Ayubu Chapter 24

For English

Read Ayubu Chapter 24 Online

Read Ayubu Chapter 24 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of Ayubu in the Old Testament. Browse every verse with easy chapter navigation, continue to the next chapter, or explore the complete Book of Ayubu and the Holy Bible online.

Choose a Chapter

Ayubu 24

Sura 24

1. Mbona nyakati zisiwekwe na Mwenyezi? Na hao wamjuao mbona hawazioni siku zake?

2. Wako waziondoao alama za mipaka; Huyachukua makundi kwa jeuri na kuyalisha.

3. Humfukuza punda wake asiye baba, Humtwaa rehani ng'ombe wake mwanamke mjane.

4. Humgeuza mhitaji aiache njia; Maskini wa nchi hujificha pamoja.

5. Tazama, kama punda-mwitu jangwani Wao hutoka kwenda kazini mwao, wakitafuta chakula kwa bidii; Jangwa huwapa chakula cha watoto wao.

6. Hukata nafaka zao mashambani; Na kuokota zabibu za waovu.

7. Hujilaza usiku kucha uchi pasipo nguo, Wala hawana cha kujifunika baridi.

8. Hutota kwa manyunyo ya milimani, Na kuambatana na jabali kwa kukosa sitara,

9. Wako wamwondoao matitini kwa nguvu huyo asiye na baba, Na kutwaa rehani kwa maskini;

10. Hata wazunguke uchi pasipo mavazi, Nao wakiwa na njaa huchukua miganda;

11. Hushindika mafuta ndani ya makuta ya watu hao; Wakanyaga mashinikizo, nao wana kiu.

12. Watu huugua toka mji ulio na watu wengi, Na roho yake aliyejeruhiwa hupiga ukelele; Wala Mungu hauangalii upumbavu.

13. Hawa ni katika hao waliouasi mwanga; Hawazijui njia zake, Wala hawakai katika mapito yake.

14. Mwuaji huamka asubuhi kukipambauka, huwaua maskini na wahitaji; Tena wakati wa usiku yu kama mwivi.

15. Tena jicho lake mzinifu hungojea wakati wa giza-giza, Akisema, Hapana jicho litakaloniona; Naye huuficha uso wake.

16. Wao hutoboa nyumba gizani; Hujifungia ndani wakati wa mchana; Hawaujui mwanga.

17. Kwani asubuhi kwao wote ni kama giza tupu; Kwani wao wavijua vitisho vya hiyo giza tupu.

18. Mwasema, Yeye ni mwepesi juu ya uso wa gharika; Sehemu yao inalaaniwa duniani; Hageuki kwenda njia ya mizabibuni.

19. Chaka na hari hukausha maji ya theluji; Kuzimu nako hao ambao wamefanya dhambi.

20. Tumbo lililomzaa litamsahau; buu litamla na kuona tamu; Hatakumbukwa tena; Na udhalimu utavunjwa kama mti.

21. Naam, yeye huwala walio tasa wasiozaa; Wala hamtendei mema mwanamke mjane.

22. Lakini Mungu huwadumisha wenye uwezo kwa nguvu zake; Huinuka, wasiokuwa na tumaini la kuishi.

23. Huwapa kuwa na salama, nao wapumzika kwayo; Na macho yake ya juu ya njia zao.

24. Wao wametukuzwa; lakini kitambo kidogo hutoweka; Naam, hushushwa, na kuondolewa njiani kama wengine wote, Nao hukatwa kama vile masuke ya ngano.

25. Na kama sivyo sasa, ni nani atakayenihukumu kuwa ni mwongo, Na kuyafanya maneno yangu kuwa si kitu?

About Ayubu Chapter 24

Read Ayubu Chapter 24 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of Ayubu in the Old Testament. Continue reading with the chapter navigation above or explore the complete book.

Book Information

Book: Ayubu
Chapter: 24
Testament: Old Testament

How to Read this Chapter

Use the Previous and Next Chapter buttons to continue reading Ayubu. You can also adjust the font size for comfortable reading and browse other books of the Bible using the navigation links.

https://www.youtube.com/watch?v=rzsT_Q3KLzE

More Resources

Continue Reading the Bible

Continue reading Ayubu Chapter 24 and explore every book, chapter and verse of the Holy Bible. Use the navigation links above and below to move through the Scriptures with ease.

Frequently Asked Questions

What is Ayubu Chapter 24?

Ayubu Chapter 24 is part of the Book of Ayubu in the Holy Bible.

Can I read this chapter online?

Yes. You can read the complete Ayubu Chapter 24 online for free with easy chapter navigation.

More Chapters from Agano la Kale

  1. Zaburi Chapter 1
  2. Habakuki Chapter 3
  3. Ayubu Chapter 1
  4. Zaburi Chapter 2
  5. 1 Samweli Chapter 1
  6. Kutoka Chapter 11
  7. Kutoka Chapter 2

Explore More from Ayubu

  1. Ayubu Chapter 20
  2. Ayubu Chapter 21
  3. Ayubu Chapter 11
  4. Ayubu Chapter 33
  5. Ayubu Chapter 22
  6. Ayubu Chapter 35
  7. Ayubu Chapter 27

Related Chapters & Readings

  1. 2 Wathesalonike Chapter 3
  2. 1 Mambo ya Nyakati Chapter 16
  3. 1 Samweli Chapter 24
  4. Filemoni Chapter 1
  5. 1 Wakorintho Chapter 5
  6. 2 Mambo ya Nyakati Chapter 33
  7. Hesabu Chapter 17
Share Your Love

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *