Waebrania Chapter 8

For English

Read Waebrania Chapter 8 Online

Read Waebrania Chapter 8 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of Waebrania in the New Testament. Browse every verse with easy chapter navigation, continue to the next chapter, or explore the complete Book of Waebrania and the Holy Bible online.

Choose a Chapter

Waebrania 8

Sura 8

1. Basi, katika hayo tunayosema, neno lililo kuu ndilo hili: Tunaye kuhani mkuu wa namna hii, aliyeketi mkono wa kuume wa kiti cha enzi cha Ukuu mbinguni,

2. mhudumu wa patakatifu, na wa ile hema ya kweli, ambayo Bwana aliiweka wala si mwanadamu.

3. Maana kila kuhani mkuu huwekwa ili atoe vipawa na dhabihu; kwa hiyo lazima huyu naye awe na kitu cha kutoa.

4. Kama angekuwa juu ya nchi, asingekuwa kuhani; maana wako watoao sadaka kama iagizavyo sheria;

5. watumikiao mfano na kivuli cha mambo ya mbinguni, kama Musa alivyoagizwa na Mungu, alipokuwa tayari kuifanya ile hema; maana asema, Angalia ukavifanye vitu vyote kwa mfano ule ulioonyeshwa katika mlima.

6. Lakini sasa amepata huduma iliyo bora zaidi, kwa kadiri alivyo mjumbe wa agano lililo bora, lililoamriwa juu ya ahadi zilizo bora.

7. Maana kama lile la kwanza lingalikuwa halina upungufu, nafasi isingalitafutwa kwa lile la pili.

8. Maana, awalaumupo, asema Angalia, siku zinakuja, asema Bwana, Nami nitawatimizia nyumba ya Israeli na nyumba ya Yuda agano jipya;

9. Halitakuwa kama agano lile nililoagana na baba zao, Katika siku ile nilipowashika mikono yao niwatoe katika nchi ya Misri. Kwa sababu hawakudumu katika agano langu, Mimi nami sikuwajali asema Bwana.

10. Maana hili ndilo agano nitakaloagana na nyumba ya Israeli Baada ya siku zile, asema Bwana; Nitawapa sheria zangu katika nia zao, Na katika mioyo yao nitaziandika; Nami nitakuwa Mungu kwao, Nao watakuwa watu wangu.

11. Nao hawatafundishana kila mtu na jirani yake, Na kila mtu na ndugu yake, akisema, Mjue Bwana; Kwa maana wote watanijua, Tangu mdogo wao hata mkubwa wao.

12. Kwa sababu nitawasamehe maovu yao, Na dhambi zao sitazikumbuka tena.

13. Kwa kule kusema, Agano jipya, amelifanya lile la kwanza kuwa kuukuu. Lakini kitu kianzacho kuwa kikuukuu na kuchakaa ki karibu na kutoweka.

About Waebrania Chapter 8

Read Waebrania Chapter 8 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of Waebrania in the New Testament. Continue reading with the chapter navigation above or explore the complete book.

Book Information

Book: Waebrania
Chapter: 8
Testament: New Testament

How to Read this Chapter

Use the Previous and Next Chapter buttons to continue reading Waebrania. You can also adjust the font size for comfortable reading and browse other books of the Bible using the navigation links.

https://www.youtube.com/watch?v=rzsT_Q3KLzE

More Resources

Continue Reading the Bible

Continue reading Waebrania Chapter 8 and explore every book, chapter and verse of the Holy Bible. Use the navigation links above and below to move through the Scriptures with ease.

Frequently Asked Questions

What is Waebrania Chapter 8?

Waebrania Chapter 8 is part of the Book of Waebrania in the Holy Bible.

Can I read this chapter online?

Yes. You can read the complete Waebrania Chapter 8 online for free with easy chapter navigation.

More Chapters from Agano Jipya

  1. Waebrania Chapter 5
  2. Waebrania Chapter 1
  3. Waebrania Chapter 6
  4. Waebrania Chapter 4
  5. Ufunuo wa Yohana Chapter 1
  6. Waebrania Chapter 11
  7. Waebrania Chapter 10

Explore More from waebrania

  1. Waebrania Chapter 10
  2. Waebrania Chapter 9
  3. Waebrania Chapter 2
  4. Waebrania Chapter 11
  5. Waebrania Chapter 4
  6. Waebrania Chapter 13
  7. Waebrania Chapter 7

Related Chapters & Readings

  1. Mika Chapter 2
  2. Mambo ya Walawi Chapter 21
  3. Danieli Chapter 2
  4. Kumbukumbu la Torati Chapter 9
  5. Mwanzo Chapter 30
  6. Zaburi Chapter 22
  7. Waefeso Chapter 1
Share Your Love

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *