Waefeso Chapter 6

For English

Read Waefeso Chapter 6 Online

Read Waefeso Chapter 6 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of Waefeso in the New Testament. Browse every verse with easy chapter navigation, continue to the next chapter, or explore the complete Book of Waefeso and the Holy Bible online.

Choose a Chapter

Waefeso 6

Sura 6

1. Enyi watoto, watiini wazazi wenu katika Bwana, maana hii ndiyo haki.

2. Waheshimu baba yako na mama yako; amri hii ndiyo amri ya kwanza yenye ahadi,

3. Upate heri, ukae siku nyingi katika dunia.

4. Nanyi, akina baba, msiwachokoze watoto wenu; bali waleeni katika adabu na maonyo ya Bwana.

5. Enyi watumwa, watiini wao walio bwana zenu kwa jinsi ya mwili, kwa hofu na kutetemeka, kwa unyofu wa moyo, kana kwamba ni kumtii Kristo;

6. wala si kwa utumwa wa macho tu kama wajipendekazao kwa wanadamu bali kama watumwa wa Kristo, mkitenda yampendezayo Mungu kwa moyo;

7. kwa nia njema kama kumtumikia Bwana wala si mwanadamu;

8. mkijua ya kuwa kila neno jema alitendalo mtu atapewa lilo hilo na Bwana kwamba ni mtumwa au kwamba ni huru.

9. Nanyi, akina bwana, watendeeni wao yayo hayo, mkiacha kuwaogofya, huku mkijua ya kuwa yeye aliye Bwana wao na wenu yuko mbinguni, wala kwake hakuna upendeleo.

10. Hatimaye, mzidi kuwa hodari katika Bwana na katika uweza wa nguvu zake.

11. Vaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kuzipinga hila za Shetani.

12. Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho.

13. Kwa sababu hiyo twaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kushindana siku ya uovu, na mkiisha kuyatimiza yote, kusimama.

14. Basi simameni, hali mmejifunga kweli viunoni, na kuvaa dirii ya haki kifuani,

15. na kufungiwa miguu utayari tupatao kwa Injili ya amani;

16. zaidi ya yote mkiitwaa ngao ya imani, ambayo kwa hiyo mtaweza kuizima mishale yote yenye moto ya yule mwovu.

17. Tena ipokeeni chapeo ya wokovu, na upanga wa Roho ambao ni neno la Mungu;

18. kwa sala zote na maombi mkisali kila wakati katika Roho, mkikesha kwa jambo hilo na kudumu katika kuwaombea watakatifu wote;

19. pia na kwa ajili yangu mimi, nipewe usemi kwa kufumbua kinywa changu, ili niihubiri kwa ujasiri ile siri ya Injili;

20. ambayo kwa ajili yake mimi ni mjumbe katika minyororo; hata nipate ujasiri katika huyo kunena jinsi inipasavyo kunena.

21. Basi ninyi nanyi mpate kuzijua habari zangu, ni hali gani, Tikiko, ndugu mpendwa, mhudumu mwaminifu katika Bwana, atawajulisheni mambo yote;

22. ambaye nampeleka kwenu kwa kusudi lilo hilo mpate kuzijua habari zetu, naye awafariji mioyo yenu.

23. Amani na iwe kwa ndugu, na pendo, pamoja na imani, zitokazo kwa Mungu Baba na kwa Bwana Yesu Kristo.

24. Neema na iwe pamoja na wote wampendao Bwana wetu Yesu Kristo katika hali ya kutokuharibika.

About Waefeso Chapter 6

Read Waefeso Chapter 6 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of Waefeso in the New Testament. Continue reading with the chapter navigation above or explore the complete book.

Book Information

Book: Waefeso
Chapter: 6
Testament: New Testament

How to Read this Chapter

Use the Previous and Next Chapter buttons to continue reading Waefeso. You can also adjust the font size for comfortable reading and browse other books of the Bible using the navigation links.

https://www.youtube.com/watch?v=rzsT_Q3KLzE

More Resources

Continue Reading the Bible

Continue reading Waefeso Chapter 6 and explore every book, chapter and verse of the Holy Bible. Use the navigation links above and below to move through the Scriptures with ease.

Frequently Asked Questions

What is Waefeso Chapter 6?

Waefeso Chapter 6 is part of the Book of Waefeso in the Holy Bible.

Can I read this chapter online?

Yes. You can read the complete Waefeso Chapter 6 online for free with easy chapter navigation.

More Chapters from Agano Jipya

  1. Waebrania Chapter 1
  2. Waebrania Chapter 5
  3. Waebrania Chapter 6
  4. Waebrania Chapter 4
  5. Waebrania Chapter 2
  6. Ufunuo wa Yohana Chapter 15
  7. Ufunuo wa Yohana Chapter 8

Explore More from waefeso

  1. Waefeso Chapter 5
  2. Waefeso Chapter 2
  3. Waefeso Chapter 3
  4. Waefeso Chapter 4
  5. Waefeso Chapter 1

Related Chapters & Readings

  1. Tito Chapter 3
  2. 1 Wafalme Chapter 11
  3. Hesabu Chapter 23
  4. Maombolezo Chapter 5
  5. Hesabu Chapter 26
  6. Mwanzo Chapter 7
  7. Wagalatia Chapter 3
Share Your Love

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *