Ezekieli Chapter 46

For English

Read Ezekieli Chapter 46 Online

Read Ezekieli Chapter 46 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of Ezekieli in the Old Testament. Browse every verse with easy chapter navigation, continue to the next chapter, or explore the complete Book of Ezekieli and the Holy Bible online.

Choose a Chapter

Ezekieli 46

Sura 46

1. Bwana MUNGU asema hivi; Lango la ua wa ndani, lielekealo upande wa mashariki litafungwa siku sita za kazi; lakini siku ya sabato litafunguliwa, na siku ya mwezi mpya litafunguliwa.

2. Naye mkuu ataingia kwa njia ya ukumbi wa lango lile, upande wa nje, naye atasimama karibu na mwimo wa lango, nao makuhani wataitengeneza sadaka yake ya kuteketezwa, na sadaka zake za amani, naye ataabudu penye kizingiti cha lango; kisha atatoka; lakini lango lile halitafungwa hata wakati wa jioni.

3. Watu wa nchi nao wataabudu mbele ya mlango wa lile lango mbele za Bwana, siku za sabato, na siku za mwezi mpya.

4. Nayo sadaka ya kuteketezwa, ambayo mkuu atamtolea Bwana siku ya sabato, itakuwa wana-kondoo sita wakamilifu, na kondoo mume mkamilifu.

5. Na sadaka ya unga itakuwa efa moja kwa kondoo mume, na sadaka ya unga kwa wale wana-kondoo, kiasi awezacho kutoa, na hini moja ya mafuta kwa efa moja.

6. Na siku ya mwezi mpya itakuwa ni ng'ombe mume mchanga mkamilifu; na wana-kondoo sita, na kondoo mume; nao watakuwa wakamilifu.

7. Naye atatengeneza sadaka ya unga, efa moja kwa ng'ombe mume, na efa moja kwa kondoo mume, na kwa wale wana-kondoo, kwa kiasi awezacho kutoa, na hini moja ya mafuta kwa efa moja.

8. Naye mkuu atakapoingia, ataingia kwa njia ya ukumbi wa lango lile, naye atatoka kwa njia iyo hiyo.

9. Lakini watu wa nchi watakapokuja mbele za Bwana katika sikukuu zilizoamriwa, yeye aingiaye kwa njia ya lango la upande wa kaskazini ili kuabudu, atatoka kwa njia ya lango la upande wa kusini; na yeye aingiaye kwa njia ya lango la upande wa kusini, atatoka kwa njia ya lango la upande wa kaskazini; hatarudi kwa njia ya lango aliloingia kwalo, lakini atatoka kwa kwenda mbele moja kwa moja.

10. Naye mkuu atakapoingia, ataingia katikati yao, nao, watakapotoka, watatoka wote pamoja.

11. Na katika sikukuu hizo, na sikukuu nyingine zilizoamriwa, sadaka ya unga itakuwa efa moja kwa ng'ombe mmoja, na efa moja kwa kondoo mume mmoja, na kwa wale wana-kondoo kiasi awezacho kutoa, na hini moja ya mafuta kwa efa moja.

12. Naye mkuu atakapotengeneza sadaka atoayo kwa hiari yake mwenyewe, sadaka ya kuteketezwa, au sadaka za amani, ziwe sadaka amtoleazo Bwana kwa hiari yake mwenyewe, mtu mmoja atamfungulia lango lile lielekealo upande wa mashariki, naye ataitengeneza sadaka yake ya kuteketezwa, na sadaka zake za amani, kama afanyavyo siku ya sabato; kisha atatoka; na baada ya kutoka kwake mtu mmoja atalifunga lango.

13. Nawe utatengeneza mwana-kondoo wa mwaka wa kwanza, mkamilifu, kuwa sadaka ya kuteketezwa kwa Bwana kila siku; kila siku asubuhi utamtengeneza.

14. Nawe utatengeneza sadaka ya unga pamoja nayo kila siku asubuhi, sehemu ya sita ya efa moja, na sehemu ya tatu ya hini moja ya mafuta; kuchanganya na unga ule mzuri; sadaka ya unga kwa Bwana daima, kwa amri ya milele.

15. Hivyo ndivyo watakavyomtengeneza mwana-kondoo, na sadaka ya unga, na mafuta, kila siku asubuhi, kuwa sadaka ya kuteketezwa ya daima.

16. Bwana MUNGU asema hivi; Mkuu akimpa mwanawe awaye yote zawadi, ni urithi wake, itakuwa mali ya wanawe; ni milki yao kwa kurithiwa.

17. Bali akimpa mmoja wa watumishi wake baadhi ya urithi wake, itakuwa mali yake mpaka mwaka wa kuacha huru; ndipo itakapomrudia mkuu; lakini urithi wake, huo utakuwa wa wanawe.

18. Tena mkuu hatawaondolea watu urithi wao, hata kuwatoa kwa nguvu katika milki yao; atawapa wanawe urithi katika mali yake mwenyewe, watu wangu wasije wakatawanyika, kila mtu mbali na milki yake.

19. Ndipo akanileta kati ya maingilio, yaliyokuwa kando ya lango, mpaka vyumba vitakatifu vya makuhani, vilivyoelekea upande wa kaskazini; na tazama, palikuwa na mahali, upande wa nyuma ulioelekea magharibi.

20. Akaniambia, Hapa ndipo mahali pa makuhani, watakapoitokosa sadaka ya hatia, na sadaka ya dhambi, watakapoioka sadaka ya unga; kusudi wasizilete nje katika ua wa nje, na kuwatakasa watu.

21. Kisha akanileta mpaka ua wa nje, akanipitisha karibu na pembe nne za ua huo; na tazama, katika kila pembe ya ua huo palikuwa na kiwanja.

22. Katika pembe nne za ua huo palikuwa na viwanja vilivyoungana, urefu wake dhiraa arobaini, na upana wake thelathini; viwanja hivyo vinne vya pembeni vilikuwa vya kipimo kimoja.

23. Tena palikuwa na safu ndani yake pande zote, kuvizunguka vile viwanja vinne; tena palifanywa meko ya kutokosea, chini ya safu pande zote.

24. Ndipo akaniambia, Hizi ni nyumba za kutokosea, ambamo wahudumu wa nyumba watatokosa sadaka za watu.

About Ezekieli Chapter 46

Read Ezekieli Chapter 46 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of Ezekieli in the Old Testament. Continue reading with the chapter navigation above or explore the complete book.

Book Information

Book: Ezekieli
Chapter: 46
Testament: Old Testament

How to Read this Chapter

Use the Previous and Next Chapter buttons to continue reading Ezekieli. You can also adjust the font size for comfortable reading and browse other books of the Bible using the navigation links.

https://www.youtube.com/watch?v=rzsT_Q3KLzE

More Resources

Continue Reading the Bible

Continue reading Ezekieli Chapter 46 and explore every book, chapter and verse of the Holy Bible. Use the navigation links above and below to move through the Scriptures with ease.

Frequently Asked Questions

What is Ezekieli Chapter 46?

Ezekieli Chapter 46 is part of the Book of Ezekieli in the Holy Bible.

Can I read this chapter online?

Yes. You can read the complete Ezekieli Chapter 46 online for free with easy chapter navigation.

More Chapters from Agano la Kale

  1. Zaburi Chapter 1
  2. Habakuki Chapter 3
  3. Ayubu Chapter 1
  4. Zaburi Chapter 2
  5. 1 Samweli Chapter 1
  6. Kutoka Chapter 11
  7. Kutoka Chapter 2

Explore More from Ezekieli

  1. Ezekieli Chapter 27
  2. Ezekieli Chapter 37
  3. Ezekieli Chapter 48
  4. Ezekieli Chapter 40
  5. Ezekieli Chapter 44
  6. Ezekieli Chapter 16
  7. Ezekieli Chapter 30

Related Chapters & Readings

  1. Hesabu Chapter 24
  2. Ezekieli Chapter 37
  3. 2 Wafalme Chapter 4
  4. Habakuki Chapter 3
  5. Hesabu Chapter 29
  6. Kumbukumbu la Torati Chapter 29
  7. Ayubu Chapter 16
Share Your Love

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *