Read Ayubu Chapter 12 Online
Read Ayubu Chapter 12 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of Ayubu in the Old Testament. Browse every verse with easy chapter navigation, continue to the next chapter, or explore the complete Book of Ayubu and the Holy Bible online.
Choose a Chapter
Ayubu 12
Sura 12
1. Ndipo Ayubu akajibu, na kusema,
2. Hapana shaka ninyi ndinyi watu halisi, Nanyi mtakapokufa, ndipo na hekima itakoma.
3. Lakini mimi pia, nina fahamu kama ninyi; Mimi si duni yenu ninyi; Naam, ni nani asiyejua mambo kama hayo?
4. Mimi ni mtu wa kuchekwa na jirani yake, Ni mtu niliyemwita Mungu, naye akanijibu; Huyo mwenye haki, aliye mtimilifu, amekuwa ni kicheko.
5. Katika mawazo yake huyo aliye na raha mna kudharau mashaka; Tayari kwa ajili ya wenye kuteleza miguu.
6. Hema za wapokonyi hufanikiwa, Na hao wamkasirishao Mungu hukaa salama; Mikononi mwao Mungu huleta vitu vingi.
7. Lakini sasa waulize hao wanyama, nao watakufundisha; Na nyuni wa angani, nao watakuambia;
8. Au nena na nchi, nayo itakufundisha; Nao samaki wa baharini watakutangazia.
9. Katika hawa wote ni yupi asiyejua, Kwamba ni mkono wa Bwana uliofanya haya?
10. Ambaye nafsi ya kila kilicho hai i mkononi mwake, Na pumzi zao wanadamu wote.
11. Je! Sikio silo lijaribulo maneno, Kama vile kaakaa lionjavyo chakula?
12. Wazee ndio walio na hekima, Na katika kuishi siku nyingi iko fahamu.
13. Hekima na amri zina yeye [Mungu]; Yeye anayo mashauri na fahamu.
14. Tazama, yuavunja, wala haiwezekani kujenga tena; Humfunga mtu, wala haiwezekani kumfungua.
15. Tazama, yuayazuia maji, nayo yakatika; Tena, huyapeleka, nayo yaipindua dunia.
16. Kwake yeye ziko nguvu, na makusudi kufanikiwa; Huyo adanganywaye, na mdanganyi pia ni wake.
17. Yeye huwaondoa washauri hali wametekwa nyara, Naye huwafanya waamuzi kuwa ni wapumbavu.
18. Yeye hulegeza kifungo cha wafalme, Na kuwafunga viuno vyao kwa mshipi.
19. Yeye huwaondoa makuhani hali wametekwa nyara. Na kuwapindua mashujaa.
20. Huondoa matamko ya hao walioaminiwa, Na kuondoa fahamu za wazee.
21. Humwaga aibu juu ya hao wakuu, Na kulegeza mshipi wa wenye nguvu.
22. Huvumbua mambo ya siri tokea gizani, Na hicho kilicho giza tupu huleta mwangani.
23. Huyaongeza mataifa, na kuyaangamiza; Huyaeneza mataifa mbali, na kuyaacha.
24. Huwaondolea moyo wakuu wa watu wa nchi, Na kuwapoteza nyikani pasipokuwa na njia.
25. Wao hupapasa gizani pasipokuwa na mwanga, Naye huwafanya kupepesuka kama vile mlevi.
About Ayubu Chapter 12
Read Ayubu Chapter 12 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of Ayubu in the Old Testament. Continue reading with the chapter navigation above or explore the complete book.
Book Information
Book: Ayubu
Chapter: 12
Testament: Old Testament
How to Read this Chapter
Use the Previous and Next Chapter buttons to continue reading Ayubu. You can also adjust the font size for comfortable reading and browse other books of the Bible using the navigation links.
More Resources
Continue Reading the Bible
Continue reading Ayubu Chapter 12 and explore every book, chapter and verse of the Holy Bible. Use the navigation links above and below to move through the Scriptures with ease.
Frequently Asked Questions
What is Ayubu Chapter 12?
Ayubu Chapter 12 is part of the Book of Ayubu in the Holy Bible.
Can I read this chapter online?
Yes. You can read the complete Ayubu Chapter 12 online for free with easy chapter navigation.
More Chapters from Agano la Kale
- Zaburi Chapter 1
- Habakuki Chapter 3
- Ayubu Chapter 1
- Zaburi Chapter 2
- Kutoka Chapter 11
- Kutoka Chapter 2
- Ayubu Chapter 4
Explore More from Ayubu
- Ayubu Chapter 40
- Ayubu Chapter 27
- Ayubu Chapter 37
- Ayubu Chapter 3
- Ayubu Chapter 17
- Ayubu Chapter 7
- Ayubu Chapter 39