Sefania Chapter 2

For English

Read Sefania Chapter 2 Online

Read Sefania Chapter 2 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of Sefania in the Old Testament. Browse every verse with easy chapter navigation, continue to the next chapter, or explore the complete Book of Sefania and the Holy Bible online.

Choose a Chapter

Sefania 2

Sura 2

1. Jikusanyeni, naam, jikusanyeni, Ee taifa lisilo na haya;

2. kabla haijazaa hiyo amri, kabla haijapita siku ile kama makapi, kabla haijawajilia hasira kali ya Bwana, kabla haijawajilia siku ya hasira ya Bwana.

3. Mtafuteni Bwana, enyi nyote mlio wanyenyekevu wa dunia, ninyi mliozitenda hukumu zake; itafuteni haki, utafuteni unyenyekevu; huenda mtafichwa katika siku ya hasira ya Bwana.

4. Kwa kuwa Gaza utaachwa, na Ashkeloni utakuwa ukiwa; wataufukuzia mbali Ashdodi wakati wa adhuhuri, na Ekroni utang'olewa.

5. Ole wao wakaao karibu na pwani ya bahari, taifa la Wakerethi! Neno la Bwana li juu yenu, Ee Kanaani, nchi ya Wafilisti; mimi nitakuangamiza, asibaki mtu akaaye kwako.

6. Na hiyo nchi ya pwani itakuwa malisho, yenye vibanda vya wachungaji, na mazizi ya makundi ya kondoo.

7. Na hiyo nchi ya pwani itakuwa nchi ya watu wa nyumba ya Yuda waliosalia; watalisha makundi yao huko; watalala katika nyumba za Ashkeloni wakati wa jioni; kwa maana Bwana, Mungu wao, atawajilia na kuwarudisha wafungwa wao.

8. Mimi nimeyasikia matukano ya Moabu, na dhihaka za wana wa Amoni, ambazo kwa hizo wamewatukana watu wangu, na kujitukuza juu ya mpaka wao.

9. Basi kama niishivyo, asema Bwana wa majeshi, Mungu wa Israeli, Hakika Moabu atakuwa kama Sodoma, na wana wa Amoni kama Gomora, yaani, milki ya upupu, na mashimo ya chumvi, ukiwa wa daima; watu wangu waliosalia watawateka nyara, na watu wa taifa langu waliobaki watawarithi.

10. Mambo hayo yatawapata kwa sababu ya kiburi chao, kwa kuwa wamewatukana watu wa Bwana wa majeshi, na kujitukuza juu yao.

11. Bwana atakuwa mwenye kuwatisha sana; kwa maana atawafisha kwa njaa miungu yote ya dunia; na watu watamsujudia yeye, kila mtu toka mahali pake; naam, nchi zote za mataifa.

12. Na ninyi Wakushi pia, mtauawa kwa upanga wangu.

13. Naye atanyosha mkono wake juu ya upande wa kaskazini, na kuiangamiza Ashuru; naye ataufanya Ninawi kuwa ukiwa, kuwa mahali pakavu kama jangwa.

14. Na makundi ya wanyama watalala kati yake, wanyama wote wa mataifa; mwari-nyuni na nungu watakaa juu ya vichwa vya nguzo zake; sauti yao itasikiwa madirishani; vizingitini mwake mtakuwa ukiwa; kwa maana ameifunua kazi ya mierezi.

15. Huu ndio mji ule wa furaha, Uliokaa pasipo kufikiri, Uliosema moyoni mwake, Mimi niko, Wala hapana mwingine ila mimi. Jinsi ulivyokuwa ukiwa, Mahali pa kulala pa wanyama wa bara! Kila mtu apitaye atazomea, Na kutikisa mkono wake.

About Sefania Chapter 2

Read Sefania Chapter 2 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of Sefania in the Old Testament. Continue reading with the chapter navigation above or explore the complete book.

Book Information

Book: Sefania
Chapter: 2
Testament: Old Testament

How to Read this Chapter

Use the Previous and Next Chapter buttons to continue reading Sefania. You can also adjust the font size for comfortable reading and browse other books of the Bible using the navigation links.

https://www.youtube.com/watch?v=rzsT_Q3KLzE

More Resources

Continue Reading the Bible

Continue reading Sefania Chapter 2 and explore every book, chapter and verse of the Holy Bible. Use the navigation links above and below to move through the Scriptures with ease.

Frequently Asked Questions

What is Sefania Chapter 2?

Sefania Chapter 2 is part of the Book of Sefania in the Holy Bible.

Can I read this chapter online?

Yes. You can read the complete Sefania Chapter 2 online for free with easy chapter navigation.

More Chapters from Agano la Kale

  1. Isaya Chapter 1
  2. Isaya Chapter 6
  3. Isaya Chapter 2
  4. Isaya Chapter 14
  5. Isaya Chapter 3
  6. Isaya Chapter 7
  7. Isaya Chapter 8

Explore More from sefania

  1. Sefanía Chapter 3
  2. Sefania Chapter 1
  3. Sefania Chapter 3
  4. Sefanía Chapter 2
  5. Sefanía Chapter 1

Related Chapters & Readings

  1. 2 Wafalme Chapter 9
  2. Marko Chapter 1
  3. Mambo ya Walawi Chapter 20
  4. Zaburi Chapter 51
  5. Kumbukumbu la Torati Chapter 34
  6. Hesabu Chapter 36
  7. 2 Samweli Chapter 20
Share Your Love

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *