Read Ayubu Chapter 23 Online
Read Ayubu Chapter 23 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of Ayubu in the Old Testament. Browse every verse with easy chapter navigation, continue to the next chapter, or explore the complete Book of Ayubu and the Holy Bible online.
Choose a Chapter
Ayubu 23
Sura 23
1. Ndipo Ayubu akajibu, na kusema,
2. Hata leo mashitaka yangu yana uchungu; Pigo langu ni zito zaidi ya kuugua kwangu.
3. Laiti ningejua mahali niwezapo kumwona, Nifike hata hapo anapokaa!
4. Ningeiweka daawa yangu mbele yake, Na kukijaza kinywa changu hoja.
5. Ningeyajua maneno atakayonijibu, Na kuelewa na hayo atakayoniambia.
6. Je! Angeshindana nami kwa ukuu wa uwezo wake? La, lakini angenisikiliza.
7. Hapo walekevu wangepata kuhojiana naye; Basi hivyo ningeachiliwa na mwamuzi wangu milele.
8. Tazama, naenda mbele, wala hayuko; Narudi nyuma, lakini siwezi kumwona;
9. Na mkono wa kushoto, afanyapo kazi, lakini siwezi kumwona; Hujificha upande wa kuume, hata nisimwone.
10. Lakini yeye aijua njia niendeayo; Akisha kunijaribu, nitatoka kama dhahabu.
11. Mguu wangu umeshikamana sana na hatua zake; Njia yake nimeishika, wala sikukengeuka.
12. Sikurudi nyuma kuiacha amri ya midomo yake; Nimeyatunza maneno ya kinywa chake zaidi ya riziki yangu,
13. Lakini yeye ni mmoja, ni nani awezaye kumgeuza? Tena nafsi yake ilitakalo, ndilo afanyalo.
14. Kwani yeye hulitimiliza hilo nililoamuriwa; Tena mambo mengi kama hayo ya pamoja naye.
15. Kwa hiyo naona taabu mbele ya uso wake; Nitakapofikiri, namwogopa.
16. Kwani Mungu ameufanya moyo wangu kuzimia, Naye Mwenyezi amenitaabisha;
17. Maana sikufadhaishwa kwa sababu ya giza, Wala kwa sababu giza kuu limenifunika uso.
About Ayubu Chapter 23
Read Ayubu Chapter 23 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of Ayubu in the Old Testament. Continue reading with the chapter navigation above or explore the complete book.
Book Information
Book: Ayubu
Chapter: 23
Testament: Old Testament
How to Read this Chapter
Use the Previous and Next Chapter buttons to continue reading Ayubu. You can also adjust the font size for comfortable reading and browse other books of the Bible using the navigation links.
More Resources
Continue Reading the Bible
Continue reading Ayubu Chapter 23 and explore every book, chapter and verse of the Holy Bible. Use the navigation links above and below to move through the Scriptures with ease.
Frequently Asked Questions
What is Ayubu Chapter 23?
Ayubu Chapter 23 is part of the Book of Ayubu in the Holy Bible.
Can I read this chapter online?
Yes. You can read the complete Ayubu Chapter 23 online for free with easy chapter navigation.
More Chapters from Agano la Kale
- Isaya Chapter 1
- Isaya Chapter 2
- Isaya Chapter 6
- Isaya Chapter 3
- Isaya Chapter 7
- Isaya Chapter 5
- Isaya Chapter 14
Explore More from Ayubu
- Ayubu Chapter 28
- Ayubu Chapter 32
- Ayubu Chapter 20
- Ayubu Chapter 41
- Ayubu Chapter 13
- Ayubu Chapter 31
- Ayubu Chapter 19