1 Wakorintho Chapter 5

For English

Read 1 Wakorintho Chapter 5 Online

Read 1 Wakorintho Chapter 5 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of 1 Wakorintho in the New Testament. Browse every verse with easy chapter navigation, continue to the next chapter, or explore the complete Book of 1 Wakorintho and the Holy Bible online.

Choose a Chapter

1 Wakorintho 5

Sura 5

1. Yakini habari imeenea ya kuwa kwenu kuna zinaa, na zinaa ya namna isiyokuwako hata katika Mataifa, kwamba mtu awe na mke wa babaye.

2. Nanyi mwajivuna, wala hamkusikitika, ili kwamba aondolewe miongoni mwenu huyo aliyetenda jambo hilo.

3. Kwa maana kweli, nisipokuwapo kwa mwili, lakini nikiwapo kwa roho, mimi mwenyewe nimekwisha kumhukumu yeye aliyetenda jambo hilo, kana kwamba nikiwapo.

4. Katika jina la Bwana wetu Yesu, ninyi mkiwa mmekusanyika pamoja na roho yangu, pamoja na uweza wa Bwana wetu Yesu;

5. kumtolea Shetani mtu huyo, ili mwili uadhibiwe, ili na roho iokolewe katika siku ya Bwana Yesu.

6. Kujisifu kwenu si kuzuri. Hamjui kwamba chachu kidogo hulichachusha donge zima?

7. Basi, jisafisheni, mkatoe ile chachu ya kale, mpate kuwa donge jipya, kama vile mlivyo hamkutiwa chachu. Kwa maana Pasaka wetu amekwisha kutolewa kuwa sadaka, yaani, Kristo;

8. basi na tuifanye karamu, si kwa chachu ya kale, wala kwa chachu ya uovu na ubaya, bali kwa yasiyochachika, ndio weupe wa moyo na kweli.

9. Naliwaandikia katika waraka wangu, kwamba msichangamane na wazinzi.

10. Sisemi msichangamane kabisa na wazinzi wa dunia hii, au na wenye kutamani, au na wanyang'anyi, au na wenye kuabudu sanamu; maana hapo ingewalazimu kutoka katika dunia.

11. Lakini, mambo yalivyo, naliwaandikia kwamba msichangamane na mtu aitwaye ndugu, akiwa ni mzinzi au mwenye kutamani au mwenye kuabudu sanamu au mtukanaji au mlevi au mnyang'anyi; mtu wa namna hii msikubali hata kula naye.

12. Maana yanihusu nini kuwahukumu wale walio nje? Ninyi hamwahukumu hao walio ndani?

13. Lakini hao walio nje Mungu atawahukumu. Ninyi mwondoeni yule mbaya miongoni mwenu.

About 1 Wakorintho Chapter 5

Read 1 Wakorintho Chapter 5 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of 1 Wakorintho in the New Testament. Continue reading with the chapter navigation above or explore the complete book.

Book Information

Book: 1 Wakorintho
Chapter: 5
Testament: New Testament

How to Read this Chapter

Use the Previous and Next Chapter buttons to continue reading 1 Wakorintho. You can also adjust the font size for comfortable reading and browse other books of the Bible using the navigation links.

https://www.youtube.com/watch?v=rzsT_Q3KLzE

More Resources

Continue Reading the Bible

Continue reading 1 Wakorintho Chapter 5 and explore every book, chapter and verse of the Holy Bible. Use the navigation links above and below to move through the Scriptures with ease.

Frequently Asked Questions

What is 1 Wakorintho Chapter 5?

1 Wakorintho Chapter 5 is part of the Book of 1 Wakorintho in the Holy Bible.

Can I read this chapter online?

Yes. You can read the complete 1 Wakorintho Chapter 5 online for free with easy chapter navigation.

More Chapters from 1-wakorintho

  1. 1 Wakorintho Chapter 14
  2. 1 Wakorintho Chapter 2
  3. 1 Wakorintho Chapter 11
  4. 1 Wakorintho Chapter 8
  5. 1 Wakorintho Chapter 1
  6. 1 Wakorintho Chapter 16
  7. 1 Wakorintho Chapter 15

Explore More from Agano Jipya

  1. 2 Petro Chapter 2
  2. 1 Timotheo Chapter 4
  3. Warumi Chapter 7
  4. Luka Chapter 10
  5. Luka Chapter 22
  6. Matendo ya Mitume Chapter 13
  7. 2 Wakorintho Chapter 6

Related Chapters & Readings

  1. Warumi Chapter 15
  2. Mhubiri Chapter 5
  3. Waebrania Chapter 3
  4. Hosea Chapter 11
  5. Kutoka Chapter 10
  6. Zaburi Chapter 14
  7. 1 Wakorintho Chapter 4
Share Your Love

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *