Ayubu Chapter 14

For English

Read Ayubu Chapter 14 Online

Read Ayubu Chapter 14 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of Ayubu in the Old Testament. Browse every verse with easy chapter navigation, continue to the next chapter, or explore the complete Book of Ayubu and the Holy Bible online.

Choose a Chapter

Ayubu 14

Sura 14

1. Mwanadamu aliyezaliwa na mwanamke Siku zake za kuishi si nyingi, naye hujaa taabu.

2. Yeye huchanua kama vile ua, kisha hukatwa; Hukimbia kama kivuli, wala hakai kamwe.

3. Nawe, je! Wafumbua macho yako kumwangalia mtu kama yeye, Na kunitia katika hukumu pamoja nawe?

4. Ni nani awezaye kutoa kitu kilicho safi kitoke katika kitu kichafu? Hapana awezaye.

5. Kwa kuwa siku zake zimeamriwa, hesabu ya miezi yake unayo wewe, Nawe umemwekea mipaka yake asiyoweza kuipita;

6. Acha kumwangalia yeye, apate kupumzika, Hata atakapoitimiza siku yake, kama aliyeajiriwa.

7. Kwani yako matumaini ya mti, ya kuwa ukikatwa utachipuka tena, Wala machipukizi yake hayatakoma.

8. Ijapokuwa mizizi yake huchakaa mchangani, Na shina lake kufa katika udongo;

9. Lakini kwa harufu ya maji utachipuka, Na kutoa matawi kama mche.

10. Lakini mwanadamu hufa, huifariki dunia; Naam, mwanadamu hutoa roho, naye yupo wapi?

11. Kama vile maji kupwa katika bahari, Na mto kupunguka na kukatika;

12. Ni vivyo mwanadamu hulala chini, asiinuke; Hata wakati wa mbingu kutokuwako tena, hawataamka, Wala kuamshwa usingizini.

13. Laiti ungenificha kuzimuni, Ukanilinda kwa siri, hata ghadhabu zako zitakapopita, Na kuniandikia muda ulioamriwa, na kunikumbuka!

14. Mtu akifa, je! Atakuwa hai tena? Mimi ningengoja siku zote za vita vyangu, Hata kufunguliwa kwangu kunifikilie.

15. Wewe ungeita, nami ningekujibu; Ungekuwa na tamaa ya kazi ya mikono yako.

16. Lakini sasa wazihesabu hatua zangu; Je! Huchungulii dhambi yangu?

17. Kosa langu limetiwa muhuri mfukoni, Nawe waufunga uovu wangu.

18. Lakini, tazama, mlima ukianguka hutoweka, Nalo jabali huondolewa mahali pake;

19. Maji mengi huyapunguza mawe; Mafuriko yake huuchukua mchanga wa nchi; Nawe matumaini ya wanadamu wayaangamiza.

20. Wewe wamshinda nguvu sikuzote, naye hupita aende zake Wabadili sura zake, na kumpeleka aondoke.

21. Wanawe hufikilia heshima, wala yeye hajui; Kisha wao huaibishwa, lakini yeye hana habari zao.

22. Lakini mwili ulio juu yake una maumivu, Na nafsi yake ndani huomboleza.

About Ayubu Chapter 14

Read Ayubu Chapter 14 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of Ayubu in the Old Testament. Continue reading with the chapter navigation above or explore the complete book.

Book Information

Book: Ayubu
Chapter: 14
Testament: Old Testament

How to Read this Chapter

Use the Previous and Next Chapter buttons to continue reading Ayubu. You can also adjust the font size for comfortable reading and browse other books of the Bible using the navigation links.

https://www.youtube.com/watch?v=rzsT_Q3KLzE

More Resources

Continue Reading the Bible

Continue reading Ayubu Chapter 14 and explore every book, chapter and verse of the Holy Bible. Use the navigation links above and below to move through the Scriptures with ease.

Frequently Asked Questions

What is Ayubu Chapter 14?

Ayubu Chapter 14 is part of the Book of Ayubu in the Holy Bible.

Can I read this chapter online?

Yes. You can read the complete Ayubu Chapter 14 online for free with easy chapter navigation.

More Chapters from Agano la Kale

  1. Zaburi Chapter 1
  2. Habakuki Chapter 3
  3. Ayubu Chapter 1
  4. Zaburi Chapter 2
  5. Kutoka Chapter 11
  6. Kutoka Chapter 2
  7. Ayubu Chapter 4

Explore More from Ayubu

  1. Ayubu Chapter 42
  2. Ayubu Chapter 22
  3. Ayubu Chapter 29
  4. Ayubu Chapter 16
  5. Ayubu Chapter 11
  6. Ayubu Chapter 34
  7. Ayubu Chapter 37

Related Chapters & Readings

  1. Warumi Chapter 3
  2. 1 Mambo ya Nyakati Chapter 14
  3. Yohana Chapter 2
  4. 1 Mambo ya Nyakati Chapter 3
  5. Zaburi Chapter 125
  6. 1 Wafalme Chapter 14
  7. Zaburi Chapter 39
Share Your Love

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *