Read Yoshua Chapter 12 Online
Read Yoshua Chapter 12 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of Yoshua in the Old Testament. Browse every verse with easy chapter navigation, continue to the next chapter, or explore the complete Book of Yoshua and the Holy Bible online.
Choose a Chapter
Yoshua 12
Sura 12
1. Basi hawa ndio wafalme wa nchi, ambao wana wa Israeli waliwapiga na kuimiliki nchi yao ng'ambo ya pili ya Yordani, upande wa maawio ya jua, kutoka bonde la Amoni mpaka mlima wa Hermoni, na nchi yote ya Araba upande wa mashariki;
2. Sihoni mfalme wa Waamori, aliyekaa huko Heshboni, naye ndiye aliyetawala toka Aroeri, ulioko kando ya bonde la Arnoni, na toka huo mji ulio katikati ya bonde, na nusu ya Gileadi, hata kuufikilia mto wa Yaboki, mpaka wa hao wana wa Amoni;
3. na nchi ya Araba mpaka bahari ya Kinerethi, kuelekea mashariki, tena mpaka bahari ya Ataba, mpaka Bahari ya Chumvi, kwendea mashariki, njia ya kwendea Beth-yeshimothi; tena upande wa kusini, chini ya matelemko ya Pisga;
4. tena mpaka wa Ogu mfalme wa Bashani, aliyekuwa wa hayo mabaki ya hao Warefai, aliyekaa Ashtarothi na Edrei,
5. naye alitawala katika mlima wa Hermoni, na katika Saleka, na katika Bashani yote, hata mpaka wa Wageshuri, na Wamaaka, na nusu ya Gileadi, mpaka wa huyo Sihoni mfalme wa Heshboni.
6. Musa mtumishi wa Bwana na wana wa Israeli wakawapiga; naye Musa mtumishi wa Bwana akawapa Wareubeni, na Wagadi, na nusu ya kabila ya Manase iwe urithi wao.
7. Hawa ni wafalme wa hiyo nchi ambao Yoshua na wana wa Israeli waliwapiga ng'ambo ya pili ya Yordani upande wa magharibi, kutoka Baal-gadi katika bonde la Lebanoni mpaka kilima cha Halaki, kilichoelekea Seiri; Yoshua naye akawapa kabila za Israeli iwe milki yao sawasawa na magawanyo yao;
8. katika nchi ya vilima, na katika Shefela, na katika nchi ya Araba, na katika matelemko, na katika bara, na katika Negebu; nchi ya Mhiti, na Mwamori, na Mkanaani, na Mperizi, na Mhivi, na Myebusi;
9. mfalme wa Yeriko, mmoja; mfalme wa Ai, ulio karibu na Betheli, mmoja;
10. mfalme wa Yerusalemu, mmoja; mfalme wa Hebroni, mmoja;
11. mfalme wa Yarmuthi, mmoja; na mfalme wa Lakishi, mmoja;
12. mfalme wa Egloni, mmoja; na mfalme wa Gezeri, mmoja;
13. mfalme wa Debiri, mmoja; na mfalme wa Gederi, mmoja;
14. mfalme wa Horma, mmoja; na mfalme wa Aradi, mmoja;
15. mfalme wa Libna, mmoja; na mfalme wa Adulamu, mmoja;
16. mfalme wa Makeda, mmoja; na mfalme wa Betheli, mmoja;
17. mfalme wa Tapua, mmoja; na mfalme wa Heferi, mmoja;
18. mfalme wa Afeka, mmoja; na mfalme wa Lasharoni, mmoja;
19. mfalme wa Madoni, mmoja; na mfalme wa Hazori, mmoja;
20. mfalme wa Shimron-meroni, mmoja; na mfalme wa Akshafu, mmoja;
21. mfalme wa Taanaki, mmoja; na mfalme wa Megido, mmoja;
22. na mfalme wa Kedeshi, mmoja; mfalme wa Yokneamu wa Karmeli, mmoja;
23. mfalme wa Dori katika kilima cha Dori, mmoja; na mfalme wa makabila katika Gilgali, mmoja;
24. na mfalme wa Tirsa, mmoja; wafalme hao wote walikuwa ni thelathini na mmoja.
About Yoshua Chapter 12
Read Yoshua Chapter 12 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of Yoshua in the Old Testament. Continue reading with the chapter navigation above or explore the complete book.
Book Information
Book: Yoshua
Chapter: 12
Testament: Old Testament
How to Read this Chapter
Use the Previous and Next Chapter buttons to continue reading Yoshua. You can also adjust the font size for comfortable reading and browse other books of the Bible using the navigation links.
More Resources
Continue Reading the Bible
Continue reading Yoshua Chapter 12 and explore every book, chapter and verse of the Holy Bible. Use the navigation links above and below to move through the Scriptures with ease.
Frequently Asked Questions
What is Yoshua Chapter 12?
Yoshua Chapter 12 is part of the Book of Yoshua in the Holy Bible.
Can I read this chapter online?
Yes. You can read the complete Yoshua Chapter 12 online for free with easy chapter navigation.
More Chapters from Agano la Kale
- Isaya Chapter 1
- Isaya Chapter 2
- Isaya Chapter 6
- Isaya Chapter 3
- Isaya Chapter 7
- Isaya Chapter 5
- Isaya Chapter 16
Explore More from yoshua
- Yoshua Chapter 7
- Yoshua Chapter 3
- Yoshua Chapter 23
- Yoshua Chapter 4
- Yoshua Chapter 5
- Yoshua Chapter 24
- Yoshua Chapter 11