1 Samweli Chapter 12

For English

Read 1 Samweli Chapter 12 Online

Read 1 Samweli Chapter 12 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of 1 Samweli in the Old Testament. Browse every verse with easy chapter navigation, continue to the next chapter, or explore the complete Book of 1 Samweli and the Holy Bible online.

Choose a Chapter

1 Samweli 12

Sura 12

1. Kisha Samweli akawaambia Israeli wote, Angalieni, nimeisikiliza sauti yenu katika hayo yote mliyoniambia, nami nimemtawaza mfalme juu yenu.

2. Basi sasa, angalieni, mfalme anakwenda mbele yenu; na mimi ni mzee, mwenye mvi; tena, tazameni, wana wangu wapo pamoja nanyi; nami nimekwenda mbele yenu toka ujana wangu hata leo.

3. Nami nipo hapa; basi, mnishuhudie mbele za Bwana, na mbele ya masihi wake, nalitwaa ng`ombe wa nani? au nalitwaa punda wa nani? au ni nani niliye mdhulumu? Ni nani niliyemwonea? Au kwa mkono wa nani nimepokea rushwa inipofushe macho? Nami nitawarudishia ninyi.

4. Nao wakasema, hukutudhulumu, wala hukutuonea, wala hukupokea kitu kwa mkono wa mtu awaye yote.

5. Akawaambia, Bwana ni shahidi juu yenu, na masihi

6. Samweli akawaambia watu, Ni yeye Bwana aliyewaweka Musa na Haruni, ndiye yeye aliyewatoa baba zenu kutoka nchi ya Misri.

7. Basi sasa simameni, ili niwahutubie mbele za Bwana, kwa kutaja matendo yote ya haki ya Bwana, aliyowatendea ninyi na baba zenu.

8. Yakobo alipokuwa ameingia Misri, na baba zenu walipomlilia Bwana, ndipo Bwana akawapeleka Musa na Haruni, nao wakawatoa baba zenu kutoka Misri, wakawakalisha mahali hapa.

9. Lakini wakamsahau Bwana, Mungu wao, naye akawauza na kuwatia katika mikono ya Sisera, jemadari wa jeshi la Hazori, na katika mikono ya Wafilisti, na katika mikono ya mfalme wa Moabu, nao wakapigana nao.

10. Nao wakamlilia Bwana, wakasema, Tumefanya dhambi, kwa kuwa tumemwacha Bwana, na kuwatumikia Mabaali na Maashtorethi; lakini sasa utuokoe na mikono ya adui zetu, nasi tutakutumikia wewe.

11. Bwana akawatuma Yerubaali, na Baraka, na Yeftha, na Samweli, akawaokoa ninyi na mikono ya adui zenu pande zote, nanyi mkakaa salama.

12. Hata mlipomwona Nahashi, mfalme wa wana wa Amoni, amekuja kupigana nanyi, mliniambia, Sivyo, lakini mfalme atatutawala; ingawa Bwana, Mungu wenu, ni mfalme wenu.

13. Basi sasa, mtazameni mfalme mliyemchagua na kumtaka; tazameni, Bwana ameweka mfalme juu yenu.

14. Kama mkimcha Bwana, na kumtumikia, na kuisikia sauti yake, msiiasi amri ya Bwana, tena kama ninyi, na mfalme anayewatawala, mkimfuata Bwana, Mungu wenu, vema!

15. Bali msipoisikia sauti ya Bwana, mkiiasi amri ya Bwana, ndipo mkono wa Bwana utakuwa juu yenu, kama ulivyokuwa juu ya baba zenu.

16. Na sasa simameni, mkalione jambo hili kubwa, Bwana atakalolitenda mbele ya macho yenu.

17. Leo je! Si mavuno ya ngano? Nitamwomba Bwana, kwamba apeleke ngurumo na mvua; nanyi mtajua na kuona ya kuwa uovu wenu ni mwingi sana, mlioufanya machoni pa Bwana, kwa kujitakia mfalme.

18. Basi Samweli akamwomba Bwana, naye Bwana akapeleka ngurumo na mvua siku ile; nao watu wote wakamwogopa Bwana sana, na Samweli pia.

19. Watu wote wakamwambia Samweli, Utuombee sisi watumwa wako kwa Bwana, Mungu wako, tusije tukafa; maana tumeongeza dhambi zetu zote kwa uovu huu, wa kujitakia mfalme.

20. Samweli akawaambia, Msiogope; ni kweli mmeutenda uovu huu wote; lakini msigeuke na kuacha kumfuata Bwana, bali mtumikieni Bwana kwa mioyo yenu yote.

21. Wala msigeuke upande, maana, kufuata vitu vya ubatili,

22. visivyoweza kusaidia wala kuokoa, kwa kuwa havifai kitu. Maana Bwana hatawaacha watu wake kwa ajili ya jina lake kuu; kwa kuwa imempendeza Bwana kuwafanya ninyi kuwa watu wake mwenyewe.

23. Walakini mimi, hasha! Nisimtende Bwana dhambi kwa kuacha kuwaombea ninyi; lakini nitawaelimisha katika njia iliyo njema, na kunyoka

24. Mcheni Bwana tu, mkamtumikie kwa kweli kwa mioyo yenu yote; maana, kumbukeni jinsi alivyowatendea mambo makuu.

25. Lakini kama mkiendelea kutenda mabaya, mtaangamia, ninyi na mfalme wenu pia.

About 1 Samweli Chapter 12

Read 1 Samweli Chapter 12 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of 1 Samweli in the Old Testament. Continue reading with the chapter navigation above or explore the complete book.

Book Information

Book: 1 Samweli
Chapter: 12
Testament: Old Testament

How to Read this Chapter

Use the Previous and Next Chapter buttons to continue reading 1 Samweli. You can also adjust the font size for comfortable reading and browse other books of the Bible using the navigation links.

https://www.youtube.com/watch?v=rzsT_Q3KLzE

More Resources

Continue Reading the Bible

Continue reading 1 Samweli Chapter 12 and explore every book, chapter and verse of the Holy Bible. Use the navigation links above and below to move through the Scriptures with ease.

Frequently Asked Questions

What is 1 Samweli Chapter 12?

1 Samweli Chapter 12 is part of the Book of 1 Samweli in the Holy Bible.

Can I read this chapter online?

Yes. You can read the complete 1 Samweli Chapter 12 online for free with easy chapter navigation.

More Chapters from 1-samweli

  1. 1 Samweli Chapter 1
  2. 1 Samweli Chapter 11
  3. 1 Samweli Chapter 2
  4. 1 Samweli Chapter 6
  5. 1 Samweli Chapter 23
  6. 1 Samweli Chapter 22
  7. 1 Samweli Chapter 9

Explore More from Agano la Kale

  1. Zaburi Chapter 126
  2. Zaburi Chapter 105
  3. Yeremia Chapter 37
  4. Mhubiri Chapter 1
  5. Zaburi Chapter 71
  6. Isaya Chapter 33
  7. Yoshua Chapter 20

Related Chapters & Readings

  1. Isaya Chapter 7
  2. Mambo ya Walawi Chapter 6
  3. 3 Yohana Chapter 1
  4. Danieli Chapter 7
  5. Mathayo Chapter 8
  6. Wakolosai Chapter 2
  7. Yohana Chapter 5
Share Your Love

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *