Read Kumbukumbu la Torati Chapter 27 Online
Read Kumbukumbu la Torati Chapter 27 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of Kumbukumbu la Torati in the Old Testament. Browse every verse with easy chapter navigation, continue to the next chapter, or explore the complete Book of Kumbukumbu la Torati and the Holy Bible online.
Choose a Chapter
Kumbukumbu la Torati 27
Sura 27
1. Musa na wazee wa Israeli wakawaagiza wale watu wakawaambia, Shikeni maagizo yote niwaagizayo leo.
2. Na iwe, siku mtakayovuka Yordani kwenda nchi akupayo Bwana, Mungu wako, ujisimamishie mawe makubwa, ukayatalize matalizo,
3. uyaandike maneno yote ya torati hii juu yake, utakapokwisha kuvuka; ili upate kuingia nchi akupayo Bwana, Mungu wako, nchi imiminikayo maziwa na asali, kama alivyokuahidi Bwana, Mungu wa baba zako.
4. Na iwe, mtakapokwisha vuka Yordani myasimamishe mawe haya, niwaagizayo hivi leo, katika mlima Ebali, nawe yatalize matalizo.
5. Na huko umjengee madhabahu Bwana, Mungu wako, madhabahu ya mawe, usitumie chombo cha chuma juu yake.
6. Jenga hiyo madhabahu ya Bwana, Mungu wako, kwa mawe yasiyochongwa; ukamtolee Bwana, Mungu wako, sadaka za kuteketezwa juu yake;
7. ufanye na sadaka za amani, ukale huko; nawe furahi mbele za Bwana, Mungu wako.
8. Kisha, andika juu ya mawe hayo maneno ya torati hii yote, waziwazi sana.
9. Musa na makuhani Walawi wakawaambia Israeli wote wakasema, Nyamaza, usikize, Ee Israeli; leo umekuwa watu wa Bwana, Mungu wako.
10. Basi isikize sauti ya Bwana, Mungu wako, ufanye maagizo yake na amri zake nikuagizavyo leo.
11. Musa akawaagiza wale watu siku iyo hiyo, akasema,
12. Hawa na wasimame juu ya mlima wa Gerizimu kwa kuwabarikia watu, mkiisha vuka Yordani; Simeoni, na Lawi, na Yuda, na Isakari, na Yusufu, na Benyamini;
13. na hawa na wasimame juu ya mlima wa Ebali kwa laana; Reubeni, na Gadi, na Asheri, na Zabuloni, na Dani, na Naftali.
14. Kisha Walawi na wajibu, wawaambie watu wote wa Israeli kwa sauti kuu,
15. Na alaaniwe mtu afanyaye sanamu ya kuchonga, au ya kusubu, machukizo kwa Bwana, kazi ya mikono ya fundi, akaisimamisha kwa siri. Na watu wote wajibu, waseme, Amina.
16. Na alaaniwe amdharauye baba yake au mama yake. Na watu wote waseme, Amina.
17. Na alaaniwe aondoaye mpaka wa jirani yake. Na watu wote waseme, Amina.
18. Na alaaniwe ampotezaye kipofu akakosa njia. Na watu wote waseme, Amina.
19. Na alaaniwe apotoaye hukumu ya mgeni, na yatima, na mjane aliyefiliwa na mumewe. Na watu wote waseme, Amina.
20. Na alaaniwe alalaye na mke wa baba yake, kwa kuwa amefunua mavazi ya babaye. Na watu wote waseme, Amina.
21. Na alaaniwe alalaye na mnyama wa aina yo yote. Na watu wote waseme, Amina.
22. Na alaaniwe alalaye na umbu lake, binti ya babaye, au binti ya mamaye. Na watu wote waseme, Amina.
23. Na alaaniwe alalaye na mkwewe, mamaye mkewe. Na watu wote waseme, Amina.
24. Na alaaniwe ampigaye mwenzake kwa siri. Na watu wote waseme Amina.
25. Na alaaniwe atwaaye ujira wa kumwua asiye makosa. Na watu wote waseme, Amina.
26. Na alaaniwe asiyeyaweka imara maneno ya torati hii kwa kuyafanya. Na watu wote waseme, Amina.
About Kumbukumbu la Torati Chapter 27
Read Kumbukumbu la Torati Chapter 27 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of Kumbukumbu la Torati in the Old Testament. Continue reading with the chapter navigation above or explore the complete book.
Book Information
Book: Kumbukumbu la Torati
Chapter: 27
Testament: Old Testament
How to Read this Chapter
Use the Previous and Next Chapter buttons to continue reading Kumbukumbu la Torati. You can also adjust the font size for comfortable reading and browse other books of the Bible using the navigation links.
More Resources
Continue Reading the Bible
Continue reading Kumbukumbu la Torati Chapter 27 and explore every book, chapter and verse of the Holy Bible. Use the navigation links above and below to move through the Scriptures with ease.
Frequently Asked Questions
What is Kumbukumbu la Torati Chapter 27?
Kumbukumbu la Torati Chapter 27 is part of the Book of Kumbukumbu la Torati in the Holy Bible.
Can I read this chapter online?
Yes. You can read the complete Kumbukumbu la Torati Chapter 27 online for free with easy chapter navigation.
More Chapters from Agano la Kale
- Zaburi Chapter 1
- Habakuki Chapter 3
- Ayubu Chapter 1
- Zaburi Chapter 2
- 1 Samweli Chapter 1
- Kutoka Chapter 11
- Kutoka Chapter 2
Explore More from Kumbukumbu La Torati
- Kumbukumbu la Torati Chapter 16
- Kumbukumbu la Torati Chapter 15
- Kumbukumbu la Torati Chapter 22
- Kumbukumbu la Torati Chapter 14
- Kumbukumbu la Torati Chapter 32
- Kumbukumbu la Torati Chapter 30
- Kumbukumbu la Torati Chapter 5