Ufunuo wa Yohana Chapter 19

For English

Read Ufunuo wa Yohana Chapter 19 Online

Read Ufunuo wa Yohana Chapter 19 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of Ufunuo wa Yohana in the New Testament. Browse every verse with easy chapter navigation, continue to the next chapter, or explore the complete Book of Ufunuo wa Yohana and the Holy Bible online.

Choose a Chapter

Ufunuo wa Yohana 19

Sura 19

1. Baada ya hayo nikasikia sauti kama sauti ya makutano mengi, sauti kubwa mbinguni, ikisema, Haleluya; wokovu na utukufu na nguvu zina BWANA MUNGU wetu.

2. kwa kuwa hukumu zake ni za kweli na za haki; maana amemhukumu yule kahaba mkuu aliyeiharibu nchi kwa uasherati wake, na kuipatiliza damu ya watumwa wake mkononi mwake.

3. Wakasema mara ya pili, Haleluya. Na moshi wake hupaa juu hata milele na milele.

4. Na wale wazee ishirini na wanne, na wale wenye uhai wanne, wakasujudu na kumwabudu Mungu, aketiye katika kile kiti cha enzi, wakisema, Amina, Haleluya.

5. Sauti ikatoka katika kile kiti cha enzi ikisema, Msifuni Mungu wetu, enyi watumwa wake wote, ninyi mnaomcha, wadogo kwa wakuu.

6. Nikasikia sauti kama sauti ya makutano mengi, na kama sauti ya maji mengi, na kama sauti ya radi yenye nguvu, ikisema, Haleluya; kwa kuwa Bwana Mungu wetu, Mwenyezi, amemiliki.

7. Na tufurahi, tukashangilie, tukampe utukufu wake; kwa kuwa arusi ya Mwana-Kondoo imekuja, na mkewe amejiweka tayari.

8. Naye amepewa kuvikwa kitani nzuri, ing'arayo, safi; kwa maana kitani nzuri hiyo ni matendo ya haki ya watakatifu.

9. Naye akaniambia, Andika, Heri walioalikwa karamu ya arusi ya Mwana-Kondoo. Akaniambia, Maneno haya ni maneno ya kweli ya Mungu.

10. Nami nikaanguka mbele ya miguu yake, ili nimsujudie; akaniambia, Angalia, usifanye hivi; mimi ni mjoli wako na wa ndugu zako walio na ushuhuda wa Yesu. Msujudie Mungu. Kwa maana ushuhuda wa Yesu ndio roho ya unabii.

11. Kisha nikaziona mbingu zimefunuka, na tazama, farasi mweupe, na yeye aliyempanda, aitwaye Mwaminifu na Wa-kweli, naye kwa haki ahukumu na kufanya vita.

12. Na macho yake yalikuwa kama mwali wa moto, na juu ya kichwa chake vilemba vingi; naye ana jina lililoandikwa, asilolijua mtu ila yeye mwenyewe.

13. Naye amevikwa vazi lililochovywa katika damu, na jina lake aitwa, Neno la Mungu.

14. Na majeshi yaliyo mbinguni wakamfuata, wamepanda farasi weupe na kuvikwa kitani nzuri, nyeupe, safi.

15. Na upanga mkali hutoka kinywani mwake ili awapige mataifa kwa huo. Naye atawachunga kwa fimbo ya chuma, naye anakanyaga shinikizo la mvinyo ya ghadhabu ya hasira ya Mungu Mwenyezi.

16. Naye ana jina limeandikwa katika vazi lake na paja lake, MFALME WA WAFALME, NA Bwana WA MABwana.

17. Kisha nikaona malaika mmoja amesimama katika jua; akalia kwa sauti kuu, akiwaambia ndege wote warukao katikati ya mbingu, Njoni mkutane kwa karamu ya Mungu iliyo kuu;

18. mpate kula nyama ya wafalme, na nyama ya majemadari, na nyama ya watu hodari, na nyama ya farasi na ya watu wawapandao, na nyama ya watu wote, waungwana kwa watumwa, wadogo kwa wakubwa.

19. Kisha nikamwona huyo mnyama, na wafalme wa nchi, na majeshi yao, wamekutana kufanya vita na yeye aketiye juu ya farasi yule, tena na majeshi yake.

20. Yule mnyama akakamatwa, na yule nabii wa uongo pamoja naye, yeye aliyezifanya hizo ishara mbele yake, ambazo kwa hizo aliwadanganya watu wale walioipokea ile chapa ya huyo mnyama, nao walioisujudia sanamu yake; hao wawili wakatupwa wangali hai katika lile ziwa la moto liwakalo kwa kiberiti;

21. na wale waliosalia waliuawa kwa upanga wake yeye aliyeketi juu ya yule farasi, upanga utokao katika kinywa chake. Na ndege wote wakashiba kwa nyama zao.

About Ufunuo wa Yohana Chapter 19

Read Ufunuo wa Yohana Chapter 19 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of Ufunuo wa Yohana in the New Testament. Continue reading with the chapter navigation above or explore the complete book.

Book Information

Book: Ufunuo wa Yohana
Chapter: 19
Testament: New Testament

How to Read this Chapter

Use the Previous and Next Chapter buttons to continue reading Ufunuo wa Yohana. You can also adjust the font size for comfortable reading and browse other books of the Bible using the navigation links.

https://www.youtube.com/watch?v=rzsT_Q3KLzE

More Resources

Continue Reading the Bible

Continue reading Ufunuo wa Yohana Chapter 19 and explore every book, chapter and verse of the Holy Bible. Use the navigation links above and below to move through the Scriptures with ease.

Frequently Asked Questions

What is Ufunuo wa Yohana Chapter 19?

Ufunuo wa Yohana Chapter 19 is part of the Book of Ufunuo wa Yohana in the Holy Bible.

Can I read this chapter online?

Yes. You can read the complete Ufunuo wa Yohana Chapter 19 online for free with easy chapter navigation.

More Chapters from Agano Jipya

  1. Waebrania Chapter 3
  2. Yohana Chapter 1
  3. Waebrania Chapter 5
  4. Waebrania Chapter 2
  5. Waebrania Chapter 12
  6. Waebrania Chapter 6
  7. Ufunuo wa Yohana Chapter 8

Explore More from ufunuo-wa-yohana

  1. Ufunuo wa Yohana Chapter 6
  2. Ufunuo wa Yohana Chapter 14
  3. Ufunuo wa Yohana Chapter 18
  4. Ufunuo wa Yohana Chapter 22
  5. Ufunuo wa Yohana Chapter 1
  6. Ufunuo wa Yohana Chapter 7
  7. Ufunuo wa Yohana Chapter 13

Related Chapters & Readings

  1. Mwanzo Chapter 6
  2. 2 Wafalme Chapter 9
  3. Ezra Chapter 9
  4. 2 Wafalme Chapter 18
  5. Yoshua Chapter 17
  6. Kutoka Chapter 23
  7. Zaburi Chapter 124
Share Your Love

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *