1 Petro Chapter 5

For English

Read 1 Petro Chapter 5 Online

Read 1 Petro Chapter 5 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of 1 Petro in the New Testament. Browse every verse with easy chapter navigation, continue to the next chapter, or explore the complete Book of 1 Petro and the Holy Bible online.

Choose a Chapter

1 Petro 5

Sura 5

1. Nawasihi wazee walio kwenu, mimi niliye mzee, mwenzi wao, na shahidi wa mateso ya Kristo, na mshirika wa utukufu utakaofunuliwa baadaye;

2. lichungeni kundi la Mungu lililo kwenu, na kulisimamia, si kwa kulazimishwa, bali kwa hiari kama Mungu atakavyo; si kwa kutaka fedha ya aibu, bali kwa moyo.

3. Wala si kama wajifanyao mabwana juu ya mitaa yao, bali kwa kujifanya vielelezo kwa lile kundi.

4. Na Mchungaji mkuu atakapodhihirishwa, mtaipokea taji ya utukufu, ile isiyokauka.

5. Vivyo hivyo ninyi vijana, watiini wazee. Naam, ninyi nyote jifungeni unyenyekevu, mpate kuhudumiana; kwa sababu Mungu huwapinga wenye kiburi, lakini huwapa wanyenyekevu neema.

6. Basi nyenyekeeni chini ya mkono wa Mungu ulio hodari, ili awakweze kwa wakati wake;

7. huku mkimtwika yeye fadhaa zenu zote, kwa maana yeye hujishughulisha sana kwa mambo yenu.

8. Mwe na kiasi na kukesha; kwa kuwa mshitaki wenu Ibilisi, kama simba angurumaye, huzunguka-zunguka, akitafuta mtu ammeze.

9. Nanyi mpingeni huyo, mkiwa thabiti katika imani, mkijua ya kuwa mateso yale yale yanatimizwa kwa ndugu zenu walioko duniani.

10. Na Mungu wa neema yote, aliyewaita kuingia katika utukufu wake wa milele katika Kristo, mkiisha kuteswa kwa muda kidogo, yeye mwenyewe atawatengeneza, na kuwathibitisha, na kuwatia nguvu.

11. Uweza una yeye hata milele na milele. Amina.

12. Kwa mkono wa Silwano, ndugu mwaminifu kama nionavyo, nimewaandikia kwa maneno machache, kuonya na kushuhudia ya kuwa hii ndiyo neema ya kweli ya Mungu. Simameni imara katika hiyo.

13. Mwenzenu mteule hapa Babeli awasalimu, na Marko mwanangu.

14. Salimianeni kwa busu la upendo. Amani na iwe kwenu nyote, mlio katika Kristo. Amina.

About 1 Petro Chapter 5

Read 1 Petro Chapter 5 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of 1 Petro in the New Testament. Continue reading with the chapter navigation above or explore the complete book.

Book Information

Book: 1 Petro
Chapter: 5
Testament: New Testament

How to Read this Chapter

Use the Previous and Next Chapter buttons to continue reading 1 Petro. You can also adjust the font size for comfortable reading and browse other books of the Bible using the navigation links.

https://www.youtube.com/watch?v=rzsT_Q3KLzE

More Resources

Continue Reading the Bible

Continue reading 1 Petro Chapter 5 and explore every book, chapter and verse of the Holy Bible. Use the navigation links above and below to move through the Scriptures with ease.

Frequently Asked Questions

What is 1 Petro Chapter 5?

1 Petro Chapter 5 is part of the Book of 1 Petro in the Holy Bible.

Can I read this chapter online?

Yes. You can read the complete 1 Petro Chapter 5 online for free with easy chapter navigation.

More Chapters from 1-petro

  1. 1 Petro Chapter 2
  2. 1 Petro Chapter 1
  3. 1 Petro Chapter 3
  4. 1 Petro Chapter 4

Explore More from Agano Jipya

  1. Waebrania Chapter 8
  2. Marko Chapter 16
  3. Wagalatia Chapter 6
  4. Yohana Chapter 10
  5. Luka Chapter 19
  6. 1 Wakorintho Chapter 8
  7. 1 Wakorintho Chapter 4

Related Chapters & Readings

  1. Isaya Chapter 61
  2. Mathayo Chapter 23
  3. Yeremia Chapter 18
  4. Yeremia Chapter 24
  5. Mhubiri Chapter 10
  6. Zaburi Chapter 91
  7. Zekaria Chapter 12
Share Your Love

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *