1 Timotheo Chapter 1

For English

Read 1 Timotheo Chapter 1 Online

Read 1 Timotheo Chapter 1 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of 1 Timotheo in the New Testament. Browse every verse with easy chapter navigation, continue to the next chapter, or explore the complete Book of 1 Timotheo and the Holy Bible online.

Choose a Chapter

1 Timotheo 1

Sura 1

1. Paulo, mtume wa Kristo Yesu, kwa amri ya Mungu Mwokozi wetu na Kristo Yesu, taraja letu;

2. kwa Timotheo, mwanangu hasa katika imani. Neema na iwe kwako, na rehema, na amani, zitokazo kwa Mungu Baba na kwa Kristo Yesu Bwana wetu.

3. Kama vile nilivyokusihi ukae Efeso, nilipokuwa nikisafiri kwenda Makedonia, ili uwakataze wengine wasifundishe elimu nyingine;

4. wala wasiangalie hadithi na nasaba zisizo na ukomo, ziletazo maswali wala si madaraka ya Mungu yaliyo katika imani; basi ufanye hivyo.

5. Walakini mwisho wa agizo hilo ni upendo utokao katika moyo safi na dhamiri njema, na imani isiyo na unafiki.

6. Wengine wakiyakosa hayo wamegeukia maneno ya ubatili;

7. wapenda kuwa waalimu wa sheria, ingawa hawayafahamu wasemayo wala mambo yale wayanenayo kwa uthabiti.

8. Lakini twajua ya kuwa sheria ni njema, kama mtu akiitumia kwa njia iliyo halali;

9. akilifahamu neno hili, ya kuwa sheria haimhusu mtu wa haki, bali waasi, na wasio wataratibu, na makafiri, na wenye dhambi, na wanajisi, na wasiomcha Mungu, na wapigao baba zao, na wapigao mama zao, na wauaji,

10. na wazinifu, na wafiraji, na waibao watu, na waongo, nao waapao kwa uongo; na likiwapo neno lo lote linginelo lisilopatana na mafundisho yenye uzima;

11. kama vile ilivyonenwa katika Habari Njema ya utukufu wa Mungu ahimidiwaye, niliyowekewa amana.

12. Nami namshukuru Kristo Yesu Bwana wetu, aliyenitia nguvu kwa sababu aliniona kuwa mwaminifu, akaniweka katika utumishi wake;

13. ingawa hapo kwanza nalikuwa mtukanaji, mwenye kuudhi watu, mwenye jeuri, lakini nalipata rehema kwa kuwa nalitenda hivyo kwa ujinga, na kwa kutokuwa na imani.

14. Na neema ya Bwana wetu ilizidi sana, pamoja na imani na pendo lililo katika Kristo Yesu.

15. Ni neno la kuaminiwa, tena lastahili kukubalika kabisa, ya kwamba Kristo Yesu alikuja ulimwenguni awaokoe wenye dhambi; ambao wa kwanza wao ni mimi.

16. Lakini kwa ajili hii nalipata rehema, ili katika mimi wa kwanza, Yesu Kristo audhihirishe uvumilivu wake wote; niwe kielelezo kwa wale watakaomwamini baadaye, wapate uzima wa milele.

17. Sasa kwa Mfalme wa milele, asiyeweza kuona uharibifu, asiyeonekana, Mungu peke yake, na iwe heshima na utukufu milele na milele. Amina.

18. Mwanangu Timotheo, nakukabidhi agizo hilo liwe akiba, kwa ajili ya maneno ya unabii yaliyotangulia juu yako, ili katika hayo uvipige vile vita vizuri;

19. uwe mwenye imani na dhamiri njema, ambayo wengine wameisukumia mbali, wakaangamia kwa habari ya Imani.

20. Katika hao wamo Himenayo na Iskanda, ambao nimempa Shetani watu hao, ili wafundishwe wasimtukane Mungu.

About 1 Timotheo Chapter 1

Read 1 Timotheo Chapter 1 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of 1 Timotheo in the New Testament. Continue reading with the chapter navigation above or explore the complete book.

Book Information

Book: 1 Timotheo
Chapter: 1
Testament: New Testament

How to Read this Chapter

Use the Previous and Next Chapter buttons to continue reading 1 Timotheo. You can also adjust the font size for comfortable reading and browse other books of the Bible using the navigation links.

https://www.youtube.com/watch?v=rzsT_Q3KLzE

More Resources

Continue Reading the Bible

Continue reading 1 Timotheo Chapter 1 and explore every book, chapter and verse of the Holy Bible. Use the navigation links above and below to move through the Scriptures with ease.

Frequently Asked Questions

What is 1 Timotheo Chapter 1?

1 Timotheo Chapter 1 is part of the Book of 1 Timotheo in the Holy Bible.

Can I read this chapter online?

Yes. You can read the complete 1 Timotheo Chapter 1 online for free with easy chapter navigation.

More Chapters from 1-timotheo

  1. 1 Timotheo Chapter 3
  2. 1 Timotheo Chapter 6
  3. 1 Timotheo Chapter 4
  4. 1 Timotheo Chapter 5
  5. 1 Timotheo Chapter 2

Explore More from Agano Jipya

  1. Luka Chapter 20
  2. Ufunuo wa Yohana Chapter 8
  3. 1 Yohana Chapter 3
  4. Waebrania Chapter 3
  5. Matendo ya Mitume Chapter 1
  6. Matendo ya Mitume Chapter 15
  7. Marko Chapter 12

Related Chapters & Readings

  1. Zaburi Chapter 15
  2. Yeremia Chapter 31
  3. Kutoka Chapter 33
  4. Mambo ya Walawi Chapter 11
  5. Yeremia Chapter 25
  6. Nahumu Chapter 2
  7. 1 Wathesalonike Chapter 4
Share Your Love

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *