Waamuzi Chapter 14

For English

Read Waamuzi Chapter 14 Online

Read Waamuzi Chapter 14 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of Waamuzi in the Old Testament. Browse every verse with easy chapter navigation, continue to the next chapter, or explore the complete Book of Waamuzi and the Holy Bible online.

Choose a Chapter

Waamuzi 14

Sura 14

1. Samsoni akatelemkia Timna, akaona mwanamke huko Timna, mmojawapo wa binti za Wafilisti.

2. Kisha akapanda, akawaambia baba yake na mama yake, akasema, Nimemwona mwanamke huko Timna, mmojawapo wa binti za Wafilisti; basi mnipatie, nimwoe.

3. Ndipo baba yake na mama yake wakamwambia, Je! Hapana mwanamke hata mmoja katika ndugu zako, au katika jamaa zangu zote, hata uende kumwoa mwanamke kwa hawa Wafilisti wasiotahiriwa? Samsoni akamwambia baba yake; Mnipatie huyo, kwa maana ananipendeza sana.

4. Lakini baba yake na mama yake hawakujua ya kuwa jambo hili ni la Bwana; maana alitaka kisa juu ya Wafilisti. Basi wakati ule Wafilisti walikuwa wakiwatawala Israeli.

5. Ndipo Samsoni na baba yake na mama yake wakatelemkia Timna, wakafika mashamba ya mizabibu huko Timna; na tazama, mwana-simba akamngurumia.

6. Roho ya Bwana ikamjilia kwa nguvu, naye akampasua kana kwamba anampasua mwana-mbuzi, wala hakuwa na kitu cho chote mkononi mwake; lakini hakuwaambia baba yake na mama yake aliyoyafanya.

7. Basi akatelemka na kuzungumza na huyo mwanamke; naye akampendeza Samsoni sana.

8. Kisha baadaye akarudi ili kumtwaa, naye akageuka kando kuuangalia mzoga wa huyo simba; na tazama, nyuki wengi walikuwamo ndani ya mzoga wa simba, na asali.

9. Akatwaa asali mikononi mwake akaenda mbele, huku akila alipokuwa akienenda, akawafikilia babaye na mamaye, akawapa, nao wakala; lakini hakuwaambia ya kuwa ameitwaa hiyo asali katika mzoga wa simba.

10. Basi babaye akamtelemkia huyo mwanamke; Samsoni naye akafanya karamu huko; kwa kuwa vijana ndivyo walivyokuwa wakifanya.

11. Basi ikawa hapo walipomwona, wakamletea wenziwe thelathini, wawe pamoja naye.

12. Samsoni akawaambia, Mimi nitawategea ninyi kitendawili; kama mwaweza kunionyesha katika hizo siku saba za karamu, na kukitambua, ndipo hapo nitawapa mavazi thelathini ya kitani na mavao mengine thelathini;

13. lakini msipoweza kunionyesha ndipo hapo ninyi mtanipa mimi mavazi thelathini ya kitani na mavao mengine thelathini. Basi wakamwambia, Haya, tega kitendawili chako, ili tupate kukisikia.

14. Naye akawaambia, Katika huyo mwenye kula kikatoka chakula, Katika huyo mwenye nguvu ukatoka utamu.

15. Ikawa kwa siku ya saba, wakamwambia mkewe Samsoni, Mbembeleze mumeo, ili atuonyeshe hicho kitendawili, tusije tukakuteketeza moto wewe na nyumba ya baba yako; je! Mmetuita ili mpate kuichukua mali yetu? Je! Sivyo?

16. Basi mkewe Samsoni akalia mbele yake, akasema, Wewe wanichukia tu, wala hunipendi; wewe umewategea kitendawili hao wana wa watu wangu, nawe hukuniambia mimi. Naye akamwambia, Angalia, sikumwambia baba yangu wala mama yangu, nami nikuambie wewe?

17. Naye akalia mbele yake hizo siku saba, wakati ulioendelea karamu yao; basi ikawa siku ya saba akamwambia, kwa sababu alikuwa akimsisitiza sana; naye akawaambia wale wana wa watu wake hicho kitendawili.

18. Nao watu wa mji wakamwambia siku ya saba kabla ya jua kuchwa, Ni kitu gani kilicho tamu kuliko asali? Ni kitu gani kilicho na nguvu kuliko simba? Naye akawaambia, kwamba hamkulima na mtamba wangu, Hamngekitambua kitendawili changu.

19. Roho ya Bwana ikamjilia juu yake kwa nguvu, naye akatelemkia Ashkeloni, akapiga watu waume thelathini katika watu hao, na kuzitwaa nyara zao, na kuwapa hao waliokitambua kitendawili mavao hayo. Hasira zake zikamwaka, naye akakwea kwenda nyumbani kwa baba yake.

20. Lakini huyo mke wa Samsoni aliozwa mwenzake, ambaye alikuwa amemtendea kama rafikiye.

About Waamuzi Chapter 14

Read Waamuzi Chapter 14 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of Waamuzi in the Old Testament. Continue reading with the chapter navigation above or explore the complete book.

Book Information

Book: Waamuzi
Chapter: 14
Testament: Old Testament

How to Read this Chapter

Use the Previous and Next Chapter buttons to continue reading Waamuzi. You can also adjust the font size for comfortable reading and browse other books of the Bible using the navigation links.

https://www.youtube.com/watch?v=rzsT_Q3KLzE

More Resources

Continue Reading the Bible

Continue reading Waamuzi Chapter 14 and explore every book, chapter and verse of the Holy Bible. Use the navigation links above and below to move through the Scriptures with ease.

Frequently Asked Questions

What is Waamuzi Chapter 14?

Waamuzi Chapter 14 is part of the Book of Waamuzi in the Holy Bible.

Can I read this chapter online?

Yes. You can read the complete Waamuzi Chapter 14 online for free with easy chapter navigation.

More Chapters from Agano la Kale

  1. Zaburi Chapter 1
  2. Habakuki Chapter 3
  3. Ayubu Chapter 1
  4. Zaburi Chapter 2
  5. Kutoka Chapter 11
  6. Kutoka Chapter 2
  7. Ayubu Chapter 4

Explore More from waamuzi

  1. Waamuzi Chapter 2
  2. Waamuzi Chapter 12
  3. Waamuzi Chapter 21
  4. Waamuzi Chapter 3
  5. Waamuzi Chapter 20
  6. Waamuzi Chapter 8
  7. Waamuzi Chapter 9

Related Chapters & Readings

  1. Zaburi Chapter 44
  2. Mithali Chapter 18
  3. Hesabu Chapter 30
  4. Mambo ya Walawi Chapter 16
  5. 2 Wakorintho Chapter 5
  6. Hesabu Chapter 5
  7. Zaburi Chapter 57
Share Your Love

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *