Mambo ya Walawi Chapter 21

For English

Read Mambo ya Walawi Chapter 21 Online

Read Mambo ya Walawi Chapter 21 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of Mambo ya Walawi in the Old Testament. Browse every verse with easy chapter navigation, continue to the next chapter, or explore the complete Book of Mambo ya Walawi and the Holy Bible online.

Choose a Chapter

Mambo ya Walawi 21

Sura 21

1. Kisha Bwana akamwambia Musa, Nena na hao makuhani, wana wa Haruni, uwaambie, Mtu asijinajisi kwa ajili ya wafu katika watu wake;

2. isipokuwa ni kwa ajili ya jamaa yake wa karibu, kwa ajili ya mama yake, na kwa ajili baba yake, na kwa ajili ya mwanawe, na kwa ajili ya binti yake, na kwa ajili ya nduguye mwanamume;

3. na kwa ajili ya umbu lake aliye mwanamwali, aliye wa udugu kwake, ambaye hajaolewa na mume; ana ruhusa kujitia unajisi kwa ajili yake huyo.

4. Asijitie unajisi, ijapokuwa ni mkubwa katika watu wake, hata akajinajisi.

5. Wasijifanyie upaa kichwani, wala wasinyoe pembe za ndevu zao, wala wasichanje chale katika miili yao.

6. Watakuwa watakatifu kwa Mungu wao, wala wasilinajisi jina la Mungu wao; kwa kuwa wao ndio wasongezao sadaka za Bwana kwa njia ya moto, chakula cha Mungu wao; kwa ajili ya hayo watakuwa watakatifu.

7. Wasimwoe mwanamke aliye kahaba, au huyo aliye mwenye unajisi; wala wasimwoe mwanamke aliyeachwa na mumewe; kwa kuwa yeye kuhani ni mtakatifu kwa Mungu wake.

8. Kwa hiyo basi utamtakasa; kwa kuwa yeye husongeza chakula cha Mungu wako; atakuwa mtakatifu kwako wewe; kwa kuwa mimi Bwana niwatakasaye ninyi ni mtakatifu.

9. Na binti ya kuhani ye yote atakapojitia unajisi kwa ukahaba, amemtia unajisi baba yake; atachomwa moto.

10. Na yeye aliye kuhani mkuu katika nduguze, ambaye mafuta ya kutiwa yamemiminwa kichwani mwake, naye akawekwa wakfu ili ayavae hayo mavazi, yeye hataziacha wazi nywele za kichwa chake, wala hatazirarua nguo zake;

11. wala hataingia penye maiti, wala asijitie unajisi kwa ajili ya baba yake wala mama yake;

12. wala asitoke katika mahali patakatifu, wala asipatie unajisi mahali patakatifu pa Mungu wake; kwa kuwa utakaso wa hayo mafuta ya kutiwa ya Mungu wake u juu yake; mimi ndimi Bwana.

13. Naye atamwoa mwanamke katika ubikira wake.

14. Asitwae mjane, wala mwanamke aliyeachwa na mumewe, wala mwanamke mwenye unajisi, wala kahaba; lakini atamwoa mwanamwali katika watu wake mwenyewe.

15. Naye asiwatie unajisi kizazi chake katika watu wake; kwa kuwa mimi ndimi Bwana nimtakasaye.

16. Kisha Bwana akanena na Musa, na kumwambia,

17. Nena na Haruni, umwambie, Mtu awaye yote wa kizazi chako wewe katika vizazi vyao, aliye na kilema, asikaribie kusongeza chakula cha Mungu wake.

18. Kwa kuwa mtu awaye yote aliye na kilema hatakaribia; mtu kipofu, au kiwete, au mtu aliye na pua iliyoharibika, au aliye na kitu kilichozidi vimpasavyo mwili,

19. au mtu aliyevunjika mguu, au aliyevunjika mkono,

20. au aliye na kijongo, au aliye kibeti, au aliye na kilema cha jichoni, au aliye na upele, au mwenye buba, au aliyevunjika mapumbu;

21. mtu awaye yote wa kizazi cha Haruni kuhani aliye na kilema asikaribie kuzisongeza sadaka za Bwana kwa njia ya moto; ana kilema huyo asikaribie kusongeza chakula cha Mungu wake.

22. Atakula chakula cha Mungu wake, katika hicho kilicho kitakatifu sana, na hicho kilicho kitakatifu.

23. Lakini hataingia ndani ya pazia, wala asikaribie madhabahu, kwa sababu ana kilema; ili kwamba asipanajisi patakatifu pangu; kwa kuwa mimi ndimi Bwana niwatakasaye.

24. Basi Musa akanena na Haruni na wanawe, na wana wa Israeli wote.

About Mambo ya Walawi Chapter 21

Read Mambo ya Walawi Chapter 21 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of Mambo ya Walawi in the Old Testament. Continue reading with the chapter navigation above or explore the complete book.

Book Information

Book: Mambo ya Walawi
Chapter: 21
Testament: Old Testament

How to Read this Chapter

Use the Previous and Next Chapter buttons to continue reading Mambo ya Walawi. You can also adjust the font size for comfortable reading and browse other books of the Bible using the navigation links.

https://www.youtube.com/watch?v=rzsT_Q3KLzE

More Resources

Continue Reading the Bible

Continue reading Mambo ya Walawi Chapter 21 and explore every book, chapter and verse of the Holy Bible. Use the navigation links above and below to move through the Scriptures with ease.

Frequently Asked Questions

What is Mambo ya Walawi Chapter 21?

Mambo ya Walawi Chapter 21 is part of the Book of Mambo ya Walawi in the Holy Bible.

Can I read this chapter online?

Yes. You can read the complete Mambo ya Walawi Chapter 21 online for free with easy chapter navigation.

More Chapters from Agano la Kale

  1. Zaburi Chapter 1
  2. Habakuki Chapter 3
  3. Ayubu Chapter 1
  4. Zaburi Chapter 2
  5. Ayubu Chapter 4
  6. Kutoka Chapter 11
  7. Kutoka Chapter 2

Explore More from mambo-ya-walawi

  1. Mambo ya Walawi Chapter 3
  2. Mambo ya Walawi Chapter 16
  3. Mambo ya Walawi Chapter 9
  4. Mambo ya Walawi Chapter 6
  5. Mambo ya Walawi Chapter 25
  6. Mambo ya Walawi Chapter 13
  7. Mambo ya Walawi Chapter 17

Related Chapters & Readings

  1. Kutoka Chapter 16
  2. Matendo ya Mitume Chapter 1
  3. Ayubu Chapter 22
  4. Hesabu Chapter 30
  5. Mwanzo Chapter 26
  6. Marko Chapter 14
  7. Amosi Chapter 2
Share Your Love

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *