Read Waebrania Chapter 2 Online
Read Waebrania Chapter 2 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of Waebrania in the New Testament. Browse every verse with easy chapter navigation, continue to the next chapter, or explore the complete Book of Waebrania and the Holy Bible online.
Choose a Chapter
Waebrania 2
Sura 2
1. Kwa hiyo imetupasa kuyaangalia zaidi hayo yaliyosikiwa tusije tukayakosa.
2. Kwa maana, ikiwa lile neno lililonenwa na malaika lilikuwa imara, na kila kosa na uasi ulipata ujira wa haki,
3. sisi je! Tutapataje kupona, tusipojali wokovu mkuu namna hii? Ambao kwanza ulinenwa na Bwana, kisha ukathibitika kwetu na wale waliosikia;
4. Mungu naye akishuhudu pamoja nao kwa ishara na ajabu na nguvu za namna nyingi, na kwa magawanyo ya Roho Mtakatifu, kama alivyopenda mwenyewe.
5. Maana hakuuweka chini ya malaika ulimwengu ule ujao tunaounena, ila mtu mmoja ameshuhudia hivi mahali fulani, akisema,
6. Mwanadamu ni nini hata umkumbuke, Ama mwana wa binadamu, hata umwangalie?
7. Umemfanya mdogo punde kuliko malaika, Umemvika taji ya utukufu na heshima, Umemtawaza juu ya kazi za mikono yako;
8. Umeweka vitu vyote chini ya nyayo zake. Kwa maana katika kuweka vitu vyote chini yake hakusaza kitu kisichowekwa chini yake. Lakini sasa bado hatujaona vitu vyote kutiwa chini yake.
9. ila twamwona yeye aliyefanywa mdogo punde kuliko malaika, yaani, Yesu, kwa sababu ya maumivu ya mauti, amevikwa taji ya utukufu na heshima, ili kwa neema ya Mungu aionje mauti kwa ajili ya kila mtu.
10. Kwa kuwa ilimpasa yeye, ambaye kwa ajili yake na kwa njia yake vitu vyote vimekuwapo, akileta wana wengi waufikilie utukufu, kumkamilisha kiongozi mkuu wa wokovu wao kwa njia ya mateso.
11. Maana yeye atakasaye na hao wanaotakaswa wote pia watoka kwa mmoja. Kwa ajili hii haoni haya kuwaita ndugu zake;
12. akisema, Nitalihubiri jina lako kwa ndugu zangu; Katikati ya kanisa nitakuimbia sifa.
13. Na tena, Nitakuwa nimemtumaini yeye. Na tena, Tazama, mimi nipo hapa na watoto niliopewa na Mungu.
14. Basi, kwa kuwa watoto wameshiriki damu na mwili, yeye naye vivyo hivyo alishiriki yayo hayo, ili kwa njia ya mauti amharibu yeye aliyekuwa na nguvu za mauti, yaani, Ibilisi,
15. awaache huru wale ambao kwamba maisha yao yote kwa hofu ya mauti walikuwa katika hali ya utumwa.
16. Maana ni hakika, hatwai asili ya malaika, ila atwaa asili ya mzao wa Ibrahimu.
17. Hivyo ilimpasa kufananishwa na ndugu zake katika mambo yote, apate kuwa kuhani mkuu mwenye rehema, mwaminifu katika mambo ya Mungu, ili afanye suluhu kwa dhambi za watu wake.
18. Na kwa kuwa mwenyewe aliteswa alipojaribiwa, aweza kuwasaidia wao wanaojaribiwa.
About Waebrania Chapter 2
Read Waebrania Chapter 2 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of Waebrania in the New Testament. Continue reading with the chapter navigation above or explore the complete book.
Book Information
Book: Waebrania
Chapter: 2
Testament: New Testament
How to Read this Chapter
Use the Previous and Next Chapter buttons to continue reading Waebrania. You can also adjust the font size for comfortable reading and browse other books of the Bible using the navigation links.
More Resources
Continue Reading the Bible
Continue reading Waebrania Chapter 2 and explore every book, chapter and verse of the Holy Bible. Use the navigation links above and below to move through the Scriptures with ease.
Frequently Asked Questions
What is Waebrania Chapter 2?
Waebrania Chapter 2 is part of the Book of Waebrania in the Holy Bible.
Can I read this chapter online?
Yes. You can read the complete Waebrania Chapter 2 online for free with easy chapter navigation.
More Chapters from Agano Jipya
- Waebrania Chapter 1
- Waebrania Chapter 5
- Waebrania Chapter 6
- Waebrania Chapter 4
- Ufunuo wa Yohana Chapter 15
- Ufunuo wa Yohana Chapter 8
- Ufunuo wa Yohana Chapter 1
Explore More from waebrania
- Waebrania Chapter 13
- Waebrania Chapter 8
- Waebrania Chapter 3
- Waebrania Chapter 4
- Waebrania Chapter 9
- Waebrania Chapter 5
- Waebrania Chapter 1