Yohana Chapter 2

For English

Read Yohana Chapter 2 Online

Read Yohana Chapter 2 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of Yohana in the New Testament. Browse every verse with easy chapter navigation, continue to the next chapter, or explore the complete Book of Yohana and the Holy Bible online.

Choose a Chapter

Yohana 2

Sura 2

1. Na siku ya tatu palikuwa na arusi huko Kana, mji wa Galilaya; naye mama yake Yesu alikuwapo.

2. Yesu naye alikuwa amealikwa arusini pamoja na wanafunzi wake.

3. Hata divai ilipowatindikia, mamaye Yesu akamwambia, Hawana divai.

4. Yesu akamwambia, Mama, tuna nini mimi nawe? Saa yangu haijawadia.

5. Mamaye akawaambia watumishi, Lo lote atakalowaambia, fanyeni.

6. Basi kulikuwako huko mabalasi sita ya mawe, nayo yamewekwa huko kwa desturi ya Wayahudi ya kutawadha, kila moja lapata kadiri ya nzio mbili tatu.

7. Yesu akawaambia, Jalizeni mabalasi maji. Nao wakayajaliza hata juu.

8. Akawaambia, Sasa tekeni, mkampelekee mkuu wa meza. Wakapeleka.

9. Naye mkuu wa meza alipoyaonja yale maji yaliyopata kuwa divai, (wala asijue ilikotoka, lakini watumishi walijua, wale walioyateka yale maji), yule mkuu wa meza alimwita bwana arusi,

10. akamwambia, Kila mtu kwanza huandaa divai iliyo njema; hata watu wakiisha kunywa sana ndipo huleta iliyo dhaifu; wewe umeiweka divai iliyo njema hata sasa.

11. Mwanzo huo wa ishara Yesu aliufanya huko Kana ya Galilaya, akaudhihirisha utukufu wake, nao wanafunzi wake wakamwamini.

12. Baada ya hayo akashuka mpaka Kapernaumu, yeye na mama yake na ndugu zake na wanafunzi wake; wakakaa huko siku si nyingi.

13. Na Pasaka ya Wayahudi ilikuwa karibu; naye Yesu akakwea mpaka Yerusalemu.

14. Akaona pale hekaluni watu waliokuwa wakiuza ng'ombe na kondoo na njiwa, na wenye kuvunja fedha wameketi.

15. Akafanya kikoto cha kambaa, akawatoa wote katika hekalu, na kondoo na ng'ombe; akamwaga fedha za wenye kuvunja fedha, akazipindua meza zao;

16. akawaambia wale waliokuwa wakiuza njiwa, Yaondoeni haya; msiifanye nyumba ya Baba yangu kuwa nyumba ya biashara.

17. Wanafunzi wake wakakumbuka ya kuwa imeandikwa, Wivu wa nyumba yako utanila.

18. Basi Wayahudi wakajibu, wakamwambia, Ni ishara gani utuonyeshayo, kwamba unafanya haya?

19. Yesu akajibu, akawaambia, Livunjeni hekalu hili, nami katika siku tatu nitalisimamisha.

20. Basi Wayahudi wakasema, Hekalu hili lilijengwa katika muda wa miaka arobaini na sita, nawe utalisimamisha katika siku tatu?

21. Lakini yeye alinena habari za hekalu la mwili wake.

22. Basi alipofufuka katika wafu, wanafunzi wake wakakumbuka ya kuwa alisema hivi, wakaliamini lile andiko na lile neno alilolinena Yesu.

23. Hata alipokuwapo Yerusalemu kwenye sikukuu wakati wa Pasaka, watu wengi waliamini jina lake, walipoziona ishara zake alizozifanya.

24. Lakini Yesu hakujiaminisha kwao; kwa kuwa yeye aliwajua wote;

25. na kwa sababu hakuwa na haja ya mtu kushuhudia habari za mwanadamu; kwa maana yeye mwenyewe alijua yaliyomo ndani ya mwanadamu.

About Yohana Chapter 2

Read Yohana Chapter 2 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of Yohana in the New Testament. Continue reading with the chapter navigation above or explore the complete book.

Book Information

Book: Yohana
Chapter: 2
Testament: New Testament

How to Read this Chapter

Use the Previous and Next Chapter buttons to continue reading Yohana. You can also adjust the font size for comfortable reading and browse other books of the Bible using the navigation links.

https://www.youtube.com/watch?v=rzsT_Q3KLzE

More Resources

Continue Reading the Bible

Continue reading Yohana Chapter 2 and explore every book, chapter and verse of the Holy Bible. Use the navigation links above and below to move through the Scriptures with ease.

Frequently Asked Questions

What is Yohana Chapter 2?

Yohana Chapter 2 is part of the Book of Yohana in the Holy Bible.

Can I read this chapter online?

Yes. You can read the complete Yohana Chapter 2 online for free with easy chapter navigation.

More Chapters from Agano Jipya

  1. Waebrania Chapter 5
  2. Waebrania Chapter 1
  3. Waebrania Chapter 6
  4. Waebrania Chapter 4
  5. Ufunuo wa Yohana Chapter 1
  6. Waebrania Chapter 11
  7. Waebrania Chapter 10

Explore More from yohana

  1. Yohana Chapter 12
  2. Yohana Chapter 13
  3. Yohana Chapter 14
  4. Yohana Chapter 17
  5. Yohana Chapter 4
  6. Yohana Chapter 18
  7. Yohana Chapter 8

Related Chapters & Readings

  1. Mathayo Chapter 18
  2. Danieli Chapter 7
  3. 1 Samweli Chapter 11
  4. Mwanzo Chapter 39
  5. Luka Chapter 17
  6. 1 Wafalme Chapter 5
  7. Hesabu Chapter 21
Share Your Love

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *