Read Ufunuo wa Yohana Chapter 5 Online
Read Ufunuo wa Yohana Chapter 5 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of Ufunuo wa Yohana in the New Testament. Browse every verse with easy chapter navigation, continue to the next chapter, or explore the complete Book of Ufunuo wa Yohana and the Holy Bible online.
Choose a Chapter
Ufunuo wa Yohana 5
Sura 5
1. Kisha nikaona katika mkono wa kuume wake yeye aliyeketi juu ya kile kiti cha enzi kitabu kilichoandikwa ndani na nyuma, kimetiwa muhuri saba.
2. Nikaona malaika mwenye nguvu akihubiri kwa sauti kuu, N'nani astahiliye kukifungua kitabu, na kuzivunja muhuri zake?
3. Wala hapakuwa na mtu mbinguni, wala juu ya nchi, wala chini ya nchi, aliyeweza kukifungua hicho kitabu, wala kukitazama.
4. Nami nikalia sana kwa kuwa hapakuonekana mtu astahiliye kukifungua hicho kitabu, wala kukitazama.
5. Na mmojawapo wa wale wazee akaniambia, Usilie; tazama, Simba aliye wa kabila ya Yuda, Shina la Daudi, yeye ameshinda apate kukifungua kile kitabu, na zile muhuri zake saba.
6. Nikaona katikati ya kile kiti cha enzi na wale wenye uhai wanne, na katikati ya wale wazee, Mwana-Kondoo amesimama, alikuwa kana kwamba amechinjwa, mwenye pembe saba na macho saba, ambazo ni Roho saba za Mungu zilizotumwa katika dunia yote.
7. Akaja, akakitwaa kile kitabu katika mkono wa kuume wake yeye aliyeketi juu ya kile kiti cha enzi.
8. Hata alipokitwaa kile kitabu, hao wenye uhai wanne na wale wazee ishirini na wanne wakaanguka mbele za Mwana-Kondoo, kila mmoja wao ana kinubi, na vitasa vya dhahabu vilivyojaa manukato, ambayo ni maombi ya watakatifu.
9. Nao waimba wimbo mpya wakisema, Wastahili wewe kukitwaa hicho kitabu na kuzifungua muhuri zake; kwa kuwa ulichinjwa, ukamnunulia Mungu kwa damu yako watu wa kila kabila na lugha na jamaa na taifa,
10. ukawafanya kuwa ufalme na makuhani kwa Mungu wetu; nao wanamiliki juu ya nchi.
11. Nikaona nikasikia sauti ya malaika wengi pande zote za kile kiti cha enzi, na za wale wenye uhai, na za wale wazee, na hesabu yao ilikuwa elfu kumi mara elfu kumi na elfu mara elfu,
12. wakisema kwa sauti kuu, Astahili Mwana-Kondoo aliyechinjwa, kuupokea uweza na utajiri na hekima na nguvu na heshima na utukufu na baraka.
13. Na kila kiumbe kilichoko mbinguni na juu ya nchi na chini ya nchi ya juu ya bahari, na vitu vyote vilivyomo ndani yake, nalivisikia, vikisema, Baraka na heshima na utukufu na uweza una yeye aketiye juu ya kiti cha enzi, na yeye Mwana-Kondoo, hata milele na milele.
14. Na wale wenye uhai wanne wakasema, Amina. Na wale wazee wakaanguka, wakasujudu.
About Ufunuo wa Yohana Chapter 5
Read Ufunuo wa Yohana Chapter 5 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of Ufunuo wa Yohana in the New Testament. Continue reading with the chapter navigation above or explore the complete book.
Book Information
Book: Ufunuo wa Yohana
Chapter: 5
Testament: New Testament
How to Read this Chapter
Use the Previous and Next Chapter buttons to continue reading Ufunuo wa Yohana. You can also adjust the font size for comfortable reading and browse other books of the Bible using the navigation links.
More Resources
Continue Reading the Bible
Continue reading Ufunuo wa Yohana Chapter 5 and explore every book, chapter and verse of the Holy Bible. Use the navigation links above and below to move through the Scriptures with ease.
Frequently Asked Questions
What is Ufunuo wa Yohana Chapter 5?
Ufunuo wa Yohana Chapter 5 is part of the Book of Ufunuo wa Yohana in the Holy Bible.
Can I read this chapter online?
Yes. You can read the complete Ufunuo wa Yohana Chapter 5 online for free with easy chapter navigation.
More Chapters from Agano Jipya
- Waebrania Chapter 1
- Waebrania Chapter 5
- Waebrania Chapter 6
- Waebrania Chapter 4
- Waebrania Chapter 3
- Waebrania Chapter 2
- Yohana Chapter 1
Explore More from ufunuo-wa-yohana
- Ufunuo wa Yohana Chapter 14
- Ufunuo wa Yohana Chapter 15
- Ufunuo wa Yohana Chapter 11
- Ufunuo wa Yohana Chapter 13
- Ufunuo wa Yohana Chapter 10
- Ufunuo wa Yohana Chapter 3
- Ufunuo wa Yohana Chapter 2