Matendo ya Mitume Chapter 11

For English

Read Matendo ya Mitume Chapter 11 Online

Read Matendo ya Mitume Chapter 11 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of Matendo ya Mitume in the New Testament. Browse every verse with easy chapter navigation, continue to the next chapter, or explore the complete Book of Matendo ya Mitume and the Holy Bible online.

Choose a Chapter

Matendo ya Mitume 11

Sura 11

1. Basi mitume na ndugu waliokuwako katika Uyahudi wakapata habari ya kwamba watu wa Mataifa nao wamelipokea neno la Mungu.

2. Na Petro alipopanda kwenda Yerusalemu, wale walio wa tohara wakashindana naye,

3. wakisema, Uliingia kwa watu wasiotahiriwa ukala nao.

4. Petro akaanza kuwaeleza kwa taratibu, akasema,

5. Nalikuwa katika mji wa Yafa, nikiomba, roho yangu ikazimia, nikaona maono; chombo kinashuka, kama nguo kubwa inatelemshwa kutoka mbinguni kwa pembe zake nne, kikanifikilia.

6. Nikakitazama sana, nikifikiri, nikaona wanyama wa nchi wenye miguu minne, na wanyama wa mwituni, nao watambaao, na ndege wa angani.

7. Nikasikia na sauti ikiniambia, Ondoka, Petro, ukachinje ule.

8. Nikasema, Hasha, Bwana, kwa maana kitu kilicho kichafu au kilicho najisi hakijaingia kabisa kinywani mwangu.

9. Sauti ikanijibu mara ya pili kutoka mbinguni, Alivyovitakasa Mungu, usivinene wewe najisi.

10. Jambo hili likatendeka mara tatu, kisha vitu vyote vikavutwa tena juu mbinguni.

11. Na tazama, mara hiyo watu watatu wakasimama mbele ya nyumba tuliyokuwamo, waliotumwa kwangu kutoka Kaisaria.

12. Roho akaniambia nifuatane nao, nisione tashwishi. Ndugu hawa sita nao wakaenda pamoja nami, tukaingia katika nyumba ya mtu yule;

13. akatueleza jinsi alivyomwona malaika aliyesimama nyumbani mwake na kumwambia, Tuma watu kwenda Yafa ukamwite Simoni aitwaye Petro,

14. atakayekuambia maneno ambayo yatakuokoa, wewe na nyumba yako yote.

15. Ikawa nilipoanza kunena, Roho Mtakatifu akawashukia kama alivyotushukia sisi mwanzo.

16. Nikalikumbuka neno lile la Bwana, jinsi alivyosema, Yohana alibatiza kwa maji kweli, bali ninyi mtabatizwa kwa Roho Mtakatifu.

17. Basi ikiwa Mwenyezi Mungu amewapa wao karama ile ile aliyotupa sisi tuliomwamini Bwana Yesu Kristo, mimi ni nani niweze kumpinga Mungu?

18. Waliposikia maneno haya wakanyamaza, wakamtukuza Mungu, wakisema, Basi, Mungu amewajalia hata mataifa nao toba liletalo uzima.

19. Basi wale waliotawanyika kwa sababu ya ile dhiki iliyotukia kwa habari ya Stefano, wakasafiri hata Foinike na Kipro na Antiokia, wasilihubiri lile neno ila kwa Wayahudi peke yao.

20. Lakini baadhi ya hao walikuwa watu wa Kipro na Kirene, nao walipofika Antiokia wakasema na Wayahudi wa Kiyunani, wakihubiri habari njema za Bwana Yesu.

21. Mkono wa Bwana ukawa pamoja nao, watu wengi wakaamini, wakamwelekea Bwana.

22. Habari hizo za watu hao zikafika masikioni mwa kanisa lililokuwako katika Yerusalemu; wakamtuma Barnaba, aende hata Antiokia.

23. Naye, alipokwisha kufika na kuiona neema ya Mungu akafurahi, akawasihi wote waambatane na Bwana kwa kusudi la moyo.

24. Maana alikuwa mtu mwema amejaa Roho Mtakatifu na imani; watu wengi wakaongezeka upande wa Bwana.

25. Kisha akatoka akaenda Tarso kumtafuta Sauli;

26. hata alipokwisha kumwona akamleta Antiokia. Ikawa kwa muda wa mwaka mzima wakakusanyika pamoja na kanisa na kuwafundisha watu wengi. Na wanafunzi waliitwa Wakristo kwanza hapo Antiokia.

27. Siku zizo hizo manabii walitelemka kutoka Yerusalemu hata Antiokia.

28. Na tulipokusanyika akasimama mmoja wao, jina lake Agabo, akaonyesha kwa uweza wa Roho Mtakatifu kwamba njaa kubwa itakuja karibu katika dunia nzima, nayo ikatukia katika siku za Klaudio.

29. Na wale wanafunzi, kila mtu kwa kadiri ya alivyofanikiwa, wakaazimu kupeleka msaada kwa ndugu zao waliokaa Uyahudi.

30. Wakafanya hivyo, wakawapelekea wazee kwa mikono ya Barnaba na Sauli.

About Matendo ya Mitume Chapter 11

Read Matendo ya Mitume Chapter 11 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of Matendo ya Mitume in the New Testament. Continue reading with the chapter navigation above or explore the complete book.

Book Information

Book: Matendo ya Mitume
Chapter: 11
Testament: New Testament

How to Read this Chapter

Use the Previous and Next Chapter buttons to continue reading Matendo ya Mitume. You can also adjust the font size for comfortable reading and browse other books of the Bible using the navigation links.

https://www.youtube.com/watch?v=rzsT_Q3KLzE

More Resources

Continue Reading the Bible

Continue reading Matendo ya Mitume Chapter 11 and explore every book, chapter and verse of the Holy Bible. Use the navigation links above and below to move through the Scriptures with ease.

Frequently Asked Questions

What is Matendo ya Mitume Chapter 11?

Matendo ya Mitume Chapter 11 is part of the Book of Matendo ya Mitume in the Holy Bible.

Can I read this chapter online?

Yes. You can read the complete Matendo ya Mitume Chapter 11 online for free with easy chapter navigation.

More Chapters from Agano Jipya

  1. Waebrania Chapter 1
  2. Waebrania Chapter 5
  3. Waebrania Chapter 6
  4. Waebrania Chapter 4
  5. Waebrania Chapter 3
  6. Waebrania Chapter 2
  7. Yohana Chapter 1

Explore More from matendo-ya-mitume

  1. Matendo ya Mitume Chapter 9
  2. Matendo ya Mitume Chapter 7
  3. Matendo ya Mitume Chapter 27
  4. Matendo ya Mitume Chapter 8
  5. Matendo ya Mitume Chapter 22
  6. Matendo ya Mitume Chapter 12
  7. Matendo ya Mitume Chapter 17

Related Chapters & Readings

  1. Isaya Chapter 2
  2. 1 Samweli Chapter 29
  3. Matendo ya Mitume Chapter 3
  4. Yoshua Chapter 17
  5. Ayubu Chapter 13
  6. Isaya Chapter 28
  7. 1 Mambo ya Nyakati Chapter 7
Share Your Love

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *