Read Ayubu Chapter 33 Online
Read Ayubu Chapter 33 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of Ayubu in the Old Testament. Browse every verse with easy chapter navigation, continue to the next chapter, or explore the complete Book of Ayubu and the Holy Bible online.
Choose a Chapter
Ayubu 33
Sura 33
1. Walakini, Ayubu, nakuomba usikilize matamko yangu, Ukayasikilize maneno yangu yote.
2. Tazama basi, nimefunua kinywa changu, Ulimi wangu umenena kinywani mwangu.
3. Maneno yangu yatatamka uelekevu wa moyo wangu; Na hayo niyajuayo midomo yangu itayanena kwa unyofu.
4. Roho ya Mungu imeniumba, Na pumzi za Mwenyezi hunipa uhai.
5. Kwamba waweza, nijibu; Yapange maneno yako sawasawa mbele yangu, usimame.
6. Tazama, mimi ni mbele ya Mungu kama ulivyo wewe; Mimi nami nilifinyangwa katika udongo.
7. Tazama, utisho wangu hautakutia hofu wewe, Wala sitakulemea kwa uzito.
8. Hakika umenena masikioni mwangu, Nami nimesikia sauti ya maneno yako, ukisema,
9. Mimi ni safi, sina makosa; Sina hatia, wala hapana uovu ndani yangu;
10. Tazama, yuaona sababu za kufarakana nami, Hunihesabu kuwa ni adui yake;
11. Hunitia miguu yangu katika mkatale, Na mapito yangu yote huyapeleleza.
12. Tazama, nitakujibu, katika neno hili huna haki; Kwa maana Mungu ni mkuu kuliko mwanadamu.
13. Nawe kwani kumnung'unikia, Kwa vile asivyotoa hesabu ya mambo yake yote?
14. Kwa kuwa Mungu hunena mara moja, Naam, hata mara ya pili, ajapokuwa mtu hajali.
15. Katika ndoto, katika maono ya usiku, Usingizi mzito uwajiliapo watu, Katika usingizi kitandani;
16. Ndipo huyafunua masikio ya watu, Na kuyatia muhuri mafundisho yao,
17. Ili amwondoe mtu katika makusudio yake, Na kumfichia mtu kiburi;
18. Yeye huizuia nafsi yake isiende shimoni, Na uhai wake usiangamie kwa upanga.
19. Yeye hutiwa adabu kwa maumivu kitandani mwake, Na kwa mashindano yaendeleayo daima mifupani mwake;
20. Hata roho yake huchukia chakula, Na nafsi yake huchukia nyama nzuri.
21. Nyama ya mwili wake huliwa, isionekane; Na mifupa yake isiyoonekana yatokea nje.
22. Naam, nafsi yake inakaribia shimoni, Na uhai wake unakaribia waangamizi.
23. Kwamba akiwapo malaika pamoja naye, Mkalimani, mmoja katika elfu, Ili kumwonyesha binadamu hayo yampasayo;
24. Ndipo amwoneapo rehema, na kusema, Mwokoe asishuke shimoni; Mimi nimeuona ukombozi.
25. Nyama ya mwili wake itakuwa laini kuliko ya mtoto; Huzirudia siku za ujana wake;
26. Yeye humwomba Mungu, naye akamtakabalia; Hata auone uso wake kwa furaha; Naye humrejezea mtu haki yake.
27. Yeye huimba mbele ya watu, na kusema, Mimi nimefanya dhambi, na kuyapotosha hayo yaliyoelekea, Wala sikulipizwa jambo hilo;
28. Yeye ameikomboa nafsi yangu isiende shimoni, Na uhai wangu utautazama mwanga.
29. Tazama, hayo yote ni Mungu anayeyafanya, Mara mbili, naam, hata mara tatu, kwa mtu,
30. Ili kurudisha roho yake itoke shimoni, Ili atiwe mwanga kwa mwanga wa walio hai.
31. Angalia sana, Ee Ayubu, unisikilize; Nyamaza, mimi nitasema.
32. Kama una neno la kusema, nijibu; Nena, kwani nataka kukuhesabia kuwa na haki.
33. Kama sivyo, unisikilize mimi; Nyamaza, nami nitakufunza hekima.
About Ayubu Chapter 33
Read Ayubu Chapter 33 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of Ayubu in the Old Testament. Continue reading with the chapter navigation above or explore the complete book.
Book Information
Book: Ayubu
Chapter: 33
Testament: Old Testament
How to Read this Chapter
Use the Previous and Next Chapter buttons to continue reading Ayubu. You can also adjust the font size for comfortable reading and browse other books of the Bible using the navigation links.
More Resources
Continue Reading the Bible
Continue reading Ayubu Chapter 33 and explore every book, chapter and verse of the Holy Bible. Use the navigation links above and below to move through the Scriptures with ease.
Frequently Asked Questions
What is Ayubu Chapter 33?
Ayubu Chapter 33 is part of the Book of Ayubu in the Holy Bible.
Can I read this chapter online?
Yes. You can read the complete Ayubu Chapter 33 online for free with easy chapter navigation.
More Chapters from Agano la Kale
- Zaburi Chapter 1
- Habakuki Chapter 3
- Ayubu Chapter 1
- Zaburi Chapter 2
- 1 Samweli Chapter 1
- Kutoka Chapter 11
- Kutoka Chapter 2
Explore More from Ayubu
- Ayubu Chapter 17
- Ayubu Chapter 32
- Ayubu Chapter 24
- Ayubu Chapter 31
- Ayubu Chapter 18
- Ayubu Chapter 15
- Ayubu Chapter 14