapter 28
- Ayubu Chapter 7
- Ayubu Chapter 16