2 Wafalme Chapter 1

For English

Read 2 Wafalme Chapter 1 Online

Read 2 Wafalme Chapter 1 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of 2 Wafalme in the Old Testament. Browse every verse with easy chapter navigation, continue to the next chapter, or explore the complete Book of 2 Wafalme and the Holy Bible online.

Choose a Chapter

A+ A A-

2 Wafalme 1

Sura 1

1. Ikawa, baada ya kufa kwake Ahabu, Moabu wakawaasi Israeli.

2. Na Ahazia akaanguka katika dirisha la chumba chake orofani, katika Samaria, akaugua; akatuma wajumbe, akawaambia, Enendeni mkaulize kwa Baal-zebubu, mungu wa Ekroni, kwamba nitapona ugonjwa huu.

3. Lakini malaika wa Bwana akamwambia Eliya Mtishbi, Ondoka, uende ukaonane na wale wajumbe wa mfalme wa Samaria, ukawaambie, Je! Ni kwa sababu hapana Mungu katika Israeli, hata mnakwenda kuuliza kwa Baal-zebubu, mungu wa Ekroni?

4. Basi sasa, Bwana asema hivi, Hutashuka katika kile kitanda ulichokipanda, bali hakika utakufa. Eliya akaondoka.

5. Wale wajumbe wakarudi, na mfalme akawaambia, Mbona mmerudi?

6. Wakamwambia, Mtu alitokea, akaonana nasi, akatuambia, Enendeni, rudini kwa mfalme yule aliyewatuma, mkamwambie, Bwana asema hivi Je! Ni kwa sababu hapana Mungu katika Israeli, hata mnakwenda kuuliza kwa Baal-zebubu, mungu wa Ekroni? Basi kwa ajili ya hayo hutashuka katika kile kitanda ulichokipanda, bali hakika utakufa.

7. Akawaambia, Je! Mtu yule aliyetokea, akaonana nanyi, akawaambia maneno hayo, alikuwa mtu wa namna gani?

8. Wakamwambia, Alikuwa amevaa vazi la manyoya, tena amejifunga shuka ya ngozi kiunoni mwake. Naye akasema, Ndiye yule Eliya Mtishbi.

9. Ndipo mfalme akatuma akida wa askari hamsini pamoja na hamsini wake, wamwendee Eliya. Akamwendea, na tazama, ameketi juu ya kilima. Akamwambia, Ewe mtu wa Mungu, mfalme asema, Shuka.

10. Eliya akajibu, akamwambia yule akida wa hamsini, Ikiwa mimi ni mtu wa Mungu, na ushuke moto kutoka mbinguni, ukuteketeze wewe na hamsini wako. Moto ukashuka, ukamteketeza, yeye na hamsini wake.

11. Akatuma tena akida wa hamsini mwingine pamoja na hamsini wake, wamwendee. Akajibu, akamwambia, Ewe mtu wa Mungu, mfalme asema, Shuka upesi.

12. Eliya akajibu, akamwambia, Ikiwa mimi ni mtu wa Mungu, na ushuke moto kutoka mbinguni, ukuteketeze wewe na hamsini wako. Moto wa Mungu ukashuka kutoka mbinguni, ukamteketeza, yeye na hamsini wake.

13. Tena akatuma akida wa hamsini wa tatu, pamoja na hamsini wake. Yule akida wa hamsini wa tatu akapanda, akaenda akapiga magoti mbele ya Eliya, akamsihi sana, akamwambia, Ee mtu wa Mungu, nakusihi, roho yangu, na roho za watumishi wako hawa hamsini, ziwe na thamani machoni pako.

14. Tazama, moto ulishuka kutoka mbinguni, ukawateketeza wale akida wa hamsini wawili wa kwanza pamoja na hamsini wao; laiti sasa roho yangu na iwe na thamani machoni pako.

15. Malaika wa Bwana akamwambia Eliya, Shuka pamoja naye; usimwogope. Akaondoka, akashuka pamoja naye hata kwa mfalme.

16. Akamwambia, Bwana asema hivi, Kwa kuwa umetuma wajumbe waulize kwa Baal-zebubu, mungu wa Ekroni, je! Ni kwa sababu hapana Mungu katika Israeli, uulize neno lake? Kwa hiyo hutashuka katika kile kitanda ulichokipanda, bali hakika utakufa.

17. Basi akafa, sawasawa na neno la Bwana alilolinena Eliya. Na Yoramu alianza kutawala mahali pake katika mwaka wa pili wa Yehoramu mwana wa Yehoshafati mfalme wa Yuda; kwa kuwa yeye hakuwa na mwana.

18. Na mambo yote yaliyosalia aliyoyafanya Ahazia, je! Hayakuandikwa katika kitabu-cha-tarehe cha wafalme wa Israeli?

About 2 Wafalme Chapter 1

Read 2 Wafalme Chapter 1 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of 2 Wafalme in the Old Testament. Continue reading with the chapter navigation above or explore the complete book.

Book Information

Book: 2 Wafalme
Chapter: 1
Testament: Old Testament

How to Read this Chapter

Use the Previous and Next Chapter buttons to continue reading 2 Wafalme. You can also adjust the font size for comfortable reading and browse other books of the Bible using the navigation links.

https://www.youtube.com/watch?v=rzsT_Q3KLzE

More Resources

Continue Reading the Bible

Continue reading 2 Wafalme Chapter 1 and explore every book, chapter and verse of the Holy Bible. Use the navigation links above and below to move through the Scriptures with ease.

Frequently Asked Questions

What is 2 Wafalme Chapter 1?

2 Wafalme Chapter 1 is part of the Book of 2 Wafalme in the Holy Bible.

Can I read this chapter online?

Yes. You can read the complete 2 Wafalme Chapter 1 online for free with easy chapter navigation.

More Chapters from 2-wafalme

  1. 2 Wafalme Chapter 2
  2. 2 Wafalme Chapter 5
  3. 2 Wafalme Chapter 14
  4. 2 Wafalme Chapter 7
  5. 2 Wafalme Chapter 12
  6. 2 Wafalme Chapter 20
  7. 2 Wafalme Chapter 18

Explore More from Agano la Kale

  1. Kutoka Chapter 28
  2. Zaburi Chapter 115
  3. Nehemia Chapter 3
  4. Zaburi Chapter 98
  5. 2 Mambo ya Nyakati Chapter 11
  6. 2 Samweli Chapter 7
  7. 2 Wafalme Chapter 24

Related Chapters & Readings

  1. 1 Mambo ya Nyakati Chapter 8
  2. 2 Samweli Chapter 19
  3. Mathayo Chapter 27
  4. Ruthu Chapter 3
  5. Zaburi Chapter 9
  6. Mwanzo Chapter 44
  7. Ufunuo wa Yohana Chapter 10
Share Your Love

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *