Waefeso Chapter 1

For English

Read Waefeso Chapter 1 Online

Read Waefeso Chapter 1 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of Waefeso in the New Testament. Browse every verse with easy chapter navigation, continue to the next chapter, or explore the complete Book of Waefeso and the Holy Bible online.

Choose a Chapter

Waefeso 1

Sura 1

1. Paulo, mtume wa Kristo Yesu, kwa mapenzi ya Mungu; kwa watakatifu walioko [Efeso] wanaomwamini Kristo Yesu.

2. Neema na iwe kwenu na amani zitokazo kwa Mungu Baba yetu na kwa Bwana Yesu Kristo.

3. Atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, aliyetubariki kwa baraka zote za rohoni, katika ulimwengu wa roho, ndani yake Kristo;

4. kama vile alivyotuchagua katika yeye kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu, ili tuwe watakatifu, watu wasio na hatia mbele zake katika pendo.

5. Kwa kuwa alitangulia kutuchagua, ili tufanywe wanawe kwa njia ya Yesu Kristo, sawasawa na uradhi wa mapenzi yake.

6. Na usifiwe utukufu wa neema yake, ambayo ametuneemesha katika huyo Mpendwa.

7. Katika yeye huyo, kwa damu yake, tunao ukombozi wetu, masamaha ya dhambi, sawasawa na wingi wa neema yake.

8. Naye alituzidishia hiyo katika hekima yote na ujuzi;

9. akiisha kutujulisha siri ya mapenzi yake, sawasawa na uradhi wake, alioukusudia katika yeye huyo.

10. Yaani, kuleta madaraka ya wakati mkamilifu atavijumlisha vitu vyote katika Kristo, vitu vya mbinguni na vitu vya duniani pia. Naam, katika yeye huyo;

11. na ndani yake sisi nasi tulifanywa urithi, huku tukichaguliwa tangu awali sawasawa na kusudi lake yeye, ambaye hufanya mambo yote kwa shauri la mapenzi yake.

12. Nasi katika huyo tupate kuwa sifa ya utukufu wake, sisi tuliotangulia kumwekea Kristo tumaini letu.

13. Nanyi pia katika huyo mmekwisha kulisikia neno la kweli, habari njema za wokovu wenu; tena mmekwisha kumwamini yeye, na kutiwa muhuri na Roho yule wa ahadi aliye Mtakatifu.

14. Ndiye aliye arabuni ya urithi wetu, ili kuleta ukombozi wa milki yake, kuwa sifa ya utukufu wake.

15. Kwa sababu hiyo mimi nami, tangu nilipopata habari za imani yenu katika Bwana Yesu, na pendo lenu kwa watakatifu wote,

16. siachi kutoa shukrani kwa ajili yenu; nikiwakumbuka katika sala zangu,

17. Mungu wa Bwana wetu Yesu Kristo, Baba wa utukufu, awape ninyi roho ya hekima na ya ufunuo katika kumjua yeye;

18. macho ya mioyo yenu yatiwe nuru, mjue tumaini la mwito wake jinsi lilivyo; na utajiri wa utukufu wa urithi wake katika watakatifu jinsi ulivyo;

19. na ubora wa ukuu wa uweza wake ndani yetu tuaminio jinsi ulivyo; kwa kadiri ya utendaji wa nguvu za uweza wake;

20. aliotenda katika Kristo alipomfufua katika wafu, akamweka mkono wake wa kuume katika ulimwengu wa roho;

21. juu sana kuliko ufalme wote, na mamlaka, na nguvu, na usultani, na kila jina litajwalo, wala si ulimwenguni humu tu, bali katika ule ujao pia;

22. akavitia vitu vyote chini ya miguu yake, akamweka awe kichwa juu ya vitu vyote kwa ajili ya kanisa; ambalo

23. ndilo mwili wake, ukamilifu wake anayekamilika kwa vyote katika vyote.

About Waefeso Chapter 1

Read Waefeso Chapter 1 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of Waefeso in the New Testament. Continue reading with the chapter navigation above or explore the complete book.

Book Information

Book: Waefeso
Chapter: 1
Testament: New Testament

How to Read this Chapter

Use the Previous and Next Chapter buttons to continue reading Waefeso. You can also adjust the font size for comfortable reading and browse other books of the Bible using the navigation links.

https://www.youtube.com/watch?v=rzsT_Q3KLzE

More Resources

Continue Reading the Bible

Continue reading Waefeso Chapter 1 and explore every book, chapter and verse of the Holy Bible. Use the navigation links above and below to move through the Scriptures with ease.

Frequently Asked Questions

What is Waefeso Chapter 1?

Waefeso Chapter 1 is part of the Book of Waefeso in the Holy Bible.

Can I read this chapter online?

Yes. You can read the complete Waefeso Chapter 1 online for free with easy chapter navigation.

More Chapters from Agano Jipya

  1. Waebrania Chapter 5
  2. Waebrania Chapter 1
  3. Waebrania Chapter 6
  4. Waebrania Chapter 4
  5. Ufunuo wa Yohana Chapter 1
  6. Waebrania Chapter 11
  7. Waebrania Chapter 10

Explore More from waefeso

  1. Waefeso Chapter 2
  2. Waefeso Chapter 4
  3. Waefeso Chapter 6
  4. Waefeso Chapter 3
  5. Waefeso Chapter 5

Related Chapters & Readings

  1. Ezekieli Chapter 18
  2. Mathayo Chapter 18
  3. 1 Samweli Chapter 5
  4. Yoshua Chapter 9
  5. Ezekieli Chapter 35
  6. Zaburi Chapter 75
  7. Zaburi Chapter 132
Share Your Love

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *