Read 2 Mambo ya Nyakati Chapter 1 Online
Read 2 Mambo ya Nyakati Chapter 1 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of 2 Mambo ya Nyakati in the Old Testament. Browse every verse with easy chapter navigation, continue to the next chapter, or explore the complete Book of 2 Mambo ya Nyakati and the Holy Bible online.
Choose a Chapter
2 Mambo ya Nyakati 1
Sura 1
1. Basi Sulemani, mwana wa Daudi, alithibitishwa katika ufalme wake, naye Bwana, Mungu wake, alikuwa pamoja naye, akamtukuza mno.
2. Sulemani akasema na Israeli wote, na maakida wa maelfu, na wa mamia, na waamuzi, na kila shehe wa Israeli wote, wakuu wa nyumba za mababa.
3. Basi Sulemani akaenda mahali pa juu pa Gibeoni, na kusanyiko lote naye; kwani ndipo ilipokuwako hema ya kukutania ya Mungu, aliyoifanya Musa mtumishi wa Bwana jangwani.
4. Lakini sanduku la Mungu, Daudi alikuwa amelipandisha kutoka Kiriath-yearimu mpaka mahali Daudi alipolitengenezea; maana amelitandia hema katika Yerusalemu.
5. Tena madhabahu ya shaba, aliyoifanyiza Bezaleli mwana wa Uri, mwana wa Huri, ilikuwako huko mbele ya maskani ya Bwana; Sulemani na kusanyiko wakaiendea.
6. Sulemani akaipandia huko madhabahu ya shaba mbele za Bwana, iliyokuwako hemani pa kukutania, akatoa sadaka elfu za kuteketezwa juu yake.
7. Usiku ule Mungu akamtokea Sulemani, akamwambia, Omba utakalo nikupe.
8. Sulemani akamwambia Mungu, Umemfanyia baba yangu Daudi fadhili kuu, nawe umenimilikisha mimi badala yake.
9. Basi sasa, Ee Bwana Mungu, na limyakinie baba yangu Daudi neno lako; maana umenitawaza niwe mfalme juu ya watu wengi kama mavumbi ya nchi.
10. Basi sasa nipe hekima na maarifa, nijue kutoka na kuingia mbele ya watu hawa; kwa kuwa ni nani awezaye kuwahukumu watu wako hawa walio wengi?
11. Naye Mungu akamwambia Sulemani, Kwa sababu neno hili lilikuwamo moyoni mwako, wala hukujitakia mali, wala utajiri, wala utukufu, wala maisha za wakuchukiao, wala hukujitakia maisha ya siku nyingi; bali umejitakia hekima na maarifa, upate kuwahukumu watu wangu, niliokutawaza juu yao;
12. basi hekima na maarifa umepewa; nami nitakupa mali, na utajiri, na utukufu, kupita walivyokuwa navyo wafalme wote waliokuwa kabla yako, wala baada yako hapatakuwa na mtu atakayekuwa navyo.
13. Akaja Sulemani kutoka mahali pa juu pa Gibeoni, toka mbele ya hema ya kukutania, mpaka Yerusalemu; akatawala juu ya Israeli.
14. Sulemani akakusanya magari na wapandao farasi; naye alikuwa na magari elfu na mia nne, na wapandao farasi kumi na mbili elfu, aliowaweka katika miji ya magari, na pamoja na mfalme huko Yerusalemu.
15. Mfalme akafanya fedha na dhahabu kuwa kama mawe humo Yerusalemu, na mierezi akaifanya kuwa kama mikuyu iliyomo Shefela, kwa kuwa mingi.
16. Nao farasi, aliokuwa nao Sulemani wakaletwa toka Misri; wakapewa wafanya biashara wake mfalme kwa makundi; kila kundi na thamani yake.
17. Nao hupandisha, na kuleta kutoka Misri gari kwa shekeli mia sita za fedha, na farasi kwa mia na hamsini, vivyo watu wakawaletea wafalme wote wa Wahiti, na wafalme wa Shamu, mikononi mwao.
About 2 Mambo ya Nyakati Chapter 1
Read 2 Mambo ya Nyakati Chapter 1 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of 2 Mambo ya Nyakati in the Old Testament. Continue reading with the chapter navigation above or explore the complete book.
Book Information
Book: 2 Mambo ya Nyakati
Chapter: 1
Testament: Old Testament
How to Read this Chapter
Use the Previous and Next Chapter buttons to continue reading 2 Mambo ya Nyakati. You can also adjust the font size for comfortable reading and browse other books of the Bible using the navigation links.
More Resources
Continue Reading the Bible
Continue reading 2 Mambo ya Nyakati Chapter 1 and explore every book, chapter and verse of the Holy Bible. Use the navigation links above and below to move through the Scriptures with ease.
Frequently Asked Questions
What is 2 Mambo ya Nyakati Chapter 1?
2 Mambo ya Nyakati Chapter 1 is part of the Book of 2 Mambo ya Nyakati in the Holy Bible.
Can I read this chapter online?
Yes. You can read the complete 2 Mambo ya Nyakati Chapter 1 online for free with easy chapter navigation.
More Chapters from 2 MambO Ya Nyakati
- 2 Mambo ya Nyakati Chapter 14
- 2 Mambo ya Nyakati Chapter 21
- 2 Mambo ya Nyakati Chapter 17
- 2 Mambo ya Nyakati Chapter 13
- 2 Mambo ya Nyakati Chapter 5
- 2 Mambo ya Nyakati Chapter 22
- 2 Mambo ya Nyakati Chapter 4
Explore More from Agano la Kale
- Isaya Chapter 22
- Hesabu Chapter 16
- 1 Wafalme Chapter 9
- Nehemia Chapter 10
- Mwanzo Chapter 4
- Yeremia Chapter 24
- Mithali Chapter 3