Ayubu Chapter 20

For English

Read Ayubu Chapter 20 Online

Read Ayubu Chapter 20 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of Ayubu in the Old Testament. Browse every verse with easy chapter navigation, continue to the next chapter, or explore the complete Book of Ayubu and the Holy Bible online.

Choose a Chapter

Ayubu 20

Sura 20

1. Ndipo Sofari, Mnaamathi, akajibu, na kusema,

2. Kwa hiyo mawazo yangu hunipa jawabu, Kwa ajili ya haraka niliyo nayo ndani yangu.

3. Nimesikia maonyo yanayonitahayarisha, Nayo roho ya ufahamu wangu hunijibu.

4. Je! Hujui neno hili tangu zamani za kale, Tangu wanadamu kuwekwa juu ya nchi,

5. Ya kuwa shangwe ya waovu ni kwa muda kidogo, Na furaha ya wapotovu ni ya dakika moja tu?

6. Ujapopanda ukuu wake mpaka mbinguni, Na kichwa chake kufikilia mawinguni;

7. Hata hivyo ataangamia milele kama mavi yake mwenyewe; Hao waliomwona watasema, Yuko wapi?

8. Ataruka mfano wa ndoto, asionekane; Naam, atafukuzwa kama maono ya usiku,

9. Jicho lililomwona halitamwona tena; Wala mahali pake hapatamtazama tena.

10. Watoto wake watataka fadhili kwa maskini, Na mikono yake itarudisha mali yake.

11. Mifupa yake imejaa ujana wake, Lakini utalala nchi naye mavumbini.

12. Ingawa uovu una tamu kinywani mwake, Ingawa auficha chini ya ulimi wake;

13. Ingawa auhurumia, asikubali kuuacha uende zake. Lakini akaushika vivyo kinywani mwake;

14. Hata hivyo chakula chake matumboni mwake kinabadilika, Kimekuwa ni nyongo za majoka ndani yake.

15. Amemeza mali, naye atayatapika tena; Mungu atayatoa tumboni mwake.

16. Ataamwa sumu ya majoka; Na ulimi wa fira utamwua.

17. Hataiangalia hiyo mito ya maji, Vile vijito vilivyojaa asali na siagi.

18. Aliyoyataabikia kazi atayarudisha, asiyameze; Kwa mali aliyoyapata, hatafurahi.

19. Kwa maana amewaonea na kuwaacha maskini; Amenyang'anya nyumba kwa jeuri, wala hataijenga.

20. Kwa sababu hakujua utulivu ndani yake, Hataponya cho chote katika hicho alichokifurahia.

21. Hakikusalia kitu asichokula; Kwa hiyo kufanikiwa kwake hakutadumu.

22. Katika kujaa kwa wingi wake atakuwa katika dhiki; Mkono wa kila anayesumbuliwa utamjia.

23. Hapo atakapo kulijaza tumbo lake, Mungu atamtupia ukali wa ghadhabu zake, Na kuunyesha juu yake akiwa anakula.

24. Ataikimbia silaha ya chuma, Na uta wa shaba utamchoma kwa pili.

25. Yeye autoa, nao watoka mwilini mwake; Naam, ncha ing'aayo yatoka katika nyongo yake; Vitisho viko juu yake.

26. Giza lote linawekwa kwa ajili ya hazina zake; Moto ambao haukuvuviwa na mtu utamla; Utayateketeza yaliyosalia hemani mwake.

27. Mbingu zitafunua wazi uovu wake, Nayo nchi itainuka kinyume chake.

28. Maongeo ya nyumba yake yataondoka, Yatamwagika mbali katika siku ya ghadhabu zake.

29. Hii ndiyo sehemu ya mtu mwovu itokayo kwa Mungu, Na urithi aliowekewa na Mungu.

About Ayubu Chapter 20

Read Ayubu Chapter 20 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of Ayubu in the Old Testament. Continue reading with the chapter navigation above or explore the complete book.

Book Information

Book: Ayubu
Chapter: 20
Testament: Old Testament

How to Read this Chapter

Use the Previous and Next Chapter buttons to continue reading Ayubu. You can also adjust the font size for comfortable reading and browse other books of the Bible using the navigation links.

https://www.youtube.com/watch?v=rzsT_Q3KLzE

More Resources

Continue Reading the Bible

Continue reading Ayubu Chapter 20 and explore every book, chapter and verse of the Holy Bible. Use the navigation links above and below to move through the Scriptures with ease.

Frequently Asked Questions

What is Ayubu Chapter 20?

Ayubu Chapter 20 is part of the Book of Ayubu in the Holy Bible.

Can I read this chapter online?

Yes. You can read the complete Ayubu Chapter 20 online for free with easy chapter navigation.

More Chapters from Agano la Kale

  1. Isaya Chapter 1
  2. Isaya Chapter 2
  3. Isaya Chapter 3
  4. Isaya Chapter 6
  5. Isaya Chapter 7
  6. Isaya Chapter 14
  7. Isaya Chapter 5

Explore More from Ayubu

  1. Ayubu Chapter 12
  2. Ayubu Chapter 7
  3. Ayubu Chapter 41
  4. Ayubu Chapter 5
  5. Ayubu Chapter 36
  6. Ayubu Chapter 32
  7. Ayubu Chapter 8

Related Chapters & Readings

  1. 2 Samweli Chapter 21
  2. Mika Chapter 1
  3. Mathayo Chapter 17
  4. Ayubu Chapter 38
  5. Yoeli Chapter 2
  6. Zaburi Chapter 77
  7. Zaburi Chapter 48
Share Your Love

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *