Mika Chapter 1

For English

Read Mika Chapter 1 Online

Read Mika Chapter 1 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of Mika in the Old Testament. Browse every verse with easy chapter navigation, continue to the next chapter, or explore the complete Book of Mika and the Holy Bible online.

Choose a Chapter

Mika 1

Sura 1

1. Hili ndilo neno la Bwana lililomjia Mika, Mmorashti, katika siku za Yothamu, na Ahazi, na Hezekia, wafalme wa Yuda; maono aliyoyaona katika habari za Samaria, na Yerusalemu.

2. Sikilizeni, enyi watu wa kabila zote; sikiliza, Ee dunia, na vyote vilivyomo; Bwana MUNGU na ashuhudie juu yenu, yeye Bwana kutoka hekalu lake takatifu.

3. Kwa maana, angalieni, Bwana anakuja akitoka mahali pake, naye atashuka, na kupakanyaga mahali pa dunia palipoinuka.

4. Na hiyo milima itayeyuka chini yake, nayo mabonde yatapasuliwa, kama vile nta iliyo mbele ya moto, kama maji yaliyomwagika tena kutelemka gengeni.

5. Kwa sababu ya kosa la Yakobo yametokea haya yote, na kwa sababu ya makosa ya nyumba ya Israeli. Nini kosa la Yakobo? Je, silo Samaria? Na nini mahali pa Yuda palipoinuka? Sipo Yerusalemu?

6. Kwa ajili ya hayo nitafanya Samaria kuwa kama chungu katika shamba, na kama miche ya shamba la mizabibu; nami nitayatupa mawe yake bondeni, nami nitaifunua misingi yake.

7. Na sanamu zake zote za kuchonga zitapondwa-pondwa, na ijara zake zote zitateketezwa kwa moto, na sanamu zake zote nitazifanya ukiwa; kwa kuwa amezikusanya kwa ujira wa kahaba, nazo zitaurudia ujira wa kahaba.

8. Kwa ajili ya hayo nitaomboleza na kulia, Nitakwenda nimevua nguo, ni uchi; Nitafanya mlio kama wa mbweha, Na maombolezo kama ya mbuni.

9. Kwa maana jeraha zake haziponyekani; Maana msiba umeijilia hata Yuda, Unalifikia lango la watu wangu, Naam, hata Yerusalemu.

10. Msiyahubiri haya katika Gathi, msilie kamwe; Katika Beth-le-Afra ugae-gae mavumbini.

11. Piteni; uende ukaaye Shafiri, hali ya uchi na aibu; Hivyo akaaye Saanani hajatokea nje; Maombolezo ya Beth-eseli yatawaondolea tegemeo lake;

12. Maana akaaye Marothi ana utungu wa mema; Kwa kuwa msiba umeshuka toka kwa Bwana, Umefika mpaka lango la Yerusalemu.

13. Mfungie gari la vita farasi Aliye mwepesi, ukaaye Lakishi; Alikuwa mwanzo wa dhambi kwa binti Sayuni; Maana makosa ya Israeli yameonekana kwako.

14. Kwa hiyo utaipa Moresheth-Gathi zawadi ya kuagia; Nyumba za Akzibu zitakuwa kijito kidanganyacho wafalme wa Israeli.

15. Bado, ukaaye Maresha, nitakuletea yeye atakayekumiliki; Utukufu wa Israeli utafika mpaka Adulamu.

16. Jifanyie upaa, jikate nywele zako, Kwa ajili ya watoto waliokufurahisha; Panua upaa wako kama tai; Kwa maana wamekwenda mbali nawe utumwani.

About Mika Chapter 1

Read Mika Chapter 1 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of Mika in the Old Testament. Continue reading with the chapter navigation above or explore the complete book.

Book Information

Book: Mika
Chapter: 1
Testament: Old Testament

How to Read this Chapter

Use the Previous and Next Chapter buttons to continue reading Mika. You can also adjust the font size for comfortable reading and browse other books of the Bible using the navigation links.

https://www.youtube.com/watch?v=rzsT_Q3KLzE

More Resources

Continue Reading the Bible

Continue reading Mika Chapter 1 and explore every book, chapter and verse of the Holy Bible. Use the navigation links above and below to move through the Scriptures with ease.

Frequently Asked Questions

What is Mika Chapter 1?

Mika Chapter 1 is part of the Book of Mika in the Holy Bible.

Can I read this chapter online?

Yes. You can read the complete Mika Chapter 1 online for free with easy chapter navigation.

More Chapters from Agano la Kale

  1. Zaburi Chapter 1
  2. Habakuki Chapter 3
  3. Ayubu Chapter 1
  4. Zaburi Chapter 2
  5. Kutoka Chapter 11
  6. Kutoka Chapter 2
  7. Ayubu Chapter 4

Explore More from Mika

  1. Mika Chapter 1
  2. Mika Chapter 2
  3. Mika Chapter 4
  4. Mika Chapter 5
  5. Míka Chapter 7
  6. Mika Chapter 7
  7. Mika Chapter 7

Related Chapters & Readings

  1. Isaya Chapter 46
  2. Zaburi Chapter 143
  3. Ezekieli Chapter 27
  4. Ufunuo wa Yohana Chapter 11
  5. Amosi Chapter 5
  6. Mwanzo Chapter 35
  7. Mika Chapter 6
Share Your Love

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *