Read Waebrania Chapter 9 Online
Read Waebrania Chapter 9 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of Waebrania in the New Testament. Browse every verse with easy chapter navigation, continue to the next chapter, or explore the complete Book of Waebrania and the Holy Bible online.
Choose a Chapter
Waebrania 9
Sura 9
1. Basi hata agano la kwanza lilikuwa na kawaida za ibada, na patakatifu pake, pa kidunia.
2. Maana hema ilitengenezwa, ile ya kwanza, mlimokuwa na kinara cha taa, na meza, na mikate ya Wonyesho; ndipo palipoitwa, Patakatifu.
3. Na nyuma ya pazia la pili, ile hema iitwayo Patakatifu pa patakatifu,
4. yenye chetezo cha dhahabu, na sanduku la agano lililofunikwa kwa dhahabu pande zote, mlimokuwa na kopo la dhahabu lenye ile mana, na ile fimbo ya Haruni iliyochipuka, na vile vibao vya agano;
5. na juu yake makerubi ya utukufu, yakikitia kivuli kiti cha rehema; basi hatuna nafasi sasa ya kueleza habari za vitu hivi kimoja kimoja.
6. Basi, vitu hivi vikiisha kutengenezwa hivyo, makuhani huingia katika hema hiyo ya kwanza daima, wakiyatimiza mambo ya ibada.
7. Lakini katika hema hiyo ya pili kuhani mkuu huingia peke yake, mara moja kila mwaka; wala si pasipo damu, atoayo kwa ajili ya nafsi yake na kwa dhambi za kutokujua za hao watu.
8. Roho Mtakatifu akionyesha neno hili, ya kwamba njia ya kupaingia patakatifu ilikuwa haijadhihirishwa bado, hapo hema ya kwanza ilipokuwa ingali ikisimama;
9. ambayo ndiyo mfano wa wakati huu uliopo sasa; wakati huo sadaka na dhabihu zinatolewa, zisizoweza kwa jinsi ya dhambi kumkamilisha mtu aabuduye,
10. kwa kuwa ni sheria za jinsi ya mwili tu, vyakula na vinywaji na kutawadha kwingine kwingine, zilizoamriwa hata wakati wa matengenezo mapya.
11. Lakini Kristo akiisha kuja, aliye kuhani mkuu wa mambo mema yatakayokuwapo, kwa hema iliyo kubwa na kamilifu zaidi, isiyofanyika kwa mikono, maana yake, isiyo ya ulimwengu huu,
12. wala si kwa damu ya mbuzi na ndama, bali kwa damu yake mwenyewe aliingia mara moja tu katika Patakatifu, akiisha kupata ukombozi wa milele.
13. Kwa maana, ikiwa damu ya mbuzi na mafahali na majivu ya ndama ya ng'ombe waliyonyunyiziwa wenye uchafu hutakasa hata kuusafisha mwili;
14. basi si zaidi damu yake Kristo, ambaye kwamba kwa Roho wa milele alijitoa nafsi yake kwa Mungu kuwa sadaka isiyo na mawaa, itawasafisha dhamiri zenu na matendo mafu, mpate kumwabudu Mungu aliye hai?
15. Na kwa sababu hii ni mjumbe wa agano jipya, ili, mauti ikiisha kufanyika kwa kukomboa makosa yaliyokuwa chini ya agano la kwanza, hao walioitwa waipokee ahadi ya urithi wa milele.
16. Maana agano la urithi lilipo, lazima iwepo mauti yake aliyelifanya.
17. Kwa maana agano la urithi lina nguvu palipotukia kufa kwa mtu; kwa kuwa halina nguvu kabisa, akiwa yu hai yeye aliyelifanya.
18. Kwa hiyo hata lile la kwanza halikuanzwa pasipo damu.
19. Maana kila amri ilipokwisha kunenwa na Musa kwa hao watu wote, kama ilivyoamuru sheria, aliitwaa damu ya ndama na ya mbuzi, pamoja na maji na sufu nyekundu na hisopo, akakinyunyizia kitabu chenyewe, na watu wote,
20. akisema, Hii ni damu ya agano mliloamriwa na Mungu.
21. Na ile hema nayo na vyombo vyote vya ibada alivinyunyizia damu vivyo hivyo.
22. Na katika Torati karibu vitu vyote husafishwa kwa damu, na pasipo kumwaga damu hakuna ondoleo.
23. Basi ilikuwa sharti nakala za mambo yaliyo mbinguni zisafishwe kwa hizo, lakini mambo ya mbinguni yenyewe yasafishwe kwa dhabihu zilizo bora kuliko hizo.
24. Kwa sababu Kristo hakuingia katika patakatifu palipofanyika kwa mikono, ndio mfano wa patakatifu halisi; bali aliingia mbinguni hasa, aonekane sasa usoni pa Mungu kwa ajili yetu;
25. wala si kwamba ajitoe mara nyingi, kama vile kuhani mkuu aingiavyo katika patakatifu kila mwaka kwa damu isiyo yake;
26. kama ni hivyo, ingalimpasa kuteswa mara nyingi tangu kuwekwa msingi wa ulimwengu; lakini sasa, mara moja tu, katika utimilifu wa nyakati, amefunuliwa, azitangue dhambi kwa dhabihu ya nafsi yake.
27. Na kama vile watu wanavyowekewa kufa mara moja, na baada ya kufa hukumu;
28. kadhalika Kristo naye, akiisha kutolewa sadaka mara moja azichukue dhambi za watu wengi; atatokea mara ya pili, pasipo dhambi, kwa hao wamtazamiao kwa wokovu.
About Waebrania Chapter 9
Read Waebrania Chapter 9 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of Waebrania in the New Testament. Continue reading with the chapter navigation above or explore the complete book.
Book Information
Book: Waebrania
Chapter: 9
Testament: New Testament
How to Read this Chapter
Use the Previous and Next Chapter buttons to continue reading Waebrania. You can also adjust the font size for comfortable reading and browse other books of the Bible using the navigation links.
More Resources
Continue Reading the Bible
Continue reading Waebrania Chapter 9 and explore every book, chapter and verse of the Holy Bible. Use the navigation links above and below to move through the Scriptures with ease.
Frequently Asked Questions
What is Waebrania Chapter 9?
Waebrania Chapter 9 is part of the Book of Waebrania in the Holy Bible.
Can I read this chapter online?
Yes. You can read the complete Waebrania Chapter 9 online for free with easy chapter navigation.
More Chapters from Agano Jipya
- Waebrania Chapter 5
- Waebrania Chapter 2
- Yohana Chapter 1
- Waebrania Chapter 3
- Waebrania Chapter 11
- Waebrania Chapter 8
- Waebrania Chapter 6
Explore More from waebrania
- Waebrania Chapter 4
- Waebrania Chapter 12
- Waebrania Chapter 7
- Waebrania Chapter 2
- Waebrania Chapter 6
- Waebrania Chapter 13
- Waebrania Chapter 5