Kumbukumbu la Torati Chapter 25

For English

Read Kumbukumbu la Torati Chapter 25 Online

Read Kumbukumbu la Torati Chapter 25 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of Kumbukumbu la Torati in the Old Testament. Browse every verse with easy chapter navigation, continue to the next chapter, or explore the complete Book of Kumbukumbu la Torati and the Holy Bible online.

Choose a Chapter

Kumbukumbu la Torati 25

Sura 25

1. Pakiwa na mashindano kati ya watu, wakaenda maamuzini, na hao waamuzi wakawaamua; na wampe haki mwenye haki, na wamhukumie makosa yule mwovu;

2. na iwe, ikimpasa kupigwa yule mwovu, alazwe chini na mwamuzi, na kupigwa mbele ya uso wake, kwa kadiri ya uovu wake, kwa kuhesabu.

3. Aweza kumpiga fimbo arobaini asizidishe asije akaonekana nduguyo kuwa amedharauliwa kwako, azidishapo kwa kumpiga fimbo nyingi juu ya hizi.

4. Ng'ombe apurapo nafaka usimfunge kinywa.

5. Watakapoketi pamoja mtu na nduguye, mmojawapo akafa, wala hana mwana wa kiume, mke wa yule aliyekufa asiolewe nje na mgeni; nduguye yule mumewe amwingilie amweke kwake awe mkewe, kumfanyia yampasayo nduguye mumewe.

6. Na iwe, yule mzaliwa wa kwanza atakayemzaa, amfuate nduguye aliyekufa kwa jina lake, lisije likafutwa jina lake katika Israeli.

7. Na yule mtu kwamba hapendi kumtwaa mke wa nduguye, aende huyo mke wa nduguye langoni kwa wazee, akawaambie, Nduguye mume wangu yuakataa kumsimamishia nduguye jina katika Israeli, hataki kunitimizia yampasayo nduguye mume wangu.

8. Ndipo wamwite wazee wa mji wake waseme naye; naye akisimama na kusema, Sitaki mimi kumtwaa mwanamke huyu,

9. ndipo mke wa nduguye amkaribie mbele ya hao wazee, amvue kiatu chake mguuni mwake, na kumtemea mate ya uso; kisha atajibu yule mwanamke, aseme, Mume akataaye kumjengea nduguye nyumba yake na afanywe hivi.

10. Na jina lake katika Israeli liitwe, Nyumba ya mvuliwa kiatu.

11. Washindanapo waume wao kwa wao, akakaribia mke wa mmojawapo, ili kumwokoa mumewe katika mkono wa ampigaye, yule mke akatoa mkono wake, na kumkamata tupu yake;

12. umkate ule mkono wake, lisiwe na huruma jicho lako.

13. Usiwe na mawe ya kupimia mbalimbali, kubwa na dogo, katika mfuko wako.

14. Usiwe na vipimo mbalimbali, kikubwa na kidogo, katika nyumba yako.

15. Uwe na jiwe timilifu la haki, uwe na kipimo kitimilifu cha haki; zipate kuwa nyingi siku zako, katika nchi akupayo Bwana, Mungu wako.

16. Kwa kuwa wote wayatendao mambo kama haya, wote watendao yasiyo haki, ni machukizo kwa Bwana, Mungu wako.

17. Kumbuka aliyokufanya Amaleki katika njia mlipokuwa mkitoka Misri;

18. jinsi alivyokukuta katika njia, akapiga katika watu wako walioachwa nyuma, wote waliokuwa wanyonge nyuma yako, ulipokuwa umechoka na kuzimia; wala asimche Mungu.

19. Basi itakuwa, hapo atakapokwisha kukupumzisha Bwana, Mungu wako, katika adui zako wote walio kando-kando, katika nchi akupayo Bwana, Mungu wako, iwe urithi uimiliki, ndipo uufute ukumbuko wa Amaleki chini ya mbingu; usisahau.

About Kumbukumbu la Torati Chapter 25

Read Kumbukumbu la Torati Chapter 25 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of Kumbukumbu la Torati in the Old Testament. Continue reading with the chapter navigation above or explore the complete book.

Book Information

Book: Kumbukumbu la Torati
Chapter: 25
Testament: Old Testament

How to Read this Chapter

Use the Previous and Next Chapter buttons to continue reading Kumbukumbu la Torati. You can also adjust the font size for comfortable reading and browse other books of the Bible using the navigation links.

https://www.youtube.com/watch?v=rzsT_Q3KLzE

More Resources

Continue Reading the Bible

Continue reading Kumbukumbu la Torati Chapter 25 and explore every book, chapter and verse of the Holy Bible. Use the navigation links above and below to move through the Scriptures with ease.

Frequently Asked Questions

What is Kumbukumbu la Torati Chapter 25?

Kumbukumbu la Torati Chapter 25 is part of the Book of Kumbukumbu la Torati in the Holy Bible.

Can I read this chapter online?

Yes. You can read the complete Kumbukumbu la Torati Chapter 25 online for free with easy chapter navigation.

More Chapters from Agano la Kale

  1. Zaburi Chapter 1
  2. Habakuki Chapter 3
  3. Ayubu Chapter 1
  4. Zaburi Chapter 2
  5. 1 Samweli Chapter 1
  6. Kutoka Chapter 11
  7. Kutoka Chapter 2

Explore More from Kumbukumbu La Torati

  1. Kumbukumbu la Torati Chapter 23
  2. Kumbukumbu la Torati Chapter 4
  3. Kumbukumbu la Torati Chapter 14
  4. Kumbukumbu la Torati Chapter 6
  5. Kumbukumbu la Torati Chapter 1
  6. Kumbukumbu la Torati Chapter 7
  7. Kumbukumbu la Torati Chapter 32

Related Chapters & Readings

  1. 1 Mambo ya Nyakati Chapter 11
  2. Luka Chapter 3
  3. Mathayo Chapter 4
  4. Zaburi Chapter 25
  5. Tito Chapter 2
  6. Mhubiri Chapter 12
  7. Marko Chapter 3
Share Your Love

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *