Mwanzo Chapter 9

For English

Read Mwanzo Chapter 9 Online

Read Mwanzo Chapter 9 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of Mwanzo in the Old Testament. Browse every verse with easy chapter navigation, continue to the next chapter, or explore the complete Book of Mwanzo and the Holy Bible online.

Choose a Chapter

Mwanzo 9

Sura 9

1. Mungu akambariki Nuhu na wanawe, akawaambia, Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi.

2. Kila mnyama wa katika nchi atawaogopa ninyi na kuwahofu, na kila ndege wa angani: pamoja na vitu vyote vilivyojaa katika ardhi, na samaki wote wa baharini; vimetiwa mikononi mwenu.

3. Kila kiendacho kilicho hai kitakuwa chakula chenu, kama nilivyowapa mboga za majani, kadhalika nawapeni hivi vyote.

4. Bali nyama pamoja na uhai, yaani, damu yake, msile.

5. Hakika damu yenu ya uhai wenu nitaitaka; na kwa mkono wa kila mnyama nitaitaka; na kwa mkono wa mwanadamu, kwa mkono wa ndugu ya mtu nitataka uhai wa mwanadamu.

6. Atakayemwaga damu ya mwanadamu, damu yake huyo itamwagwa na mwanadamu, maana kwa mfano wake Mungu alimfanya mwanadamu.

7. Nanyi zaeni, mkaongezeke; zaeni sana katika nchi, mkaongezeke ndani yake.

8. Mungu akamwambia Nuhu, na wanawe pamoja naye, akisema,

9. Mimi, tazama, nalithibitisha agano langu nanyi; tena na uzao wenu baada yenu;

10. tena na kila kiumbe hai kilichoko pamoja nanyi, ndege, na mnyama wa kufugwa, na kila mnyama wa mwitu katika nchi pamoja nanyi; wote wanaotoka katika safina, hata kila kilicho hai katika nchi.

11. Na agano langu nitalithibitisha nanyi; wala kila chenye mwili hakitafutwa tena kwa maji ya gharika; wala hakutakuwa tena gharika, baada ya hayo, kuiharibu nchi.

12. Mungu akasema, Hii ndiyo ishara ya agano nifanyalo kati yangu na ninyi, na kila kiumbe hai kilichoko pamoja nanyi, kwa vizazi vyote hata milele;

13. Mimi nauweka upinde wangu winguni, nao utakuwa ni ishara ya agano kati yangu na nchi.

14. Hata itakuwa nikitanda mawingu juu ya nchi, upinde utaonekana winguni,

15. nami nitalikumbuka agano langu, lililoko kati yangu na ninyi, na kila kiumbe hai katika wote wenye mwili, wala maji hayatakuwa gharika tena kuwaharibu wote wenye mwili.

16. Basi huo upinde utakuwa winguni; nami nitauangalia nipate kulikumbuka agano la milele lililoko kati ya Mungu na kila kiumbe hai katika wote wenye mwili kilichoko katika nchi.

17. Mungu akamwambia Nuhu, Hii ndiyo ishara ya agano nililoliweka kati yangu na wote wenye mwili walioko katika nchi.

18. Wana wa Nuhu waliotoka katika safina, ni Shemu, na Hamu, na Yafethi; na Hamu ndiye baba wa Kanaani.

19. Hawa watatu walikuwa wana wa Nuhu na kwa hao nchi yote ikaenea watu.

20. Nuhu akaanza kuwa mkulima, akapanda mizabibu;

21. akanywa divai, akalewa; akawa uchi katika hema yake.

22. Hamu, baba wa Kanaani, akauona uchi wa baba yake, akawaeleza ndugu zake wawili waliokuwa nje.

23. Shemu na Yafethi wakatwaa vazi, wakalitanda mabegani mwao wote wawili, wakaenda kinyumenyume, wakaufunika uchi wa baba yao; na nyuso zao zilielekea nyuma, wala hawakuuona uchi wa baba yao.

24. Nuhu akalevuka katika ulevi wake, akajua mwana wake mdogo alivyomtendea.

25. Akasema, Na alaaniwe Kaanani; Atakuwa mtumwa kabisa kwa ndugu zake.

26. Akasema, Na atukuzwe Bwana, Mungu wa Shemu; Na kaanani awe mtumwa wake.

27. Mungu akamnafisishe Yafethi, Na akae katika hema za Shemu; Na kaanani awe mtumwa wake.

28. Na Nuhu akaishi baada ya ile gharika miaka mia tatu na hamsini.

29. Siku zote za Nuhu zilikuwa miaka mia kenda na hamsini, akafa.

About Mwanzo Chapter 9

Read Mwanzo Chapter 9 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of Mwanzo in the Old Testament. Continue reading with the chapter navigation above or explore the complete book.

Book Information

Book: Mwanzo
Chapter: 9
Testament: Old Testament

How to Read this Chapter

Use the Previous and Next Chapter buttons to continue reading Mwanzo. You can also adjust the font size for comfortable reading and browse other books of the Bible using the navigation links.

https://www.youtube.com/watch?v=rzsT_Q3KLzE

More Resources

Continue Reading the Bible

Continue reading Mwanzo Chapter 9 and explore every book, chapter and verse of the Holy Bible. Use the navigation links above and below to move through the Scriptures with ease.

Frequently Asked Questions

What is Mwanzo Chapter 9?

Mwanzo Chapter 9 is part of the Book of Mwanzo in the Holy Bible.

Can I read this chapter online?

Yes. You can read the complete Mwanzo Chapter 9 online for free with easy chapter navigation.

More Chapters from Agano la Kale

  1. Zaburi Chapter 1
  2. Habakuki Chapter 3
  3. Ayubu Chapter 1
  4. Zaburi Chapter 2
  5. Kutoka Chapter 11
  6. Kutoka Chapter 2
  7. Ayubu Chapter 4

Explore More from mwanzo

  1. Mwanzo Chapter 30
  2. Mwanzo Chapter 21
  3. Mwanzo Chapter 4
  4. Mwanzo Chapter 28
  5. Mwanzo Chapter 18
  6. Mwanzo Chapter 34
  7. Mwanzo Chapter 45

Related Chapters & Readings

  1. Matendo ya Mitume Chapter 16
  2. Ayubu Chapter 21
  3. Mwanzo Chapter 30
  4. Zaburi Chapter 28
  5. Hesabu Chapter 18
  6. Mwanzo Chapter 15
  7. Zaburi Chapter 138
Share Your Love

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *