Ufunuo wa Yohana Chapter 6

For English

Read Ufunuo wa Yohana Chapter 6 Online

Read Ufunuo wa Yohana Chapter 6 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of Ufunuo wa Yohana in the New Testament. Browse every verse with easy chapter navigation, continue to the next chapter, or explore the complete Book of Ufunuo wa Yohana and the Holy Bible online.

Choose a Chapter

Ufunuo wa Yohana 6

Sura 6

1. Kisha nikaona napo Mwana-Kondoo alipofungua moja ya zile muhuri saba, nikasikia mmoja wa wale wenye uhai wanne akisema, kama kwa sauti ya ngurumo, Njoo!

2. Nikaona, na tazama, farasi mweupe, na yeye aliyempanda ana uta, akapewa taji, naye akatoka, ali akishinda tena apate kushinda.

3. Na alipoifungua muhuri ya pili, nikamsikia yule mwenye uhai wa pili akisema, Njoo!

4. Akatoka farasi mwingine, mwekundu sana, na yeye aliyempanda alipewa kuiondoa amani katika nchi, ili watu wauane, naye akapewa upanga mkubwa.

5. Na alipoifungua muhuri ya tatu, nikamsikia yule wa tatu mwenye uhai akisema, Njoo! Nikaona, na tazama, farasi mweusi, na yeye aliyempanda ana mizani mkononi mwake.

6. Nikasikia kama sauti katikati ya hao wenye uhai wanne, ikisema, Kibaba cha ngano kwa nusu rupia, na vibaba vitatu vya shayiri kwa nusu rupia, wala usiyadhuru mafuta wala divai.

7. Na alipoifungua muhuri ya nne, nikasikia sauti ya yule mwenye uhai wa nne akisema, Njoo!

8. Nikaona, na tazama, farasi wa rangi ya kijivujivu, na yeye aliyempanda jina lake ni Mauti, na Kuzimu akafuatana naye. Nao wakapewa mamlaka juu ya robo ya nchi, waue kwa upanga na kwa njaa na kwa tauni na kwa hayawani wa nchi.

9. Na alipoifungua muhuri ya tano, nikaona chini ya madhabahu roho zao waliochinjwa kwa ajili ya neno la Mungu, na kwa ajili ya ushuhuda waliokuwa nao.

10. Wakalia kwa sauti kuu, wakisema, Ee Mola, Mtakatifu, Mwenye kweli, hata lini kutokuhukumu, wala kuipatia haki damu yetu kwa hao wakaao juu ya nchi?

11. Nao wakapewa kila mmoja nguo ndefu, nyeupe, wakaambiwa wastarehe bado muda mchache, hata itakapotimia hesabu ya wajoli wao na ndugu zao, watakaouawa vile vile kama wao.

12. Nami nikaona, alipoifungua muhuri ya sita, palikuwa na tetemeko kuu la nchi; jua likawa jeusi kama gunia la singa, mwezi wote ukawa kama damu,

13. na nyota zikaanguka juu ya nchi kama vile mtini upukutishavyo mapooza yake, utikiswapo na upepo mwingi.

14. Mbingu zikaondolewa kama ukurasa ulivyokunjwa, na kila mlima na kisiwa kikahamishwa kutoka mahali pake.

15. Na wafalme wa dunia, na wakuu, na majemadari, na matajiri, na wenye nguvu, na kila mtumwa, na mwungwana, wakajificha katika pango na chini ya miamba ya milima,

16. wakiiambia milima na miamba, Tuangukieni, tusitirini, mbele za uso wake yeye aketiye juu ya kiti cha enzi, na hasira ya Mwana-Kondoo.

17. Kwa maana siku iliyo kuu, ya hasira yao, imekuja; naye ni nani awezaye kusimama?

About Ufunuo wa Yohana Chapter 6

Read Ufunuo wa Yohana Chapter 6 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of Ufunuo wa Yohana in the New Testament. Continue reading with the chapter navigation above or explore the complete book.

Book Information

Book: Ufunuo wa Yohana
Chapter: 6
Testament: New Testament

How to Read this Chapter

Use the Previous and Next Chapter buttons to continue reading Ufunuo wa Yohana. You can also adjust the font size for comfortable reading and browse other books of the Bible using the navigation links.

https://www.youtube.com/watch?v=rzsT_Q3KLzE

More Resources

Continue Reading the Bible

Continue reading Ufunuo wa Yohana Chapter 6 and explore every book, chapter and verse of the Holy Bible. Use the navigation links above and below to move through the Scriptures with ease.

Frequently Asked Questions

What is Ufunuo wa Yohana Chapter 6?

Ufunuo wa Yohana Chapter 6 is part of the Book of Ufunuo wa Yohana in the Holy Bible.

Can I read this chapter online?

Yes. You can read the complete Ufunuo wa Yohana Chapter 6 online for free with easy chapter navigation.

More Chapters from Agano Jipya

  1. Waebrania Chapter 1
  2. Waebrania Chapter 5
  3. Waebrania Chapter 6
  4. Waebrania Chapter 4
  5. Ufunuo wa Yohana Chapter 1
  6. Waebrania Chapter 3
  7. Waebrania Chapter 2

Explore More from ufunuo-wa-yohana

  1. Ufunuo wa Yohana Chapter 7
  2. Ufunuo wa Yohana Chapter 19
  3. Ufunuo wa Yohana Chapter 12
  4. Ufunuo wa Yohana Chapter 2
  5. Ufunuo wa Yohana Chapter 14
  6. Ufunuo wa Yohana Chapter 11
  7. Ufunuo wa Yohana Chapter 20

Related Chapters & Readings

  1. Mithali Chapter 4
  2. Yoshua Chapter 3
  3. Matendo ya Mitume Chapter 2
  4. Ayubu Chapter 37
  5. Isaya Chapter 37
  6. 1 Timotheo Chapter 1
  7. Danieli Chapter 6
Share Your Love

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *