Ayubu Chapter 41

For English

Read Ayubu Chapter 41 Online

Read Ayubu Chapter 41 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of Ayubu in the Old Testament. Browse every verse with easy chapter navigation, continue to the next chapter, or explore the complete Book of Ayubu and the Holy Bible online.

Choose a Chapter

Ayubu 41

Sura 41

1. Je! Waweza wewe kumvua mamba kwa ndoana? Au, kuufunga ulimi wake kwa kamba?

2. Je! Waweza kutia kamba puani mwake? Au kutoboa taya yake kwa kulabu?

3. Je! Atakusihi sana? Au, atakuambia maneno ya upole?

4. Je! Atafanya agano pamoja nawe, Umtwae kuwa mtumishi wako milele?

5. Je! Utamchezea kama ndege? Au, kumfunga kwa ajili ya wasichana wako?

6. Je! Vikosi vya wavuvi watamfanyia biashara? Watamgawanya kati ya wafanyao biashara?

7. Je! Waweza kuijaza ngozi yake na vyuma vyenye ncha, Au kichwa chake kwa vyusa?

8. Mwekee mkono wako; Vikumbuke vile vita, wala usifanye tena.

9. Tazama, kumtamani ni bure; Je! Hatambwaga chini huyo atakayemtazama?

10. Hapana aliye mkali hata akathubutu kumwamsha; Bali ni nani awezaye kusimama mbele yangu mimi?

11. Ni nani aliyetangulia kunipa hata nimlipe? Kila kilicho chini ya mbingu nzima ni changu.

12. Sitanyamaa kusema habari za via vyake, Wala nguvu zake kuu, wala umbo lake zuri.

13. Ni nani awezaye kumbambua magamba yake? Ni nani atakayepenya dirii yake maradufu?

14. Ni nani awezaye kuifungua milango ya uso wake? Meno yake yatisha kandokando yake.

15. Magamba yake yenye nguvu ndiyo fahari yake, Yamefungamana pamoja kama kwa kufungwa kwa muhuri.

16. Jinsi yalivyoshikamana Hata upepo hauwezi kupita kati.

17. Yamefungamana pamoja; Yameshikamana, hata hayawezekani kutengwa.

18. Kwa kuchemua kwake mwanga humemetuka, Na macho yake yanafanana na makope ya alfajiri.

19. Mienge iwakayo hutoka kinywani mwake, Na macheche ya moto huruka nje.

20. Moshi hutoka katika mianzi ya pua yake, Kama nyungu ikitokota, na manyasi yawakayo.

21. Pumzi zake huwasha makaa, Na miali ya moto hutoka kinywani mwake.

22. Katika shingo yake hukaa nguvu, Na utisho hucheza mbele yake.

23. Manofu ya nyama yake hushikamana; Yanakazana juu yake; hayawezi kuondolewa.

24. Moyo wake una imara kama jiwe; Naam, imara kama jiwe la chini la kusagia.

25. Anapojiinua, mashujaa huogopa; Kwa sababu ya woga wao huvunjwa moyo.

26. Mtu akimpiga kwa upanga, haumwingii; Wala fumo, wala mshale, wala mkuki wenye ncha.

27. Yeye huona chuma kuwa kama nyasi, Na shaba kama mti uliooza.

28. Mshale hauwezi kumkimbiza; Na mawe ya teo kwake hugeuka kuwa kama makapi.

29. Marungu huhesabiwa kama mabua; Naye hucheka mshindo wa mkuki ukitupwa.

30. Pande zake za chini ni kama vigae vikali; Hutandika malazi kama kuweka chombo cha kupuria nafaka juu ya matope.

31. Yeye huchemsha kilindi mfano wa nyungu; Hufanya bahari kuwa kama mafuta.

32. Hufanya mapito yake kung'aa nyuma yake Hata mtu angedhani kilindi kina mvi.

33. Juu ya nchi hapana aliyefanana naye, Aliyeumbwa pasipo oga.

34. Yeye hutazama kila kitu kilicho juu; Ni mfalme juu ya wote wenye kiburi.

About Ayubu Chapter 41

Read Ayubu Chapter 41 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of Ayubu in the Old Testament. Continue reading with the chapter navigation above or explore the complete book.

Book Information

Book: Ayubu
Chapter: 41
Testament: Old Testament

How to Read this Chapter

Use the Previous and Next Chapter buttons to continue reading Ayubu. You can also adjust the font size for comfortable reading and browse other books of the Bible using the navigation links.

https://www.youtube.com/watch?v=rzsT_Q3KLzE

More Resources

Continue Reading the Bible

Continue reading Ayubu Chapter 41 and explore every book, chapter and verse of the Holy Bible. Use the navigation links above and below to move through the Scriptures with ease.

Frequently Asked Questions

What is Ayubu Chapter 41?

Ayubu Chapter 41 is part of the Book of Ayubu in the Holy Bible.

Can I read this chapter online?

Yes. You can read the complete Ayubu Chapter 41 online for free with easy chapter navigation.

More Chapters from Agano la Kale

  1. Isaya Chapter 1
  2. Isaya Chapter 2
  3. Isaya Chapter 6
  4. Isaya Chapter 3
  5. Isaya Chapter 7
  6. Isaya Chapter 5
  7. Isaya Chapter 14

Explore More from Ayubu

  1. Ayubu Chapter 32
  2. Ayubu Chapter 15
  3. Ayubu Chapter 23
  4. Ayubu Chapter 18
  5. Ayubu Chapter 35
  6. Ayubu Chapter 19
  7. Ayubu Chapter 3

Related Chapters & Readings

  1. Wimbo Ulio Bora Chapter 4
  2. Mambo ya Walawi Chapter 4
  3. 1 Samweli Chapter 3
  4. Zaburi Chapter 66
  5. Warumi Chapter 8
  6. Hesabu Chapter 17
  7. Mwanzo Chapter 40
Share Your Love

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *