Yoshua Chapter 15

For English

Read Yoshua Chapter 15 Online

Read Yoshua Chapter 15 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of Yoshua in the Old Testament. Browse every verse with easy chapter navigation, continue to the next chapter, or explore the complete Book of Yoshua and the Holy Bible online.

Choose a Chapter

Yoshua 15

Sura 15

1. Kura ya kabila ya wana wa Yuda kwa kuandama jamaa zao ilikuwa kufikilia hata mpaka wa Edomu, hata bara ya Sini upande wa kusini, huko mwisho upande wa kusini.

2. Mpaka wao wa kusini ulikuwa kutoka mwisho wa Bahari ya Chumvi, kutoka ile hori ielekeayo kusini;

3. nao ukaendelea upande wa kusini wa kukwea kwenda Akrabimu, kisha ukaendelea hata Sini, kisha ukaenda upande wa kusini wa Kadesh-barnea, kisha ukaendelea karibu na Hesroni, kisha ukafikilia Adari, na kuzunguka kwendea Karka;

4. kisha ukaendelea hata Azmoni, na kutokea hapo penye kijito cha Misri; na matokeo ya huo mpaka yalikuwa baharini; huu ndio mpaka wenu wa upande wa kusini.

5. Na mpaka wa upande wa mashariki ulikuwa Bahari ya Chumvi, hata mwisho wa mto wa Yordani. Na mpaka wa upande wa kaskazini ulikuwa kutoka pale penye hori ya baharini mwisho wa mto wa Yordani;

6. na huo mpaka ukaendelea hata Beth-hogla, kisha ukaendelea upande wa kaskazini wa Beth-araba; kisha mpaka ukaendelea hata jiwe la Bohani mwana wa Reubeni;

7. kisha mpaka ukaendelea hata Debiri kutoka bonde la Akori, vivyo ukaendelea upande wa kaskazini, kwa kuelekea Gilgali, iliyo mkabala wa kukwelea kwenda Adumimu, ulio upande wa kusini wa mto; kisha huo mpaka ukaendelea hata ukafikilia maji ya Enshemeshi, na matokeo yake yalikuwa hapo Enrogeli;

8. kisha mpaka ukaendelea karibu na bonde la mwana wa Hinomu, na kufikilia ubavuni mwa huyu Myebusi upande wa kusini (ndio Yerusalemu); kisha mpaka ukaendelea hata kilele cha mlima ulio pale mkabala wa bonde la Hinomu upande wa magharibi, lililo pale mwisho wa bonde la Warefai upande wa kaskazini;

9. kisha mpaka ulipigwa kutoka juu ya mlima huo hata kufikilia chemchemi ya maji ya Neftoa kisha ukatokea hata miji ya kilima cha Efroni; kisha mpaka ulipigwa hata kufikilia Baala (ndio Kiriath-yearimu);

10. kisha mpaka ukazunguka kutoka Baala kwendelea upande wa magharibi hata kilima Seiri, kisha ukaendelea hata upande wa mlima wa Yearimu upande wa kaskazini (huo ndio Kesaloni), kisha ukatelemkia Beth-shemeshi, na kwendelea karibu na Timna;

11. kisha mpaka ukatokea hata kufikilia upande wa Ekroni upande wa kaskazini; tena mpaka ulipigwa hata Shikroni, na kwendelea hata kilima cha Baala, kisha ukatokea hapo Yabneeli; na matokeo ya mpaka yalikuwa baharini.

12. Na mpaka wa upande wa magharibi ulifikilia hata bahari kubwa, na mpaka wake. Huo ndio mpaka wa wana wa Yuda kwa kuzunguka kote kote sawasawa na jamaa zao.

13. Kisha alimpa huyo Kalebu mwana wa Yefune sehemu kati ya wana wa Yuda, kama Bwana alivyomwamuru Yoshua, maana ni Kiriath-arba, ni huyo Arba aliyekuwa babaye Anaki (huo ndio Hebroni).

14. Huyo Kalebu aliwafukuza watoke hapo hao wana watatu wa Anaki, nao ni Sheshai, na Ahimani, na Talmai, wana wa Anaki.

15. Kisha akakwea kutoka huko ili kuwaendea wenyeji wa Debiri; jina la Debiri hapo kwanza lilikuwa Kiriath-seferi.

16. Kalebu akasema, Yeye atakayeupiga Kiriath-seferi na kuutwaa, mimi nitampa Aksa binti yangu awe mkewe.

17. Naye Othnieli mwana wa Kenazi, nduguye Kalebu, aliutwaa; basi akampa Aksa binti yake awe mkewe.

18. Kisha ikawa, hapo huyo mwanamke alipokwenda kwa mumewe, akamtaka aombe shamba kwa baba yake; akashuka katika punda wake; Kalebu akamwuliza, Wataka nini?

19. Huyo mwanamke akasema, Nipe baraka; kwa kuwa umeniweka katika nchi ya kusini, unipe na chemchemi za maji pia. Ndipo akampa chemchemi za maji ya juu, na chemchemi za maji ya chini.

20. Huu ndio urithi wa kabila ya wana wa Yuda sawasawa na jamaa zao.

21. Miji ya mwisho ya kabila ya wana wa Yuda upande wa kuelekea mpaka wa Edomu katika nchi ya Negebu ilikuwa ni Kabseeli, na Ederi, na Yaguri;

22. na Kina, na Dimona, na Adada;

23. na Kedeshi, na Hazori, na Ithnani;

24. na Zifu, na Telemu, na Bealothi;

25. na Hazor-hadata, na Kerioth-hezroni (ndio Hazori);

26. na Amamu, na Shema, na Molada;

27. na Hasar-gada, na Heshmoni, na Bethpeleti;

28. na Hasarshuali, na Beer-sheba, na Biziothia;

29. na Baala, na Iyimu, na Esemu;

30. na Eltoladi, na Kesili, na Horma;

31. na Siklagi, na Madmana, na Sansana;

32. na Lebaothi, na Shilhimu, na Aini, na Rimoni; miji hiyo yote ni miji ishirini na kenda, pamoja na vijiji vyake.

33. Katika nchi ya Shefela, Eshtaoli, na Sora, na Ashna,

34. na Zanoa, na Enganimu, na Tapua, na Enamu;

35. na Yarmuthi, na Adulamu, na Soko, na Azeka;

36. na Shaarimu, na Adithaimu, na Gedera, na Gederothaimu miji kumi na minne, pamoja na vijiji vyake.

37. Senani, na Hadasha, na Migdal-gadi;

38. na Dilani, na Mispe, na Yoktheeli;

39. na Lakishi, na Boskathi, na Egloni;

40. na Kaboni, na Lamasi, na Kithilishi;

41. na Gederothi, na Beth-dagoni, na Naama, na Makeda; miji kumi na sita, pamoja na vijiji vyake.

42. Libna, na Etheri, na Ashani;

43. na Yifta, na Ashna, na Nesibu;

44. na Keila, na Akizibu, na Maresha; miji kenda, pamoja na vijiji vyake.

45. Ekroni, pamoja na miji yake na vijiji vyake;

46. kutoka huko Ekroni mpaka baharini, yote iliyokuwa upande wa Ashdodi, pamoja na vijiji vyake.

47. Ashdodi, na miji yake na vijiji vyake; na Gaza, na miji yake na vijiji vyake; mpaka kijito cha Misri, na bahari kubwa, na mpaka wake.

48. Na katika nchi ya vilima, Shamiri, na Yatiri, na Soko;

49. na Dana, na Kiriath-sana (ambao ni Debiri);

50. na Anabu, na Eshtemoa, na Animu;

51. na Gosheni, na Holoni, na Gilo; miji kumi na mmoja, pamoja na vijiji vyake.

52. Arabu, na Duma, na Eshani;

53. na Yanumu, na Beth-tapua, na Afeka;

54. na Humta, na Kiriath-arba (ndio Hebroni), na Siori; miji kenda, pamoja na vijiji vyake.

55. Maoni, na Karmeli, na Zifu, na Yuta;

56. na Yezreeli, na Yokdeamu, na Zanoa;

57. na Kaini, na Gibea, na Timna; miji kumi, pamoja na vijiji vyake.

58. Halhuli, na Bethsuri, na Gedori;

59. na Maarathi, na Bethanothi, Eltekoni; miji sita, pamoja na vijiji vyake.

60. Kiriath-baali (ndio Kiriath-yearimu), na Raba; miji miwili, pamoja vijiji vyake.

61. Huko nyikani, Betharaba, na Midini, na Sekaka;

62. na Nibshani, na huo Mji wa Chumvi, na Engedi; miji sita, pamoja na vijiji vyake.

63. Tena katika habari ya Wayebusi, hao wenye kukaa Yerusalemu, wana wa Yuda hawakuweza kuwatoa; lakini hao Wayebusi walikaa pamoja na wana wa Yuda huko Yerusalemu hata hivi leo.

About Yoshua Chapter 15

Read Yoshua Chapter 15 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of Yoshua in the Old Testament. Continue reading with the chapter navigation above or explore the complete book.

Book Information

Book: Yoshua
Chapter: 15
Testament: Old Testament

How to Read this Chapter

Use the Previous and Next Chapter buttons to continue reading Yoshua. You can also adjust the font size for comfortable reading and browse other books of the Bible using the navigation links.

https://www.youtube.com/watch?v=rzsT_Q3KLzE

More Resources

Continue Reading the Bible

Continue reading Yoshua Chapter 15 and explore every book, chapter and verse of the Holy Bible. Use the navigation links above and below to move through the Scriptures with ease.

Frequently Asked Questions

What is Yoshua Chapter 15?

Yoshua Chapter 15 is part of the Book of Yoshua in the Holy Bible.

Can I read this chapter online?

Yes. You can read the complete Yoshua Chapter 15 online for free with easy chapter navigation.

More Chapters from Agano la Kale

  1. Zaburi Chapter 1
  2. Habakuki Chapter 3
  3. Ayubu Chapter 1
  4. Zaburi Chapter 2
  5. 1 Samweli Chapter 1
  6. Kutoka Chapter 11
  7. Kutoka Chapter 2

Explore More from yoshua

  1. Yoshua Chapter 4
  2. Yoshua Chapter 24
  3. Yoshua Chapter 12
  4. Yoshua Chapter 14
  5. Yoshua Chapter 2
  6. Yoshua Chapter 6
  7. Yoshua Chapter 13

Related Chapters & Readings

  1. 2 Samweli Chapter 22
  2. 2 Wafalme Chapter 14
  3. Ayubu Chapter 37
  4. Yeremia Chapter 3
  5. 1 Wakorintho Chapter 12
  6. 2 Mambo ya Nyakati Chapter 6
  7. 1 Wafalme Chapter 18
Share Your Love

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *