1 Mambo ya Nyakati Chapter 14

For English

Read 1 Mambo ya Nyakati Chapter 14 Online

Read 1 Mambo ya Nyakati Chapter 14 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of 1 Mambo ya Nyakati in the Old Testament. Browse every verse with easy chapter navigation, continue to the next chapter, or explore the complete Book of 1 Mambo ya Nyakati and the Holy Bible online.

Choose a Chapter

1 Mambo ya Nyakati 14

Sura 14

1. Naye Hiramu, mfalme wa Tiro, akatuma wajumbe kwa Daudi, akampelekea na mierezi, na waashi, na maseremala, ili wamjengee nyumba.

2. Daudi akajua ya kwamba Bwana amemweka imara ili amiliki juu ya Israeli, kwa kuwa milki yake imeinuka kwa ajili ya watu wake Israeli.

3. Tena Daudi akazidi kuoa wake huko Yerusalemu; akazidi Daudi kuzaa wana na binti.

4. Na haya ndiyo majina ya watoto aliozaliwa huko Yerusalemu; Shamua, na Shobabu, na Nathani, na Sulemani;

5. na Ibhari, na Elishua, na Elpeleti;

6. na Noga, na Nefegi, na Yafia;

7. na Elishama, na Eliada, na Elifeleti.

8. Na waliposikia hao Wafilisti ya kwamba Daudi ametiwa mafuta ili awe mfalme juu ya Israeli wote, Wafilisti wote wakapanda kumtafuta Daudi; naye Daudi akasikia, akatoka nje kupigana nao.

9. Basi hao Wafilisti walikuwa wamekuja na kuteka nyara katika bonde la Warefai.

10. Daudi akamwuliza Mungu, kusema, Je! Nipande juu ya Wafilisti! Utawatia mikononi mwangu? Naye Bwana akamwambia, Panda; kwa kuwa nitawatia mikononi mwako.

11. Basi wakapanda mpaka Baal-perasimu, Daudi naye akawapiga huko; Daudi akasema, Bwana amewafurikia adui zangu kwa mkono wangu, kama mafuriko ya maji. Basi wakapaita mahali pale jina lake Baal-perasimu.

12. Nao wakaiacha miungu yao huko; naye Daudi akaamuru, ikateketezwa kwa moto.

13. Lakini hao Wafilisti wakateka nyara tena mara ya pili bondeni.

14. Na Daudi akamwuliza Mungu tena; naye Mungu akamwambia, Hutapanda kuwafuata; uwageukie mbali, ukawajie huko kuielekea miforsadi.

15. Kisha itakuwa utakapoisikia sauti ya kwenda katika vilele vya miforsadi, ndipo utakapokwenda nje vitani; kwa maana ndipo Mungu ametoka mbele yako, awapige jeshi la Wafilisti.

16. Daudi akafanya kama vile Mungu alivyomwamuru; wakawapiga jeshi la Wafilisti toka Geba mpaka Gezeri.

17. Sifa za Daudi zikafika nchi zote; naye Bwana akawaletea mataifa yote hofu yake.

About 1 Mambo ya Nyakati Chapter 14

Read 1 Mambo ya Nyakati Chapter 14 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of 1 Mambo ya Nyakati in the Old Testament. Continue reading with the chapter navigation above or explore the complete book.

Book Information

Book: 1 Mambo ya Nyakati
Chapter: 14
Testament: Old Testament

How to Read this Chapter

Use the Previous and Next Chapter buttons to continue reading 1 Mambo ya Nyakati. You can also adjust the font size for comfortable reading and browse other books of the Bible using the navigation links.

https://www.youtube.com/watch?v=rzsT_Q3KLzE

More Resources

Continue Reading the Bible

Continue reading 1 Mambo ya Nyakati Chapter 14 and explore every book, chapter and verse of the Holy Bible. Use the navigation links above and below to move through the Scriptures with ease.

Frequently Asked Questions

What is 1 Mambo ya Nyakati Chapter 14?

1 Mambo ya Nyakati Chapter 14 is part of the Book of 1 Mambo ya Nyakati in the Holy Bible.

Can I read this chapter online?

Yes. You can read the complete 1 Mambo ya Nyakati Chapter 14 online for free with easy chapter navigation.

More Chapters from 1-mambo-ya-nyakati

  1. 1 Mambo ya Nyakati Chapter 17
  2. 1 Mambo ya Nyakati Chapter 6
  3. 1 Mambo ya Nyakati Chapter 25
  4. 1 Mambo ya Nyakati Chapter 2
  5. 1 Mambo ya Nyakati Chapter 1
  6. 1 Mambo ya Nyakati Chapter 15
  7. 1 Mambo ya Nyakati Chapter 28

Explore More from Agano la Kale

  1. Zaburi Chapter 15
  2. Kumbukumbu la Torati Chapter 15
  3. Yeremia Chapter 47
  4. 2 Wafalme Chapter 20
  5. 2 Mambo ya Nyakati Chapter 7
  6. 2 Mambo ya Nyakati Chapter 22
  7. Zaburi Chapter 46

Related Chapters & Readings

  1. Kumbukumbu la Torati Chapter 24
  2. Mwanzo Chapter 10
  3. 1 Mambo ya Nyakati Chapter 10
  4. 1 Mambo ya Nyakati Chapter 5
  5. Nehemia Chapter 1
  6. Ayubu Chapter 27
  7. Nehemia Chapter 11
Share Your Love

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *