Kutoka Chapter 24

For English

Read Kutoka Chapter 24 Online

Read Kutoka Chapter 24 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of Kutoka in the Old Testament. Browse every verse with easy chapter navigation, continue to the next chapter, or explore the complete Book of Kutoka and the Holy Bible online.

Choose a Chapter

Kutoka 24

Sura 24

1. Kisha Bwana akamwambia Musa, Kweeni wewe, na Haruni, na Nadabu, na Abihu, na watu sabini wa wazee wa Israeli, mkamfikilie Bwana; mkasujudie kwa mbali;

2. na Musa peke yake ndiye atakayekaribia karibu na Bwana; lakini hao hawatakaribia karibu; wala hao watu hawatakwea pamoja naye.

3. Musa akaenda akawaambia watu maneno yote ya Bwana, na hukumu zake zote; watu wote wakajibu kwa sauti moja, wakasema, Maneno yote aliyoyanena Bwana tutayatenda.

4. Basi Musa akayaandika maneno yote ya Bwana, akaondoka asubuhi na mapema, akajenga madhabahu chini ya mlima, na nguzo kumi na mbili, kwa hesabu ya kabila kumi na mbili za Israeli,

5. akapeleka vijana wa wana wa Israeli, waliotoa sadaka za kuteketezwa, wakamchinjia Bwana sadaka za amani za ng'ombe.

6. Musa akatwaa nusu ya ile damu, akaitia katika mabakuli; na nusu ya ile damu akainyunyiza juu ya madhabahu.

7. Kisha akakitwaa kitabu cha agano akakisoma masikioni mwa watu; wakasema, Hayo yote aliyoyanena Bwana tutayatenda, nasi tutatii.

8. Musa akaitwaa ile damu, akawanyunyizia watu, akasema, Hii ndiyo damu ya agano alilolifanya Bwana pamoja nanyi katika maneno haya yote.

9. Ndipo akakwea juu, Musa, na haruni, na Nadabu, na Abihu, na watu sabini miongoni mwa wazee wa Israeli;

10. wakamwona Mungu wa Israeli; chini ya miguu yake palikuwa na kama sakafu iliyofanyizwa kwa yakuti samawi, kama zile mbingu zenyewe kwa usafi wake.

11. Naye hakuweka mkono wake juu ya hao wakuu wa wana wa Israeli; nao wakamwona Mungu, wakala na kunywa.

12. Bwana akamwambia Musa, Njoo huku juu kwangu mlimani, uwe huku; nami nitakupa mbao za mawe na ile sheria na hiyo amri niliyoiandika ili uwafundishe.

13. Musa akaondoka na Yoshua, mtumishi wake, Musa akapanda mlimani kwa Mungu.

14. Akawaambia hao wazee, Tungojeeni hapa, mpaka tutakaporudi kwenu; na tazameni, Haruni na Huri wapo pamoja nanyi; kila mtu aliye na neno na awaendee.

15. Musa akapanda mlimani, lile wingu likaufunikiza mlima.

16. Na huo utukufu wa Bwana ukakaa juu ya mlima wa Sinai; lile wingu likaufunikiza siku sita; na siku ya saba akamwita Musa toka kati ya lile wingu.

17. Na kuonekana kwake ule utukufu wa Bwana kulikuwa kama moto uteketezao, juu ya mlima machoni pa wana wa Israeli.

18. Musa akaingia ndani ya lile wingu, akapanda mlimani; Musa akawa humo katika ule mlima siku arobaini, mchana na usiku.

About Kutoka Chapter 24

Read Kutoka Chapter 24 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of Kutoka in the Old Testament. Continue reading with the chapter navigation above or explore the complete book.

Book Information

Book: Kutoka
Chapter: 24
Testament: Old Testament

How to Read this Chapter

Use the Previous and Next Chapter buttons to continue reading Kutoka. You can also adjust the font size for comfortable reading and browse other books of the Bible using the navigation links.

https://www.youtube.com/watch?v=rzsT_Q3KLzE

More Resources

Continue Reading the Bible

Continue reading Kutoka Chapter 24 and explore every book, chapter and verse of the Holy Bible. Use the navigation links above and below to move through the Scriptures with ease.

Frequently Asked Questions

What is Kutoka Chapter 24?

Kutoka Chapter 24 is part of the Book of Kutoka in the Holy Bible.

Can I read this chapter online?

Yes. You can read the complete Kutoka Chapter 24 online for free with easy chapter navigation.

More Chapters from Agano la Kale

  1. Isaya Chapter 1
  2. Isaya Chapter 2
  3. Isaya Chapter 6
  4. Isaya Chapter 3
  5. Isaya Chapter 7
  6. Isaya Chapter 14
  7. Isaya Chapter 5

Explore More from Kutoka

  1. Kutoka Chapter 23
  2. Kutoka Chapter 40
  3. Kutoka Chapter 35
  4. Kutoka Chapter 3
  5. Kutoka Chapter 13
  6. Kutoka Chapter 36
  7. Kutoka Chapter 21

Related Chapters & Readings

  1. 1 Wakorintho Chapter 3
  2. 2 Wafalme Chapter 3
  3. Yoshua Chapter 5
  4. Marko Chapter 10
  5. Mathayo Chapter 10
  6. 2 Mambo ya Nyakati Chapter 7
  7. Hosea Chapter 5
Share Your Love

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *