Kumbukumbu la Torati Chapter 26

For English

Read Kumbukumbu la Torati Chapter 26 Online

Read Kumbukumbu la Torati Chapter 26 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of Kumbukumbu la Torati in the Old Testament. Browse every verse with easy chapter navigation, continue to the next chapter, or explore the complete Book of Kumbukumbu la Torati and the Holy Bible online.

Choose a Chapter

Kumbukumbu la Torati 26

Sura 26

1. Na itakuwa, ukiisha kuingia katika nchi akupayo Bwana, Mungu wako, iwe urithi, na kuimiliki, na kukaa ndani yake;

2. twaa malimbuko ya ardhi, utakayoyavuna katika nchi akupayo Bwana, Mungu wako; ukayatie katika kikapu, ukaende hata mahali pale atakapopachagua Bwana, Mungu wako, ili alikalishe jina lake huko.

3. Ukamwendee kuhani atakayekuwapo siku zile, ukamwambie, Ninakiri leo kwa Bwana, Mungu wako, ya kuwa nimeingia katika nchi Bwana aliyowaapia baba zetu ya kwamba atatupa.

4. Naye kuhani atakipokea kikapu mkononi mwako, akiweke chini mbele ya madhabahu ya Bwana, Mungu wako.

5. Nawe ujibu, ukaseme mbele za Bwana, Mungu wako, Baba yangu alikuwa Mwarami karibu na kupotea, akashuka Misri, akakaa huko ugenini, nao ni wachache hesabu yao; akawa taifa kubwa huko, yenye nguvu na watu wengi.

6. Wamisri wakatuonea, wakatutesa, wakatutumikisha utumwa mzito.

7. Tukamlilia Bwana, Mungu wa baba zetu; Bwana akasikia sauti yetu, akaona na taabu yetu, na kazi yetu, na kuonewa kwetu.

8. Bwana akatutoa kutoka Misri kwa mkono wa nguvu, na kwa mkono ulionyoshwa, na kwa utisho mwingi, na kwa ishara, na kwa maajabu;

9. naye ametuingiza mahali hapa, na kutupa nchi hii, nchi ijaayo maziwa na asali.

10. Na sasa, tazama, nimeleta malimbuko ya mazao ya ardhi uliyonipa, Ee Bwana. Kisha ukiweke chini mbele za Bwana, Mungu wako, ukasujudu mbele za Bwana, Mungu wako;

11. ukayafurahie mema yote ambayo Bwana, Mungu wako, amekupa, na nyumba yako, wewe, na Mlawi, na mgeni aliye kati yako.

12. Utakapokwisha kutoa zaka, katika zaka zote za maongeo yako mwaka wa tatu, ambao ndio mwaka wa kutolea zaka, umpe zile zaka Mlawi, na mgeni, na yatima, na mjane, wapate kula ndani ya malango yako na kushiba;

13. nawe sema mbele ya Bwana, Mungu wako, Vitu vilivyo vitakatifu nimeviondoa katika nyumba yangu, nami mimewapa Mlawi, na mgeni, na yatima, na mjane, kwa mfano wa maagizo yako uliyoniusia yote; sikukosa maagizo yako yo yote, wala sikuyasahau;

14. katika vitu hivyo sikula wakati wa kukaa matanga mimi, wala sikuviondoa nikiwa na unajisi, wala sikutoa kwa ajili ya wafu katika vitu hivyo; sauti ya Bwana, Mungu wangu, nimeisikiza, nimefanya yote, kama ulivyoniamuru.

15. Uangalie kutoka makazi yako matakatifu mbinguni, uwabarikie watu wako Israeli, na nchi uliyotupa kama ulivyowaapia baba zetu, nchi imiminikayo maziwa na asali.

16. Leo hivi akuamuru Bwana, Mungu wako, kuzifanya amri hizi na hukumu; basi uzishike na kuzifanya kwa moyo wako wote na roho yako yote.

17. Umemwungama Bwana leo, kuwa ndiye Mungu wako, na kuwa yakupasa kutembea katika njia zake, na kushika amri zake na maagizo yake, na hukumu zake, na kusikiza sauti yake;

18. naye Bwana amekuungama hivi leo kuwa taifa iliyotengwa iwe yake yeye, kama alivyokuahidi, na kuwa yakupasa kushika maagizo yake yote;

19. na kuwa atakutukuza juu ya mataifa yote aliyoyafanya, kwa sifa, na jina, na heshima, nawe upate kuwa taifa takatifu kwa Bwana, Mungu wako, kama alivyosema.

About Kumbukumbu la Torati Chapter 26

Read Kumbukumbu la Torati Chapter 26 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of Kumbukumbu la Torati in the Old Testament. Continue reading with the chapter navigation above or explore the complete book.

Book Information

Book: Kumbukumbu la Torati
Chapter: 26
Testament: Old Testament

How to Read this Chapter

Use the Previous and Next Chapter buttons to continue reading Kumbukumbu la Torati. You can also adjust the font size for comfortable reading and browse other books of the Bible using the navigation links.

https://www.youtube.com/watch?v=rzsT_Q3KLzE

More Resources

Continue Reading the Bible

Continue reading Kumbukumbu la Torati Chapter 26 and explore every book, chapter and verse of the Holy Bible. Use the navigation links above and below to move through the Scriptures with ease.

Frequently Asked Questions

What is Kumbukumbu la Torati Chapter 26?

Kumbukumbu la Torati Chapter 26 is part of the Book of Kumbukumbu la Torati in the Holy Bible.

Can I read this chapter online?

Yes. You can read the complete Kumbukumbu la Torati Chapter 26 online for free with easy chapter navigation.

More Chapters from Agano la Kale

  1. Zaburi Chapter 1
  2. Habakuki Chapter 3
  3. Ayubu Chapter 1
  4. Zaburi Chapter 2
  5. Ayubu Chapter 4
  6. Kutoka Chapter 11
  7. Kutoka Chapter 2

Explore More from Kumbukumbu La Torati

  1. Kumbukumbu la Torati Chapter 23
  2. Kumbukumbu la Torati Chapter 10
  3. Kumbukumbu la Torati Chapter 22
  4. Kumbukumbu la Torati Chapter 30
  5. Kumbukumbu la Torati Chapter 21
  6. Kumbukumbu la Torati Chapter 28
  7. Kumbukumbu la Torati Chapter 4

Related Chapters & Readings

  1. 1 Wafalme Chapter 1
  2. Isaya Chapter 23
  3. Ufunuo wa Yohana Chapter 10
  4. Ezekieli Chapter 43
  5. Ezra Chapter 2
  6. Isaya Chapter 12
  7. Ezekieli Chapter 2
Share Your Love

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *